Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 15

Kiswahili Paper 2

1. UFAHAMU (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
1.

HABARI zisizoridhisha kuhusu shambulizi la kigaidi katika kituo cha biashara cha Westgate, Kaunti ya Nairobi ambapo watu wapatao 67 waliaga dunia na wengine zaidi ya 175 wakaachwa na majeraha, zinaendelea kufichuka. Magazeti yaliangazia habari kwamba mawaziri wanne pamoja na maafisa wakuu wa usalama nchini walipashwa habari za kijasusi kuhusu mipango ya magaidi wa Al-Shabaab kutekeleza shambulizi hilo. Inadaiwa kwamba viongozi hao hawakuchukua hatua za kuzuia shambulizi hilo.

Habari zaidi zilieleza kwamba kituo hicho kilikuwa kinafanyiwa uchunguzi na idara ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) kabla ya kushambuliwa na magaidi. Imeripotiwa kwamba wachunguzaji wa ujasusi walikuwa katika kituo hicho masaa machache kabla ya magaidi hao kufika na kuanza kuwafyatulia risasi walinda usalama, wateja na wafanyabiashara. Inadaiwa wachunguzaji hao 'waliwasiliana' na maafisa wa polisi wanaoshika doria mara kwa mara katika kituo hicho ambacho kimetajwa kuwa miongoni mwa maeneo muhimu sana jijini Nairobi.

Habari hizi zote zinawapa Wakenya ujumbe mmoja; kwamba baadhi ya maafisa wakuu na idara za serikali zilizembea katika majukumu yao ya kuwahakikishia Wakenya na wageni wote wanaozuru Kenya, usalama. Ingawa hatupingi kwamba maafisa hao wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuzembea kazini, jambo muhimu ambalo Wakenya wanataka sasa si lawama bali hakikisho kwamba maisha yao hayapo hatarini wanapoendelea na shughuli zao za kila siku za kuijenga nchi.

Vitisho vilivyotolewa na magaidi hao ambao wamesema wanapanga kutekeleza mashambulizi mengine ndivyo vinavyowakosesha Wakenya Usingizi. Wahenga walisema tusahau yaliyopita na tugange yajayo. Serikali inapaswa kutumia shambulizi la Westgate kama funzo litakalozifanya idara zake za usalama kuamka usingizini na kuhakikisha kwamba Wakenya wasio na hatia hawapotezi tena maisha yao katika mashambulizi kama haya.

Lakini mbona Wakenya nao wasianze kuuthamini usalama wao wenyewe? Hali ya usalama nchini itaimarika maradufu kama Wakenya wote watachakua jukumu la kuwajua vyema majirani wao na kuripoti jambo lolote lisilo la kawaida kwa maafisa wa usalama.

Shambulizi hili lingezuiwa kama Wakenya wangekuwa na mazoea ya kutaka kuwafahamu vyema watu wanaoishi karibu nao kwani inadaiwa kwamba magaidi hawa waliwasili nchini kitambo na kukodisha nyumba ambako waliendeleza mipanga yao. Badala ya kuwalimbikizia lawama polisi, mbona tusishikane nao ili kuhakikisha kwamba watu wenye nia mbaya mitaani mwetu wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria?

MASWALI
a. Toa anwani mwafaka kwa taarifa hii. (al. 1)

................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................................

b. Taja maafa yaliyosababishwa na tukio linalorejelewa. (al. 2) ................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................................

c. Eleza kinaya kinachojitokeza kuhusu tukio la Westgate. (al.4) ................................................................................................................................................................
................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................................

d. Ni nini mtazamo wa mwandishi kuhusuu maafisa wakuu serikalini. (al. 2) ................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................................

e. Ni mambo yapi yanayowatia hofu Wakenya. (al. 2)

................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................................

f. “Tusahau yaliyopita na tugange yajayo”. Thibitisha ukweli wa usemi huu katika kuwahakikishia wakenya usalama. (al. 2) ................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................................

g. Ni hatua zipi zinazoweza kuchukuliwa na wakenya ili kuhakikisha usalama wao. (al. 2) ................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................................

15 marks

2. UFUPISHO (Alama 15)

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
2.

Ugonjwa wa utando wa ubongo ambao kwa kiingereza unafahamika kama ‘meningitis’ huzua hofu miongoni mwa watu wengi. Ugonjwa huo pia hujulikana kama homa ya uti wa mgongo.

Hofu kama hizo zinaeleweka kwa sababu utando wa ubongo ni ugonjwa unaoathiri ngozi inayofunika ubongo na uti wa mgongo na kwa hivyo ni rahisi mno kusababisha kifo ikiwa mgonjwa hatahudumiwa haraka iwezekanavyo.

Utando wa ubongo ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na bacteria. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, utando wa ubongo unaosababishwa na virusi sio hatari sana kwa uhai wa mtu ukilinganishwa na bakteria. Japo watu wengi wanaougua utando wa ubongo hutibiwa na kupona, baadhi yao huachwa wakiwa bubu au vipofu na wengine kufariki.

Shida kubwa ya ugonjwa huu ni kwamba unatokea bila kutarajiwa. Kwa mfano mtoto au mtu wa umri mkubwa anaweza kuwa mzima kwa muda wa dakika kadha ila baadaye kuwa mgonjwa mahututi baada ya kukumbwa na ugonjwa huo. Shida nyingine ya ugomjwa huu ni kwamba huwa vigumu kutenganisha dalili za ugonjwa huu na dalili za magonjwa mengine ya kawaida kama vile maumivu ya kichwa. Kwa
hivyo kuna baadhi ya watu wanaomeza dawa za kupunguza maumivu ya kichwa bila kujua wanaugua utando wa ubongo.

Dalili za watoto wanaougua utando wa ubongo ni homa, kutapika, mtoto kukataa kula na kulia kwa uchungu. Mtoto anayeugua ugonjwa huu kadhalika huwa anaonyesha dalili za kufura kichwa, kupumua kwa haraka na kutupatupa miguu huku mwili wake ukiwa umejikunyata. Watu walio wa umri mkubwa nao huonyesha dalili za maumivu makali ya kichwa, na shingo nzito (stiff neck) na mgonjwa kuepukana na mwangaza. Kadhalika mgonjwa hushikwa na homa na pia kutapika kando na kukosa ufahamu.

Utafiti umeonyesha kwamba watu walio na umri mkubwa kadhalika huonyesha dalili za kuwa na mikono au miguu baridi, maumivu ya misuli na tumbo hasa kutokana na damu kuwa na sumu. Ni muhimu kufahamu kwamba sio kila mtu anahisi dalili hizi. Ikiwa yeyote atashuhudia baadhi ya dalili hizi itakuwa bora kufika hospitalini haraka kupata usaidizi wa daktari kabla ya ugonjwa huo kuzidi sana.

Yeyote anayeshuku kwamba anaugua utando wa ubongo anapaswa kupelekwa hospitalini mara moja. Hii ni kwa sababu ni rahisi kwa daktari kutibu mgonjwa anayepelekwa hospitalini punde tu anapoonyesha dalili ikilinganishwa na yule anayepelekwa huko kama amechelewa.

MASWALI

a) Bila kubadilisha maana fupisha aya nne za mwanzo (Maneno 70 -80) (Ala. 7, 1 – mtiririko)

MATAYARISHO

................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. .................................................................................................................................................................
................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. .................................................................................................................................................................

NAKALA SAFI

................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. .................................................................................................................................................................
b) Ukizingatia aya tatu za mwisho, eleza dalili za ugonjwa wa utando wa ubongo na huduma kwa mhasiriwa. (maneno 55 -65) (Alama 6, 1 mtiririko)

MATAYARISHO
................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. .................................................................................................................................................................
................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. .................................................................................................................................................................

NAKALA SAFI
................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. .................................................................................................................................................................

15 marks

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 30)

3.

a) i) Tunga sentensi inayodhihirisha matumizi ya ngeli ya LI – YA (al. 1) ................................................................................................................................................................. .................................................................................................................................................................

ii) Kwa kutoa mfano, bainisha matumizi matatu ya nukta/ kitone / kikomo (.) (al.3) ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. ................................................................................................................................................................. .................................................................................................................................................................
.................................................................................................................................................................

b) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya vielezi vya silabi moja vya: (al.3)

i) Wakati

.................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

ii) Mahali

iii) Namna .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

c) Ikiwa kitenzi kimbiliwa ni cha kauli ya kutendewa, je kauli ya ‘fumbata’ ni kauli gani? (al.1) .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

d) Andika kinyume cha sentensi hii (al. 1)

Aliangika bendera baada ya kifo cha mfalme wao.

.................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................
e) Ainisha viambishi katika neno hili (al. 2)

Sitakupiga

.................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

f) Onyesha kiwakilishi cha wakati katika neno: Sikumkuta (al. 1)

.................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

g) Yakinisha sentensi hii katika nafsi ya pili umoja. (al.2) T

usipoelewana na walimu hatutapata amani siku zote shuleni.

.................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... ....................................................................................................................................................
...................................................................................................................................................

h) Changanua kwa mtindo wa jedwali Wazazi wengi waliofika shuleni mapema walileta vitabu vingi sana. (al.5) .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

i) Onyesha shamirisho tofauti katika sentensi hii (al.2) Shangazi alimnunulia mwanangu kondoo. .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

j) Andika katika usemi halisi Mvulana alimwambia baba yake kuwa alitaka kwenda sokoni. (al.2) .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

k) Eleza maana mbili zinazotokana na sentensi ifuatayo. (al. 2) Sisikii vizuri .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

l) Andika visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari (al.2) Mwanafunzi aliyejeruhiwa uwanjani amevuja damu nyingi sana. .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................
.................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

m) Weka shadda katika neno lifuatalo (al.1)

Nne. .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

n) Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya: (al.2) i) randa

.................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

ii) landa

o) Sahihisha sentensi zifuatazo bila kubadilisha maana (al.2)

i) Nimepeana kitabu kwa mwalimu mkuu.

.................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

ii) Sahani yenye imevunjika ni mpya.

p) Fafanua maana ya misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi (al. 2)

i) Enda joshi .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

ii) Hana hanani

.................................................................................................................................................... ..................................................................................................................................................
q) Taja sauti yenye sifa zifuatazo: (al.2)

i) Mbele, juu, tandazwa

.................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

ii) Kikwamizo sighuna cha ufizi

r) Ainisha mofimu hizi: (al.2) Kungun

i .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

Mgeni

.................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

30 marks

4. ISIMUJAMII (Alama 10)

4.

a) Dhibitisha kuwa Kiswahili kimeendelea nchini Kenya baada ya uhuru. (al.5) .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

b) Kwa nini watu hufanya makosa katika matumizi ya lugha? Toa mifano. (al.5) ................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... ................................................................................................................................................... .................................................................................................................................................... ...................................................................................................................................................

10 marks

Back Top