Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TEST 14

Kiswahili Paper 3

SEHEMU YA A (Alama 20)

Riwaya
1.

Ken Walibora – Kidagaa Kimemwozea.

“ Tembo itakuua ndugu yangu. Punguza ulevi bwana, siku hizi naona aibu kukuita ndugu yangu”.

a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b) “Nyani haoni kundule” Thibitisha ukweli wa methali hii ukirejelea dondoo. (alama 6)

c) Mbinu ya sadfa imetumiwa sana katika riwaya ya ‘Kidagaa kimemwozea. Jadili mifano mitano. (alama10)

20 marks

SEHEMU YA B (Alama 20)

Tamthilia
2.

Timothy Arege. Mstahiki Meya – Jibu swali 2 au 3.

2. Mhusika Siki amesawiriwa kama mhusika nguli na mstahiki Meya hasidi wake. Thibitisha.

3. “Wakisubiri nao ugonjwa utasubiri? Hujui ngoja ngoja huumiza matumbo?”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b) Eleza sifa tatu za msemaji ukirejelea tamthilia nzima. (alama 6)

c) Mbali na kungoja kunakoumiza matumbo eleza matatizo mengine matano yanayowakabili wanacheneo. (alama10)

20 marks

SEHEMU YA C (Alama 20)

Ushairi
3.

Jibu swali la 4 au 5

4. RASILMALI

MASWALI

a) Huku ukitoa mifano, taja mbinu ya lugha inayotawala katika shairi nzima (alama 2)

b) Ni kwa nini utungo huu unaweza kuitwa shairi la arudhi. (alama 4)

c) Toa mifano tatu ya idhini ya ushairi iliyotumika na sababu za kutumika kwake. (alama 6)

d) Onyesha kinaya katika ubeti 8. (alama 2)

e) Hakiki matumizi ya kibwagizo katika shairi hili. (alama 4)

f) Eleza matumizi ya maneno haya kama yalilivyo tumika katika shairi (alama 2)

i) Mazagavu

ii) Majilisi

5)

MASWALI

a) Pendekeza anwani nyingine mwafaka kwa shairi hili. (alama 2)

b) Shairi la ‘mche’ ni shairi huru. Dhibitisha. (alama 4)

c) Eleza dhamira ya mtunzi. (alama 2)

d) Andika ubeti 5 katika lugha Nathari/ Tutumbi. (alama 4)

e) Toa mifano miwili ya mishata kutoka katika shairi. (alama 2)

f) Taja taswira inayoibuliwa na umbo la shairi hili. (alama 2)

g) Taja na utoe mfano wa tamathali moja ya usemi katika shairi. (alama 2)

h) Uakifishi katika mshororo wa mwisho wa ubeti 8 una umuhimu gani? (alama 2)

20 marks

SEHEMU YA D (Alama 20)

Damu nyeusi na hadithi nyinginezo
4.

Ken Walibora – Damu Nyeusi.

6. “Leo ni siku ya siku, siku ya nyani kufa na ambapo miti yote huteleza.....”

a) Yaweke maneno haya katika mukadha wake (alama 4)

b) Taja fani za lugha zilizotumiwa katika maneno haya. ( alama 4)

c) Kwa mifano mwafaka eleza yote ambayo mhusika katika dondoo alikumbana nayo. (alama 12)

20 marks

SEHEMU YA E (Alama 20)

Fasihi simulizi
5.

7. a) Eleza maana ya ngomezi. (alama 2)

b) Eleza sifa za ngomezi kama utanzu wa Fasihi Simulizi (alama 10)

c) Fafanua umuhimu wa ngomezi katika jamii (alama 5)

d) Taja udhaifu wa ngomezi (alama 3)

20 marks

Back Top