Kiswahili Paper 3 Question Paper
KCSE CLUSTER TESTS 25
Kiswahili Paper 3
1. SEHEMU YA A (Alama 20)
FASIHI SIMULIZIa) Eleza maana ya miviga kisha uonyeshe inakotumika. (alama 10)
b) Nini umuhimu wa miviga ? (alama 10)
20 marks
SEHEMU YA B (Alama 20)
TamthiliaJibu swali la2 au la 3.
2. Eleza jinsi jina mstahiki Meya ni kinyume na matarajio. (alama 20)
3. ‘’Tumechoka kuumbuliwa. Miaka yote tulifanya kazi na hatuoni matunda yake’’.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza malalamishi ya mzungumzaji na alioandamana nao. (alama 16)
20 marks
SEHEMU YA C. (Alama 20)
RIWAYA : UtenganoUtengano Jibu swali la 4 au la 5.
4. ‘’Sikutaraji kwamba mambo yatokuwa wao kiasi hiki. Tumefuzu shoga’’……………
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama
4) b) Eleza yale mzungumzaji na msemewa waliyokuwa wamefuzu kwayo. (alama 16)
5. Huku ukirejelea riwaya ya utengano, taja na ueleze matatizo kumi yanayokumba mataifa yanayoendelea barani Afrika. (alama 20)
20 marks
SEHEMU YA D (Alama 20)
UshairiJibu swali la 6 au la 7.
6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Abdulatif Abdalla: Chema hakidumu
Chema hakidumu, kingapendekeza,
Saa ikitimu, kitakuteleza
Ukawa na hamu, kukingojeleza
Huwa ni vigumu, kamwe hutaweza
Chema sikiimi, kwamba nakitweza,
Japo mara tumbi, kinshaniliza,
Na japo siombi, kipate n’ongeza,
Mtu haniambi, pa kujikimbiza.
Chema mara ngapi, kiniondoka,
Mwanangu yu wapi ?,
Hakukaa mwaka, Kwa muda mfupi, aliwatilika,
Ningefanya lipi, ela, kumzika?
Chema wangu Poni, kipenzi nyanyangu,
Hadi siku hini, yu moyoni mwangu,
Yu moyoni ndani, hadi kufa kwangu,
Ningemtamani,hatarudi kwangu.
a) Eleza bahari za shairi hili. (al.6)
b) Eleza umbo la beti mbili za mwisho. (al.4)
c) Eleza maudhui ya shairi hili. (al.2)
d) Toa mfano wa matumizi ya mbinu ya tabdila katika shairi hili (al.2)
e) Eleza maana ya maneno haya jinsi yalivyotumiwa
i) Ningemtamani
ii) Kitakuteleza
iii) Kinshaniliza
iv) Ela
v) Alojipa tabu
vi) Hini
7. Weusi likosa nini
1) Sie watu weusi, lipataje weusi?
2) Kila kitu kibaya, hupewa sifa mbaya
3) Sifa hii ‘eusi’, yaleta wasiwasi.
4) Rangi hii hakika, ni wapi litoka?
5) Ibada za mweusi, harusi kuzitusi.
6) Kama mtu mweusi, Lusifa ni mweusi.
7) Ibada ya weupe, hupokewa peupe.
8) Adamu naye Hawa, weupe walipewa
9) Yesu mwana wa Mungu, alikuwa Mzungu.
10) Malaika wa Mungu, daima wazungu.
11) Mweusi ti hatendi, silaumiwe pindi.
12) Mweusi duniani, likosa kitu gani?
13) Mweusi jilaumu, measi yako damu.
14) Mweusi umeiga, hata ya kutoiga.
15) Asojali mkuu, atavunjika guu.
16) Baa mejitakia, nani takulilia ?
a) Hili ni shairi la aina gani ? (al.2)
b) Eleza umbo la shairi hili (al.8)
c) Eleza jinsi mtunzi alivyotumia uhuru wa kishairi (al.6)
d) Eleza maudhui ya shairi hili. (al.4)
20 marks
SEHEMU YA E (Alama 20)
Hadithi fupi-Damu Nyeusi : Ken Walibora
8. ‘’Nani ndugu yako’’ ?
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
b) Eleza dhana waliyokuwa nayo watu wa Marekani kuhusu watu Waafrika. (al. 16)
20 marks