Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 20

Kiswahili Paper 3

1.SEHEMU YA A (Alama 20)

RIWAYA
1.

..na sasa matarajio ya Uhuru...
...bado Afrika inatawaliwa...
...inatawaliwa kwa mlango wa nyuma...
(a). Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b). Eleza sifa za msemaji wa maneno haya. (alama 4)
(c). Wakati wa kisa hiki, msemaji na msemewa wanasababisha aina fulani ya utengano. Taja utengano huu na ueleze sababu zake. (alama 4).
(d). Thibitisha madai kwamba uhuru wa wahusika fulani katika riwaya hii bado haujatimia .
(alama 8).

20 marks

2.SEHEMU YA B: (Alama 20)

TAMTHILIA
2.

Basi si kitu.(kimya) wamefika wangapi hii leo?

Wengi
(Akimtazama)wengi?

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(b) Eleza matatizo yaliyowakumba wanaozungumziwa (alama 8)

(c) Je, matatizo haya yalisababishwa na nini? (alama 8)

20 marks

3. SEHEMU YA C: (Alama 20)

HADITHI FUPI.
3.

Diwani ya Damu nyeusi:
Hadithi ya samaki wa nchi za joto ni kinaya. Jadili. (alama 20)

20 marks

4.

au

Basi limemwacha. Basi la abiria ambalo linajuzu kusimama kwenye kila kituo rasmi kama hiki. Limemwacha kwenye baridi ya mzizimo.
(a). Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b). Ni maudhui gani inayochotwa kutokana na muktadha huu. (alama 2)
(c). Eleza jinsi maudhui hayo yalivyoendelezwa kwenye hadithi nzima. (alama 14)

20 marks

4.SEHEMU YA D: (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI
5.

Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe hawa ni kinyonga na mjusi. Kwanza alimtuma kinyonga na kumwagiza akaseme``wanadamu hamtakufa.” Kinyonga alienda kwa mwendo wa kuduwaa, akasimama hapa na pale akila matunda ya mti . Kwa sababu ya hali hii alichelewa sana kufikisha ujumbe kwa banadamu.


Baada ya muda kupita, Mungu alimtuma mjusi na ujumbe akasema,’’Mwanadamu sharti kufa” Mjusi alinyanyua mkia akafyatua, pu! Mbio akawahi duniani kabla ya kinyonga kuwasili. Kwa haraka aliitangaza agizo kuu. “Wanadamu sharti kufa!” Akarejea haraka kwa Mungu. Baada ya muda kinyonga naye akafika duniani na kutangaza, “Wanadamu hamtakufa!”. Wanadamu wakampinga mara na kusema,”La! Tumeshapata ujumbe wa mjusi. Wanadamu sharti kufa! Hatuwezi kupokea tena neno lako!” Basi kulingana na neno la mjusi.Wanadamu hufa.

(a)

(i) Hadithi hii huitwaje? (Alama 1)
(ii) Toa sababu yako. (alama 2)
(b) Eleza sababu tatu zinazohusishwa na ngano za fasihi simulizi katika hadithi hii. (alama 3)
(c) Kinyonga ni mhusika wa aina gani? (alama 3)
(d) Hadithi hii ina umuhimu gani? (alama 4)

(e) Taja njia zozote tatu za kukusanya kazi za fasihi simulizi. (alama 4)

(f) Tambulisha vipera hivi.

(i). kula hepi

(ii).Sema yako ni ya kuazima

(iii). Baba wa taifa (alama 3)

20 marks

6.MAGHANI (Alama 10)

6.

Au
(a) Maghani ni nini? (alama 2)

(b) Eleza fani zifuatazo za maghani.

(i). Vivugo (alama 2)

(ii). Tondozi (alama 2)

(iii). Pembezi (alama 2)

(iv). Rara (alama 2)

(c) Eleza maana ya neno ulumbi. (alama 2)

(d) Bainisha sifa za ulumbi (alama 8)

20 marks

7.SEHEMU YA E: (Alama 10)

SHAIRI
7.

Swali
Dhana ya ufuke imedhihirishwaje katika mashairi haya mawili A na B?

10 marks

Back Top