Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 24

Kiswahili Paper 2

A. UFAHAMU (Alama 15)

Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata
1.

Uchumi ni mfumo wa mapato na matumizi ya watu katika nchi fulani. Uchumi huu huhusisha sekta mbalimbali kama vile utalii, kilimo, sanaa, miongoni mwa sekta nyingine muhimu. Ukuaji wa kiuchumi hutegemea mambo kadha. Katika nchi zote ulimwenguni, sera za kisiasa huamua jinsi uchumi utakavyokua na kunawiri. Kama siasa hazitilii maanani sera za ukuaji wa kiuchumi, basi mapato ya nchi hiyo hugubikwa katika wingu kubwa la uchochole.

Nchini Kenya, kwa mfano, kuna ulinganifu mkubwa kati ya siasa na ukuaji wa kiuchumi. Ukuaji wa kiuchumi hutegemea uteuzi wa maafisa wanaosirnamia asasi muhimu sana katika usimamizi wa uchumi. Asasi hizi ni kama vile Wizara ya Fedha, Wizara ya Mipango ya Kitaifa na Ruwaza ya 2030, Mamlaka ya Ukusanyaji wa Ushuru (KRA), Benki Kuu ya Kenya (CBK), na Tume ya Kupambana na Ufisadi (KACC). Usimamizi wa asasi hizi huwa muhimu sana katika kuamua hatima ya uchumi wa nchi hii.

Katika mwezi wa Juni kila mwaka, Waziri wa fedha husoma bajeti kwa wabunge. Katika maelezo yake iitwayo nakisi ya bajeti hujitokeza. Kabla ya bajeti kuandaliwa, Wizara ya Mipango huandaa hati iitwayo Usoroveya wa Kiuchumi. Baada ya kusomwa kwa bajeti, ni jukumu la wabunge kupitisha mswada wa kifedha unaohusisha wizara zote au kuutupilia mbali. Jukumu hili linafaa kutekelezwa kufikia tarehe 31 Oktoba ya kila mwaka kulingana na sheria.

Wakati huo huo afisa anayejulikana kama Mhasibu Mkuu wa serikali huwa na jukumu la kuchunguza na kutathmini matumizi ya fedha ya wizara mbalimbali na kutoa ripoti yake kwa Kamati ya Uhasibu wa Umma bungeni (PAC). Kamati hii hutoa mapendekezo yake kwa Mkuu wa Sheria na pia kwa tume ya kupambana na ufisadi ili haki iweze kutekelezwa mahakamani iwapo dosari za kifedha zimefanyika.

Benki kuu ya Kenya kupitia kwa gavana wake huwa na jukumu la kutoa ushauri kwa serikali kuhusu usimamizi wa kifedha, kuchunguza nguvu za shilingi ya Kenya dhidi ya sarafu za kigeni, kutoa sarafu za Kenya kwa umma na usimamizi wa benki zote nchini miongoni mwa majukumu mengine.

Kwa upande mwingine, mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini huwa na jukumu la kuhakikisha kuwa malengo ya ushuru yamefikiwa na pia kuhakikisha kuwa hakuna mtu binafsi au kampuni yoyote inayokwepa kulipa ushuru. Iwapo kuna udanganyifu wowote, basi swala hili linafaa kuangaliwa na mahakama zetu kutekelezwa.

Kwa ujumla, sisi kama wananchi tunafaa kusaidia asasi hizi zote kufikia malengo yake ili tupate ukuaji wa kiuchumi utakaofaidi watu wote. Jambo hili litahakikisha kuwa pengo lililo kali ya walalahoi limezibwa. Sisi kama wananchi, tunafaa kuonyesha uzalendo wetu kwa nchi yetu kwa kulipa ushuru unavyotakikana, tukifuata mwito kuwa KULIPA USHURU NI KUJITEGEMEA. Mwisho tusaidie viongozi wetu katika kuendeleza sera mwafaka za kiuchumi ili nchi yetu ipige hatua kubwa katika ukuaji wa kiuchumi. Iwapo afisa yeyote atatuhumiwa kushiriki katika kashfa yoyote ya kuhujumu nidhamu ya kifedha, basi anafaa kukabiliwa vilivyo kisheria bila kujali hadhi yake ya kijamii au kisiasa.

MASWALI
a. Ipe habari hii kichwa mwafaka. (Alama 1)

.........................................................................................................................................................................................................................

b. Ukuaji wa kiuchumi nchini Kenya hutegemea nini? (Alama 2)

c. Benki kuu ya Kenya ina majukumu yepi? (Alama 3).

d. Pendekeza hatua mbili za kufufua uchumi. (Alama 2)

e. Ufisadi umehujumu vipi ukuaji wa kiuchumi? (Alama 3)

f. Ni vipi wakenya wanaweza kuonyesha uzalendo? (Alama 2)

g. Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika ufahamu: (Alama 3)
i) Hatima………………………………………………………………………………………
ii) Walalahai…………………………………………………………………………………….
iii) Walalahoi ……………………………………………………………………………………

15 marks

B. MUHTASARI (UFUPISHO) (Alama 15)

2.

Taifa lolote lile haliwezi kupiga hatua za kimaendeleo kama halina miundo inayofaa. Nchi nyingi ulimwenguni zimejaribu kujiimarisha kimaendeleo licha ya changamoto zinazozikabili. Mataifa yaliyo katika ulimwengu wa tatu yamekabiliwa na changamoto nyingi kuliko yale yaliyostawi.

Barani Afrika, mataifa mengi Kenya ikiwemo yamepata pigo kubwa. Miongo minne tangu tulipojinyakulia uhuru nchini Kenya imepita, na bado taifa letu lakwamizwa na changamoto si haba. Msingi wa maendelo nchini ni katiba - kitovu cha maendeleo.

Vita vya uhuru nchini vililenga ustawi wa nchi kiuchumi, kisiasa na hata kijamii. Katiba iliyoasisiwa ilikuwa ya kikoloni yenye mfumo wa kikapitalisti ambao uliwanyanyasa wengi. Mfumo huu uliwanufaisha wachache- wenye nchi. Demokrasia haikufuatwa katika ugavi wa rasilmali za nchi. Katiba hii ilitumbukiza nchi katika lindi la maangamizi huku jinamizi la ufisadi likitishia kuipondaponda nchi.

Tunafaa kuuenzi uongozi wa tatu nchini Kenya ambao bila shaka ulichangia pakubwa katika kuchochea mabadiliko nchini katiba ikiwa moja wayo. Simaanishi maongozi tangulizi hayakufanya chochote lakini juhudi za kuleta mabadiliko ya kikatiba zilisombwa na ubinafsi-miongoni mwa viongozi. Hata hivyo ni wimbi la mabadiliko na kiu ya usawa na haki ya kidemokrasia iliyochangia mabadiliko haya. Wanavuguvugu waliotupa katiba kieielezo ambayo kufikia sasa ni katiba mpya walikoleza wino jina la taifa letu kwenye ramani ya dunia. Hili ni kwa kuwa kielelezo cha mataifa bora barani kuthamini demokrasia.

Licha ya maendeleo haya yote ambayo yanatuelekeza katika ruwaza ya kimaendeleo ya 2030, zipo changamoto si haba! Kuwepo vipengele katika katiba mpya ambavyo si wazi ni tishio kuu katika kuafikia malengo ya kimaendeleo. Mfumo wa magatuzi huenda ukawanyima baadhi ya wananchi hisia za kibinadamu hivyo kudai utambulisho mwingine. Mfano bora ni kundi linalojiita 'MRC' huko pwani. Hali hii huenda ikagawanya nchi kwa misingi fulani.

Aidha kipengele cha usawa wa uwakilishi ni pigo kubwa. Suala hili la jinsia limekabiliwa na changamoto huku jinsia moja ikitamalaki taasisi kuu. Hizi ni taasisi zile muhimu.

Siasa za nchi bado zi changa mno kwani viongozi tunaowategemea labda baadhi yao wamelala au kukwama kwenye joto la viti vyao. Hawa wanathamini vitita wanavyovipata na sio wale wanaowawakilisha. Maji yakizidi unga, wao huwa katika mstari wa mbele katika uundaji tume za uchanuzi. Tume hizi huwapa mgawo fulani.

Suala la ardhi na matumizi yake pamoja na mgawo wa fedha za serikali kuu magatuzi ni tatizo kuu. Je, serikali za magatuzi zina mamlaka yapi ambayo hayakinzani na serikali kuu?

Usalama wa taifa ni suala la kupigiwa darubini nchini. Uteuzi wa mkuu wa tume ya polisi nchini pasina kuzingatia taaluma au tajriba katika nyanja hiyo waweza kuathiri utendakazi. Tume zilizoundwa ikiwemo ile ya kuchunguza na kuoanisha mishahara ya wafanyikazi nchini. Pigo kwa tume hizi ni vyama vya wafanyikazi ambavyo havina uwakilishi mzuri. Katika tume hizo tishio kuu ni migomo ya wafanyikazi kwa hofu kuwa mikataba awali na serikali huenda ikapuuzwa.

Matatizo hayo yaweza kutatuliwa kwa kutoa elimu kuhusu katiba kwa kila mkenya. Katiba itafsiriwe kwa lugha rahisi na yenye kueleweka. Katiba ni baba na mama wa taifa

MASWALI

a) Fupisha aya ya pili na ya tatu kwa maneno kati ya 40 -60. (Alama 5)
Matayarisho

................................................................................................................................................................................................................................

Jibu

b) Kwa maneno 40-50 fafanua changamoto kuu katika kuidhinishwa kwa katiba mpya.
(alama 10)

C. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

3.

a) Eleza tofauti ya sauti / th/na/dh/ (Alama 2)

...................................................................................................................................................................................................................................................

b) Taja vipashio vikuu vya lugha. (Alama 2)

...................................................................................................................................................................................................................................................

..................................................................................................................................................................................................................................................

c) Bainisha viambishi na mzizi katika neno ‘wamchiapo’ (Alama 2)

d) i) Eleza matumizi mawili ya ‘po’ (Alama 2)

ii) Tunga sentensi moja tu kudhihirisha matumizi hayo. (Alama 2)

e) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kubadilisha kitenzi kuwa nomino. (Alama 1)
i) Aliadhibiwa kwa kukosa.

...................................................................................................................................................................................................................................................

...................................................................................................................................................................................................................................................

f) Tofautisha matumizi ya ‘ngali’ katika sentensi zifuatazo. (Alama 2)
i) Mueni angali anasoma.

ii) Kerich angalisoma angalipata kazi.

g) Tofautisha kati ya mofimu na viambishi (Alama 2)

h) Tunga sentensi ukitumia, ‘suka’ katika kauli ya kutendata (Alama 1)

...................................................................................................................................................................................................................................................

...................................................................................................................................................................................................................................................

i) Andika maana mbili za sentensi. (Alama 2)
Alimlilia mzaziwe

j) Andika kwa msemo wa taarifa : (Alama 3)
Kasisi aliuliza, “Mtapenda kuombea nini wakati huu wa pasaka?’’ Waumini walimjibu, Tunataka kuombea katiba kwa kuwa tumeingojea kwa muda mrefu”.

...................................................................................................................................................................................................................................................

...................................................................................................................................................................................................................................................

...................................................................................................................................................................................................................................................

...................................................................................................................................................................................................................................................

k) Onyesha kirai nomino na kirai elezi (Alama 2)
Mwalimu aliyetufunza Kiswahili alienda Ulaya jana jioni.

l) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mishale. (Alama 4)
Mvulana mrefu ambaye aliwasili jana ni mwizi hodari.

m) Tunga sentensi mbili kuonyesha maana tofauti za neno ’oza’ (Alama 2)

n) Tumia visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari kuandika upya sentensi ifuatayo. (A1.3)
Ukuta umemuumiza mvulana alipokuwa akiuparaga.

...................................................................................................................................................................................................................................................

...................................................................................................................................................................................................................................................

...................................................................................................................................................................................................................................................

...................................................................................................................................................................................................................................................

o) Taja matumizi matatu ya kibainishi. (Ala.3)

p) Tunga sentensi kwa kutumia kiunganishi kinachoonyesha dhana ya kinyume. (Al. 2)

...................................................................................................................................................................................................................................................

..................................................................................................................................................................................................................................................

...................................................................................................................................................................................................................................................

..................................................................................................................................................................................................................................................

q) Kwa kutoa mifano, taja majukumu matatu ya sentensi. (Alama 3)

40 marks

D. ISIMUJAMII (Alama 10)

4.

a) Matumizi ya lugha katika kila jamii hutegemea mambo kadha ya kimsingi. Eleza matano.
(Alama 5)

........................................................................................................................................................................................................

b) Eleza sifa tano za sajili ya kitaaluma. (Alama 5)

.......................................................................................................................................................................................................

10 marks

Back Top