Kiswahili Paper 3 Question Paper
KCSE CLUSTER TESTS 19
Kiswahili Paper 3
1.SEHEMU A: (Alama 20)
FASIHI SIMULIZIa) Eleza isitilahi zifuatazo za fasihi simulizi. (al.4)
i) Ngomezi
ii) Tarihi
iii) Miviga
iv) Mapisi
b)
i) Misimu ni nini? (al.2)
ii) Taja sifa zozote mbili za misimu. (al.2)
iii) Andika mifano miwili ya misimu . (al. 2)
c) Taja matatizo yoyote matano yanayoikabili Fasihi simulizi katika ulimwengu
wa leo. (al.5)
d) Taja sifa zozote tano za jagina. (al.5)
20 marks
2. SEHEMU B: (Alama 20)
RIWAYA S.A MOHAMED‘’Kumbe bwana wewe mjinga eeh. Yupo mtu asiyejua siasa dunia hii? Wadanganye hao wasiokujua, mimi nakujua vilivyo’’.
a) Eleza muktadha wa maneno haya. (al. 4)
b) Onyesha inavyodhihirika kuwa ‘’hapana asiyejua siasa dunia hii’’. (al.8)
c) Thibitisha kuwa mnenaji anamjua mnenewa vilivyo. (al.8)
20 marks
‘’Msiba wa kujitakia hauna kilio’’.Ukizingatia wahusika wowote watano kutoka riwaya ya ‘’Utengano,’’thibitisha ukweli wa kauli hii. (al.20)
20 marks
3.SEHEMU C: (Alama 20)
TAMTHILIAJadili maudhui yafuatayo kutoka tamthilia ya ‘’Mstahiki Meya’’. (al.20)
i) Uongozi mbaya.
ii) Umaskini.
iii) Utabaka
iv) Usaliti.
v) Ukombozi
20 marks
Au
‘’Ndugu wafanya kazi wenzangu tumefika hapa tukiwa kitu kimoja....tumedhalilishwa vya kutosha....................’’
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
b) Fafanua sabau kuu zilizosababisha tukio linalosababisha maneno haya. (al.4)
c) Eleza jinsi tatizo zima linavyoshughulikiwa kufikia mwishoni mwa tamthilia. (al.12)
20 marks
4.SEHEMU D: (Alama 20)
HADITHI FUPI. Fafanua kikamilifu jinsi maudhui ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi kwa ujumla yanavyoendelezwa katika hadithi ya ‘’Damu Nyeusi.’’
Au
20 marks
‘’Utanioa lini?’’.....alimuuliza. ‘’
Utakapojifungua...................alimjibu.
a) Eleza muktadha wa maneno haya. (al.4)
b) Eleza masaibu yaliyompata aliyeuliza swali na hatima yake. (al.10)
c) Taja na ueleze maovu matatu ya kijamii yaliyoibuka katika hadithi hii. (al.6)
20 marks
5. SEHEMU E: (Alama 20)
USHAIRIa) Linganisha bahari za shairi A na B (al.4)
b) Andika ubeti wa pili wa shairi B kati lugha nathari. (al.4)
c) Taja na utoe mifano miwili ya tamathali za usemi zilizotumika katika mashairi yote mawili. (al.4)
d) Taja na utoe mifano miwili idhini ya mtunzi uliotumika katika mashairi yote mawili. (al.4)
e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika mashairi. (al.4)
i) Ja
ii) Sharuti
iii) Utukufu
iv) Baidi
20 marks