Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 24

Kiswahili Paper 3

1.SEHEMU YA A (Alama 20)

RIWAYA UTENGANO
1.

Kwa kurejelea vipengele vifuatavyo vya matumizi ya lugha, onyesha jinsi mwandishi alivyovitumia kufanikisha maudhui katika Riwaya.
a) Sadfa (alama 10)
b) Uzungumzi nafsia (alama 10)

20 marks

2. SEHEMU YA B (Alama 20)

TAMTHILIA Mstahiki Meya Timothy Arege
2.

‘’Sisi wafanyakazi tuna matatizo mengi yaliyotuzonga kwa muda mrefu. Kwanza mishahara yetu midogo ‘’.
i) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
ii) Taja na ueleze kwa kifupi matatizo mengine yaliyoikabili jamii inayosawiriwa katika tamthilia hii. (alama 8)
iii) Je, utatuzi wake ulikuwaje? (alama 8)
AU

3. a) Jadili sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao kama wanavyojitokeza katika Tamthilia ya ‘’Mstahiki Meya’’.
i) Meya (alama 6)
ii) Siki (alama 6)
b) Kwa kurejelea vipengele vifuatavyo vya matumizi ya lugha, eleza jinsi vilivyofanikisha
maudhui katika tamthilia. (alama 8)
i. Majazi
ii. Utatu

20 marks

3. SEHEMU YA C (Alama 20)

DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE
3.

Kwa kurejelea hadithi zozote tano, jadili maudhui yafuatayo kama yanavyojitokeza katika hadithi hizo. (alama 20)
a) Nafasi ya mwanamke
b) Utamaduni na usasa
c) Mapenzi na athari zake
d) Elimu
Au
. ‘’You !.................Unataka kumbaka dadangu kwa nini?’’
a) Eleza muktadha huu. (alama 4)
b) Eleza maudhui yanayojitokeza katika tukio hili (alama 8)
c) Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
d) Taja sifa zozote nne za mnenewa wa uneni huu. (alama 4)

20 marks

4. SEHEMU YA D (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI
4.

a) Fasihi simulizi ni nini? (alama 2)
b) Eleza tofauti nne baina ya fasihi simulizi na Fasihi andishi (alama 8)
c) Ni nini umuhimu wa Fasihi simulizi ? (alama 10)

20 marks

SEHEMU YA E (Alama 20)

USHAIRI
5.

Soma shairi hili kisha ujibu maswali.
KWELI
1. Neno kweli daima, lina nguvu za kutosha,

Ni silaha ilo uzima, shabaha kutopotosha,
Neno ngome ya heshima, msema kweli hunyosha,
La urongo lapotosha, dumu katika ukweli.


2. Ukitaka taadhima,na lafudha ya kutosha,
Uishi penye huduma, uwe ndiwe muongosha,
Uwe mkweli daima, ukweli wako ondosha,
La urongo lapotosha, dumu katika ukweli.


3. La kweli lina salama, ghayati linaridhisha
Lakuiga mbele na nyuma, na kati lafurahisha
Hata kesini ungama, Mola hatasahalisha
La urongo lapotosha, dumu katika ukweli


4. Ruhusa urongo sema, patatu hakujulisha
Ni kauli ya heshima, wengi wamesadikisha
Ni hadithi twaisoma, nasi tumejifundisha
La urongo lapotosha, dumu katika ukweli.


5. Kwa urongo useme, iwapo wapatanisha
Pili ni mke na mume, ili ndoa kudumisha
Na vitani usikome, ni haki kuhadaisha
La urongo lapotosha, dumu katika ukweli

6. Wasalama kaditama, sitaki kuyurefusha
Waja wa leo si wema, si hoja kuwagutusha
Wathamini darahima, haki wakaziangusha
La urongo lapotosha, dumu katika ukweli

Maswali
a) Taja manufaa ya ukweli kama ilivyoelezwa na mshairi (alama 4)
b) Taja na kutoa mifano ya tamathali mbili za usemi katika shairi (alama 4)
c) Dondoa na ueleze mifano miwili tofauti ya uhuru wa mwandishi katika shairi hili.
(alama 4)
d) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari (alama 4)
e) Eleza maana ya
i) Ghayati (alama 1)
ii) Hata kesini ungama, mola atasahalisha (alama 2)
iii) Wamesadikisha (alama 1)

20 marks

Back Top