Kiswahili Paper 3 Question Paper
KCSE CLUSTER TESTS 15
Kiswahili Paper 3
SEHEMU YA A (Alama 20)
UshairiSoma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali yanayofuata.
Ni wimbo najimbia, nijaliwe nafusi,
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi,
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi,
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia.
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa,
Hamna nami imani, wala kupanga siasa,
Mwasema sayansini, siko ningali tosa,
Mwanambia niko tosa, kuiva sijafika.
Sasa lishikeni hili, msamiatiwe ninao,
Natohoza Kiswahili, sayansi majina yao,
Kwani neno kemikali, huoni linawafao,
Nimepea nani sasa, huomba linalofaa.
Ela muelewe sana, maamuma na imamu,
Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa tamu,
Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu,
Mujue kuwa mwainama utumwa mwauridhia.
Mzaliwapo mwalia, ‘maa’ maneno ya kwanza,
Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza
Walugha muwe doria, muweze na kuikuza
Sio kujipendekeza, uzungu kuigizia.
Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza
Lugha muliidhamini, Kiswahili kufukiza
Hata kule risavuni, kizungu hamkuwaza
Hata mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia,
Enyi viongozi wetu, ipangeni natharia
Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria,
Lugha hutambusha watu, tuache kuriaria
Sifa ni kwa chake mtu, cha mwizi hutoringia
Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
Msamiati hususa, ni wa Africa yote,
Ni methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilia.
Afrika ndipo petu, pa mabantu halisi,
Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
Warabu na wengi watu, sio wangu
Adinasi Kwao ameomba kiazi, ili kujizidishia.
Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
Kiswahili ni ibara, kila mtu kuimanya,
Methali imetuonya, mtu si mwasilia.
Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
Kukua imeridhia, msamiati kufana
Wengi watajiulia, kwa marefu na mapana
Lugha yetu ya maana, mwaipuuze yalia.
MASWALI
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (al.2)
b) Kwa nini mshairi anasema Kiswahili chalilia? (al.3)
c) Eleza muundo wa shairi hili. (al.5)
d) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa 4 (al.3)
e) Eleza maana inayotokana na mstari ufuatayo. Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Baba na mama ni bantu, shina la wangu ukwasi.
f) Kwa nini mshairi anaupongeza mfumo mpya wa elimu? (al.2)
g) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi (al.3)
i) Nasongwa
ii) Ningali tosa
iii) Dawamu
20 marks
SEHEMU YA B (Alama 20)
TAMTHILIATimothy Arege – MSTAHIKI MEYA
Jibu swali la 2 au 3
2) Fafanua namna asasi na vikundi vifuatavyo vinachangia kuendeleza maovu dhidi ya ummawa cheneo huku ukirejelea tamthilia husika. (al.20)
a) Idara ya polisi
b) Dini
c) Nchi za magharibi
d) Kamati za Barasa la mji
3) “Uvundo haswa! Hata hao wageni sijui wataonaje hali hii. Aibu kubwa inatungoja kama watakujaâ€
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al.4)
b) Fafanua sifa nne za msemaji wa maneno haya. (al.4)
c) Kwa kutolea mfano, taja mbinu moja ya utunzi inayojitokeza katika dondoo hili. (al.2)
d) Mbali na uvundo unaorejelewa katika dondoo, Jadili uvundo mwingine unaojitokeza katika Barasa la Mji wa Cheneo. (al.10)
20 marks
SEHEMU YA C (Alama 20)
RiwayaKen Walibora: KIDAGAA KIMEMWOZEA
4) a) “Kidagaa kimemwozea†ni anwani faafu ya riwaya hii ya kidagaa kimemwozea. Thibitisha ukweli wa usemi huu. (al.10)
b) Kwa kutoa mifano mwafaka, onyesha namna mbinu rejeshi (kisengere nyuma) imetumika katika riwaya hii. (al.10)
20 marks
SEHEMU YA D (Alama 20)
HADITHI FUPIJibu swali la 5 au 6
Ken Walibora: DAMU NYEUSI
5. “Leo ni siku ya siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote hutelezaâ€.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
b) Eleza tamathali za usemi zilizotumika katika dondoo hili (al. 4)
c) Jadili maudhui yanayorejelewa katika dondoo hili. (al. 12)
6. a) Anwani “kanda la Usufi†inaafiki hadithi husikaâ€. Thibitisha. (al. 10)
b) Dhihirisha matumizi ya kinaya katika hadithi ya “Tazamana na mautiâ€. (al.10)
20 marks
SEHEMU YA E (Alama 20)
FASIHI SIMULIZI
Jibu swali la 7 au 8
7. a) Taja sifa zozote nne za maigizo. (al.4)
b) Taja aina zozote nne za maigizo. (al.4)
c) Ni nini tofauti ya maigizo na hadithi? (al.6)
d) Eleza dhima ya maigizo kama utanzu wa fasihi simulizi. (al.6)
8. a) i) Tofautisha kati ya misimu na lakabu. (al.2)
ii) Onyesha dhima ya lakabu katika jamii. (al.6)
iii) Fafanua sifa za misimu (al.6)
b) Eleza matatizo yanayoweza kumkabili mkusanyaji wa data kuhusu Fasihi simulizi nyanjani. (al.6)
20 marks