Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 23

Kiswahili Paper 3

1. SEHEMU A: (Alama 20)

USHAIRI
1.

Lazima.
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
BOUKHEIT AMANA: Huyo si mwenzio


1. Lakini ndugu wendapi, huko uendako siko,
Wenda wala huogopi, ukawaza utokako,
Yule ni mwenzio wapi, sione kile kicheko,
Ndugu yule si mwenzako, wenzako haswa ni sisi.


2. Yule anakuthamini, kwa sababu una kitu,
Usambe akutamani, kwa kuwa mwema wa utu,
Kiwa huna humuoni, atakwacha mwanakwetu,
Asikutishe si mtu, si shani kuwa ni fisi.


3. Atakula yako nyama, na mifupa kuguguna,
Wishapo atakusema, ‘siku hizi wajiona’,
Usuhuba atagoma, wa leo si kama jana,
Hakuoni mtu tena, japo utu hujaasi.


4. Ndugu fikiri vizuri, upate kutaamali,
Yake yeye ni magari, wewe yako basikeli,
Wala sima na achari, yeye maini na wali,
Walani? yeye hajali, kattu hana wasi wasi.
5. Wewe mchunguze sana, ila yake uione,
Naye mukisemezana, yeye aola kwengine,
Huitika na kuguna, hajali muelewane,
Kitambicho si kinene, huna ela kumughasi.


6. Mtovu wa haya kweli, huyo si wa kufuata,
Ikiisha yako mali, guu kwako atakata,
Mutakuwa mbali mbali, kama watu waloteta,
Usingoje kuja juta, kheri tanga ulikisi.

7. Sijitie kushitadi, ukamba waona mbali
Ubora kwenu urudi, utuze yako akili,
Tuishi na yetu jadi, kama siku za awali,
Tushikane kila hali, ya dunia ni mapisi

MASWALI

a) Eleza shabaha ya malenga wa utungo huu (alama 2)
b) Nafsi nenewa ni mtu wa aina gani? Thibitisha (alama 3)
c) Ni bayana kuwa nafsinenwa ni mnafiki asiyetegemewa kamwe. Fafanua.
(alama 3)
d) Kwa kurejelea mifano yoyote miwili, eleza dhima ya uhuru wa ushairi katika shairi hili.
(alama 4)
e) Tambua tamathali zozote mbili ambazo zimetumiwa katika shairi hili.
(alama 2)
f) Andika ubeti wa pili kiriwaya. (alama 4)

g) Thibitisha matumizi ya bahari zifuatazo katika shairi hili (alama 2)
i) Ukaraguni
ii) Sabilia

20 marks

2. SEHEMU YA B (Alama 20)

Tamthilia
2.


Mstahiki Meya: Timothy M. Arege
Jibu swali la 2 au la 3

2. Tamthilia ya Mstahiki Meya inaangazia migogoro mbalimbali baina ya wahusika. Onyesha
mifano ya migogoro inayojitokeza. (alama 20)
AU
3. “Hii harufu mbaya ya taka iliyoupamba mji wetu ni kiwakilishi tu cha uozo ulio ndani”.
a) Weka dondoo hili katika mkutadha wake. (alama 4)
b) Eleza uozo ulio ndani ya baraza la mji wa cheneo. (alama 16)

20 marks

3. SEHEMU YA C (Alama 20)

Riwaya
3.


Kidagaa kimemwozea: Ken walibora.
Jibu swali la 4 au la 5
4. “Damu nzito kuliko maji? Alaa! Falsafa hiyo ndiyo kidonda ndugu cha Bara hili la Afrika.
Hakina dawa”.
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Taja tamathali mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
c) Kwa kutolea mifano saba onyesha ukweli wa falsafa ya damu ni nzito kuliko maji kama
inavyojitokeza katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (alama 14)
Au
5. Mtemi Nasaba Bora alipenda kujiambia kuwa …”aliuua tembo kwa ubua”. Thibitisha ukweli
wa kauli hii ukiirejelea riwaya ya kidagaa kimemwozea. (alama 20)

20 marks

4. SEHEMU YA D (Alama 20)

HADITHI FUPI
4.

Ken Walibora: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 6 au la 7
Said A. Mohammed: Gilasi ya Mwisho Makaburini
6. “Anatutisha kaka, anatutisha sisi kama watoto wadogo, anatutisha kaka”.
a) Tambua muktadha wa dondoo hili. (alama 6)
b) Taja kwa ithibati mbinu mbili za sanaa zinazojitokeza katika dondooo hili.
(alama 4)
c) Fafanua masuala yoyote matano ya kijamii yanayoangaziwa katika hadithi hii.
(alama 10)
Au
7. Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya Damu Nyeusi na hadithi nyingine jadili
nafasi ya mwanamke katika jamii. (alama 20)

20 marks

5. SEHEMU YA E (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI
5.

a) Ushirikina ni nini? (alama 2)
b) Bainisha sifa nne za kimsingi za methali za Kiswahili (alama 4)
c)Eleza dhima zozote saba za semi za Kiswahili. (alama 14)

20 marks

Back Top