Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2016 KASSU JET JOINT EXAMINATION

Kiswahili Paper 3

1. USHAIRI (Alama 20)

1.

SIKUJUA!

1. Kama ningefuga ng’ombe, mafahali na vindama,
Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.

2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.

3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.

4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.

Kiitikio
Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida


SHAIRI B

Afrika na Watu Wake

Mimi ninaona mgonjwa
Bado amelala kitandani.
Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
Mgonjwa hataweka miguu yake chini
Ili kutembea bila ya kujiegemeza.

Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.

Lakini kuitoa miiba hii
Tunahitaji macho makali
Mikono isiyotetemeka
Moyo usio na huruma
Na kuona miiba ilipoingilia.

MASWALI
(a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B
unavyokatisha tamaa. (Alama 4)
(b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
(Alama 2)
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
(c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
(alama 4)
(d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi
Mshairi alivyotumia kibali chake. (alama 2)
(e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za
aina hii. (alama 2)
(f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A? (alama 1)
(g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B. (alama 2)
(h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari. (alama 3)

20 marks

2. KIDAGAA KIMEMWOZEA (Alama 20)

2.

‘Wanyonge ndio wanyongwao ni kauli inayodhihirka vyema kupitia wahusika tofauti katika
riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Jadili.

20 marks

3.

“Alipofikishwa kwenye zahanati hakushughulikiwa ipasavyo.Ubwete ni ugonjwa mmoja
mbaya walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko”
a) Eleza Muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Dhihirisha jinsi mtunzi alivyoitumia tamathali yoyote moja inayobainika
kifunguni.(alama 4)
c) Riwaya Ya Kidagaa Kimemwozea ni muhtasari wa maradhi yanayolihujumu Bara
Afrika.Tetea rai hii kwa mifano faafu riwayani. (alama12)

20 marks

3. FASIHI SIMULIZI (Alama 20)

4.

(a) Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano. (alama5)
(b) Jadili sifa tano za michezo ya watoto. (alama 5)
(c) Fafanua mambo matano yanayomfanya mtu awe mlumbi bora. (alama 10)

20 marks

4. MSTAHIKI MEYA (Alama 20)

5.

Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.
(a) Jazanda
(b) Uzungumzi nafsia
(c) Majazi
(d) Methali

20 marks

6.

Nonsense! Hivi huyu ana nia gani?
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Taja na ueleze mbinu za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
(c) Jadili umuhimu wa msemaji katika tamthilia hii. (alama 6)
(d) Jadili njia za kuondoa uozo katika jamii ukijikita katika tamthilia ya Mstahiki Meya.
(alama 6)

20 marks

5. DAMU NYEUSI (Alama 20)

7.

“Ikamchagiza kama vile kiu ya mtu aliyekuwa akisafiri jangwani”.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
(b) Fafanua sifa zozote nne za mrejelewa (alama 8)
(c) Eleza fani uliotumiwa na mwandishi katika dondoo hili (alama 2)
(d) Kwa kurejea hadithi zozote tatu,eleza namna wahusika wowote watatu walivyoathiriwa na
kiu. (alama 6)

20 marks

Back Top