Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TEST 14

Kiswahili Paper 2

1. UFAHAMU (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujiba maswali.
1.

Babu na nyanya zetu waliweza kuwafundisha vijana mambo mengi na watu walikuwa wamenyooka sawasawa. Ilikuwa wajibu wa kila mzee kupitisha hekima yake kwa vijana kila mara kwa njia ya methali, vitendawili na shirikina zenye mafundisho maalum. Mambo yote haya yaliwafanya vijana kuwaheshimu wakubwa kwa wadogo na watu wa jamii yao. Watu walipokutana na wageni waliwaheshimu nao waliheshimiwa. Ilieleweka kwamba neno 'heshima' iilikuwa na maana kwa kila binadamu na walijua kuwa heshima hainunuliki. Ilikuwa ni nadra sana kusikia zogo limetokea

Vijana wengi wa siku hizo walikuwa wakisifika kwa bidii, uaminifu, ushirikiano, utu, ukarimu, unyenyekevu utiifu na upole wao. Vijana walikubali kuelekezwa kutenda mambo mengi sana katika jamii bila ya maswali ama ukaidi wowote. Hata wakati walipoona mambo yamekuwa magumu, waliomba msaada kwa unyenyekevu mkubwa.

Kila walipoamka asubuhi waliwasalimu watu wazima na kujuliana hali kwa undani na kwa heshima ya kiwango cha juu sana. Wengine walizoea kuwapigia watu wazima magoti wakati walipokuwa.wakiwasalimu. Kama palikuwa na tatizo walishikana bega kwa bega kuliondoa.

Watu walipomaliza shughuli zao za mchana, walikutana jioni na kuulizana habari za siku na kuzungumza yaliyowahusu. Vijana walienda kucheza ngoma ama kwenda kwa vikongwe kufunzwa mambo ya kuwakomaza. Walipozimaliza shughuli hizo zote hawakwenda kulala bila kuwaaga wazazi wao wakinuia kukutana tena siku iliyofuata.

Vijana wachache waliokosa sifa nyingi kati ya hizo walikosa wachumba. Hakuna aliyeweza kuficha tabia mbaya kwa muda mrefu kwa kuwa kila kijana pamoja na ndugu zake walifanya uchunguzi wa kutosha kabla ya kutoa posa. Upelelezi huo wa tabia ulianza mara tu mtu aliposema kuwa anataka jiko. Watu hawakujali ulemavu, Aghalabu waliokuwa na kasoro za kimwili waliweza kuoa ama kuolewa baada ya kuonekana kwamba wametimiza sifa nilizozitaja hapo awali.

Hapo kale hapakuwa na mtindo wa vijana kupiga malapa mitaani. Waovu walikuwa wachache na waliweza kuadhibiwa na yeyote. Hata kama ni mtoto wa watu, wananchi wengine walimrudi bila kujali. Waliamini kwamba mtoto ni wa wote. Hakuna kijana aliyetoka kwao na kulala nje bila idhini ya wazazi wake, na kama msichana angeweza kufanya hivyo wazazi wangeweza kumlazimisha kurudi alipokuwa na arudi na huyo mtu aliyekuwa naye.

Siku hizi mambo yamebadilika sana. Unaweza kuona vioja vya Firauni. Mzee mmoja kikongwe alishangaa. mtoto ameshikia kiuno mtu wa makamo, huku akimnyambua vilivyo. Mzee huyo alisema, "Lahaula! Mbingu zingefunguka hii ni miujiza ambayo sijawahi kuiona. Kweli, kuishi kwingi ni kuona mengi!" Alitazama filamu hiyo ya bure mtu, kuadhiriwa mbele ya umati wa watu. Alibaki akijiwazia kuwa mtoto huyo hakuwa na kaba ya ulimi, na kutegemea siku moja, asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na dunia. Badala ya kuchukua hatua, yule bwana aliyekuwa akitukanwa alinyamaza. Mzee alidhani kuwa yule bwana alikuwa ni bazazi, si mume. Alikuwa ni gumegume. Alishangaa alikubali kutusiwa vile. Mzee huyo alikumbuka enzi zake za ujana na kusema, “Lo! Ingekuwa ni ule wakati wangu huyu angekiona cha mtema kuni. Angewaeleza wenziwe kilichomkosesha kuku matiti!" Alipoona watu wanazidi kujaa mahali pale, alienda zake kwa hasira huku akifyonza fyonza na kulaani utamaduni wa kigeni uliobadilisha ule uliokuwa unadumisha ubinadamu.
a) Andika anwani mwafaka kwa taarifa uliyoisoma. (al.1)

............................................................................................................................................................... ...............................................................................................................................................................

b) Kwa nini vijana wa zamani hawakuwa wakipiga malapa? (al.2) ............................................................................................................................................................... ...............................................................................................................................................................

............................................................................................................................................................... ...............................................................................................................................................................

c) Wazee wa kale walikuwa na jukumu gani katika jamii hiyo? (al.2) ............................................................................................................................................................... ............................................................................................................................................................... ............................................................................................................................................................... ...............................................................................................................................................................

d) Onyesha tofauti mbili baina ya vijana wa sasa na wale wa kale. (al.2) ............................................................................................................................................................... ............................................................................................................................................................... ............................................................................................................................................................... ...............................................................................................................................................................

e) Ni kwa vipi mtoto na bwana wakalaumiwa na yule kikongwe? (al. 2) ............................................................................................................................................................... ............................................................................................................................................................... ............................................................................................................................................................... ...............................................................................................................................................................

f) Ni mambo yapi yaliyomshangaza mzee? (al. 2)

............................................................................................................................................................... ............................................................................................................................................................... ............................................................................................................................................................... ...............................................................................................................................................................

g) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (al.4)

i) Gumegume

............................................................................................................................................................... ...............................................................................................................................................................

ii) Kuwapigia watu wazima magoti.

............................................................................................................................................................... ...............................................................................................................................................................

iii) Kumnyambua vilivyo

iv) Kupiga malapa.

15 marks

2. UFUPISHO (Alama 15)

Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
2.

Ujambazi wa kimataifa ni tatizo lilowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi zimetumia mapesa mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana na janga hili. Hata hivyo, fanaka haijapatikana, wala haielekei kamwe kuwa itapatikana leo au karne nyingi baadaye.

Yumkini tatizo kubwa lililopo ni kuhusu jelezi la dhana ya “ujambazi” tena “wa kimataifa”. Hili ni tatizo mojawapo na yapo mengi sana. Tatizo la pili ni kiburi. Kuna wale watu binafsi na hasa viongozi wa nchi kubwakubwa na serikali zao zilizojiaminisha kuwa ujambazi ni balaa kweli, tena belua, lakini huo ni wa huko, wala hauwezi kuwagusa licha ya kuwashtua wao.

Kulingana na maoni ya watakaburi hao, ujambazi ni wa watu 'washenzi' wasiostaarabika, wapatikanao katika nchi zisizoendelea bado. Ujambazi pekee wanaouona unafaa kukabiliwa ni dhidi ya mbubujiko wa madawa ya kulevya uliosababishwa na vinyangarika kutoka nchi hizo maaluni za "ulimwengu wa tatu". Kulingana na wastaarabu wa nchi zilizoendelea, vinyangarika. hivi ndivyo hasa adui mkubwa wa ustaarabu ulimwenguni na ni sharti vifagiliwe mbali bila huruma. Baada ya kusagwasagwa, ulimwengu mstaarabu utazidi kutononoka na ahadi ya mbingu hapa ardhini itakamilika.

Imani ya watu hawa ya kuwa ujambazi wa kimataifa, hata iwapo upo, hauwezi kuwashtua wala kuwatingisha wao ilikuwa kamili na timamu. Ilikuwa kamili na timamu hadi hapo mwezi Septemba tarehe 11 mwaka wa 2001, ndege tatu za abiria zilipoelekezwa katika majumba mawili ya fahari, yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mia moja na kuyatwangilia mbali. Mshtuko na kimako! Kimako kwa kuwa, kabla ya siku hiyo, Wamarekani hawangeweza kudhani kwamba ingewezekana taifa lolote au mtu yeyote kuthubutu kuishambulia nchi yao, taifa wasifa lililojihami barabara dhidi ya aina yoyote ile ya uchokozi kutoka pembe lolote la dunia.

Hakuna ulimwenguni mzima, aliyeamini kuwa Marekani ingeweza kushambuliwa. Kwa ajili hiyo, mshtuko uliitingisha ardhi yote na huzuni ilitanda kote, kama kwamba sayari nzima imeshambuliwa, wala sio Marekani pekee.

Mintarafu hiyo, Marekani ilipolipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mabomu hatari huko Afghanistan, idadi kubwa ya watu duniani ilishangilia na kusherehekea. Kwa bahati mbaya, tafsiri ya shambulizi la minara-pacha ya Newyork na lile la Pentagon, uti wa uwezo wa kivita wa Marekani, ilizorota. Kuna wengi waliodhani huo ni mwanzo wa vita vya Waislamu dhidi ya Wakristo na kwa muda, Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa kimataifa.

a) Bila kubadilisha maana, fupisha aya tatu za kwanza (maneno 65 -75) (alama 7, 2 za mtiririko)

Matayarisho

........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

Jibu

........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................
...........................................................................................................................................................................................................

b) Ukizingatia aya tatu za mwisho, fafanua fikra za watu na mambo yote yaliyotokea baada ya Septemba tarehe 11 2001 (maneno 65 -75) (alama 6, moja ya mtiririko).

Matayarisho

........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

15 marks

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

3.

a) Taja sauti moja ambayo ni: (al.2)

i) Nazali ya kaakaa laini

...........................................................................................................................................................................................................

ii) Kipasuo sighuna cha ufizi

...........................................................................................................................................................................................................

b) Tungia vitate vifuatavyo sentensi ili kudhihirisha maana (al.2)

i) Chali

...........................................................................................................................................................................................................

ii) Shali

c) Tunga sentensi moja kubainisha matumizi ya :

i) Kivumishi cha pekee chenye maana ‘bila kubakisha’. (al.1) ...........................................................................................................................................................................................................

ii) Kihusishi cha dharau. (al. 1)

...........................................................................................................................................................................................................

d) Andika sentensi hii upya ukitumia chagizo ya wakati badala ya chagizo iliyotumika. Mechi baina ya Harambee Stars na Taifa Stars itachezewa Mombasa. (al.1)

...........................................................................................................................................................................................................

e) Tambulisha kirai kilichopigiwa mstari

Mtumbuizaji mahiri mno anatumbuiza. (al.1) ...........................................................................................................................................................................................................

f) Akifisha sentensi ifuatayo

Labeka njeri aliitika nikuhudumie vipi. (al.2) ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

g) Badilisha kiambishi awali cha ngeli kiwe kiambishi cha kati.

Mipira ilitolewa hewa na watundu wale. (al.1) ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

h) Eleza matumizi ya ‘ku’ yanayodhihirika katika sentensi hii.

Kukimbia kumekutajirisha ingawa hakujaniletea chochote (al.2) ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

i) Changanua sentensi hii ukitumia mtindo wa matawi. Walijitahidi sana kazini ila hawakufaulu kamwe. (al.4) ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

j) Tunga sentensi yenye viungo vifuatavyo

i) Shina la kitenzi cha silabi moja.

ii) Mnyambuliko wa kauli ya kutendea.

iii) Kikanushi.

iv) Kiwakilishi cha wakati uliopita.

v) Mtendwa katika nafsi ya tatu umoja.

vi) Kiishio. (al. 3)

........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

k) Andika upya sentensi hii ukitumia ‘O’ rejeshi tamati Elimu ambayo ilimsaidia ni iliyomletea riziki. (al. 2) ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

l) Tunga sentensi moja moja ukitumia nomino zifuatazo na kivumishi –ngi (al.2)

i) Joto

........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................
ii) Meko

m) Ainisha viambishi katika neno: Tumewajihiana (al.2) ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

n) Andika katika wakati ujao hali timilifu (al.2)

Wanafunzi walifanya mtihani wa kitaifa

........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

o) Unda kitenzi kutokana na: (al.2)

i) Mirathi

........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

ii) Kakamavu

p) Andika kwa udogo wingi Jisu langu nililolinunua juzi lilimkera mzee wangu na ndugu yake. (al.2) ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

q) Jaza pengo kwa kutumia kinyume cha neno lililopigwa mstari.

Mlango ulikuwa umekomewa lakini ________________________ tulipobisha (al. 1)

r) Bainisha yambwa Omari alipigwa na Juma huku Jane akimpiga mwanawe kwa kupasua kitabu chake (al.3) ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................
...........................................................................................................................................................................................................

s) Taja na utolee mifano miundo yoyote mitatu ya nomino katika ngeli ya U – ZI (al.3) ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

t) Eleza maana ya nahau : kaa tutwe. (al.1) ........................................................................................................................................................................................................... ..........................................................................................................................................................................................................

40 marks

4. ISIMUJAMII (Alama 10)

4.

a) Tofautisha:

i) Uwililugha (al.2)

........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

ii) Wingilugha

b) Fafanua sababu nne zinachangia kuwepo kwa uwililugha na wingi lugha. (al.8) ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ........................................................................................................................................................................................................... ...........................................................................................................................................................................................................

10 marks

Back Top