Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2016 KASSU JET JOINT EXAMINATION

Kiswahili Paper 2

1. UFAHAMU (Alama 15)

Soma makala yafuatao kisha ujibu maswali yanayofuata.
1.

Miaka 15 iliyopita, Umoja wa Mataifa uliitangaza August 12 kila mwaka, kuwa ‘Siku ya Vijana
Duniani’ ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema ‘Vijana na Afya ya Akili’.

Kwa mujibu wa andiko kutoka Umoja wa Mataifa, asilimia 20 ya vijana duniani kote hupata
tatizo linalohusiana na afya ya akili kila mwaka. Hatari zaidi hutokea katika kipindi cha kuhama
kutoka utoto kuingia utu uzima.

Kutengwa pamoja na aibu mara nyingi huongeza zaidi tatizo kwa kuwa vijana wengine
hushindwa kutafuta msaada wanaouhitaji. Hivyo mwaka huu, Umoja wa Mataifa umeazimia
kuitumia siku hii kukuza uelewa kuhusu afya ya akili kwa vijana.

“Wakati tunaadhimisha Siku ya Vijana Duniani 2014, tuwawezeshe vijana wenye matatizo ya
afya ya akili kubaini umuhimu wao, na tuoneshe kuwa afya ya akili inatuhusu sote,” amesema
Katibu Mkuu wa Umoja wa Maitafa, Ban Ki Moon kwenye maelezo yake.

Miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia tatizo la afya ya akili ni umaskini unaochangiwa
kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa ajira. Asimilia kubwa ya vijana walio chini ya miaka 25 au
wale wanaohitimu masomo yao nchini hawana ajira.

Wanachuo wengi wameendelea kuzunguka huku na kule kuomba kazi bila mafanikio. Wengi
wamekaa zaidi ya miaka mitatu nyumbani tangu wamalize masomo yao bila kuwa na ajira
inayowaingizia kipato.

Na pia wachache wanaopata kazi, wamekuwa wakilipwa ujira mdogo na hivyo kuendelea kuishi
maisha magumu. Ukosefu wa ajira na kukosa fedha za kujikimu, umewafanya vijana wengi
kuwa na msongo wa mawazo, tatizo kubwa linalohusiana na afya ya akili.

Tatizo ni kubwa zaidi pale ambapo takwimu zinaonesha kuwa kwa wastani soko la ajira nchini
lina uwezo wa kuzalisha ajira zipatazo 300,000 kwa mwaka katika sekta rasmi ukilinganisha na
wastani wa wahitimu 600,000 hadi 800,000 wanaoingia katika soko la ajira nchini.

Kwa kijana ambaye hana mahali pa kuishi, hajui atakula nini kesho, hana fedha za kununua
nguo, kukata tamaa na kuamua kufanya lolote si kitu anachoweza kukifikiria mara mbili.
Kwa vijana wa kiume wapo wanaoamua kuwa wezi au matapeli huku wengine wakijikuta
wakiwa walevi wa kutupwa au kuvuta unga kama njia ya kupunguza msongo wa mawazo
unaotokana na maisha magumu.Utumiaji wa vilevi hivyo, umechangia kwa kiasi kikubwa
kuongeza tatizo la afya ya akili kwa vijana wengine.

Kwa wasichana, ukosefu wa ajira, huwaingiza wengi katika wimbi la kutumia miili yao kujipatia
kipato kutoka kwa wanaume. Wengine hujikuta wakiolewa mapema na hivyo kupoteza ndoto za
kujiendeleza kielimu ili kujitegemea.

Mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini kwakuwa wasichana wadogo huzalishwa katika umri
mdogo na wengine kukumbana na unyanyasaji wa nyumbani kutoka kwa waume zao.Katika
maeneo ya vijijini ambako shughuli kubwa ya kiuchumi ni kilimo, ufugaji au uvuvi, baadhi ya
wasichana waliolewa, hujikuta wakiachiwa familia zao kwa muda mrefu na waume zao
wanaoenda kutafuta maisha. Baadhi ya wanaume hao huondoka kimoja na kuwaachia wake
mzigo wa ulezi wa familia.
Hivyo, tatizo kubwa la ajira kwa vijana lipo kwa wale ambao hawana elimu ya kutosha kustahili
kuajiriwa katika ajira rasmi. Kwa mujibu wa survey iliyofanywa na Restless Development,
Tanzania ina takriban watu milioni 25 walio chini ya miaka 25 nchini. Hiyo ina maana kuwa
karibu nusu ya watu wote nchini ni vijana.

Dunia nzima, vijana wamekuwa wakitambulika kwa kuwa na mchango mkubwa kuanzia katika
upatikanaji wa uhuru enzi za ukoloni hadi katika kuvumbua teknolojia mpya na kugundua njia
mpya za sanaa na muziki. Vijana ndio wanaolisukuma zaidi gurudumu la maendeleo kwa
uchapakazi wao kutokana na miili na akili zao kuwa na uchangamfu zaidi.

Hata hivyo Tanzania ni nchi iliyo na matabaka yanayotokana na umri na jinsia huku vijana
wakioneana kutopewa fursa katika mchakato wa maamuzi katika hatua za kijamii na hata katika
serikali.

Ili kuwapa nafasi zaidi vijana katika nafasi za juu za maamuzi, vijana wanapaswa kutambua
kuwa huu ndio wakati wao na sio kesho. Vijana wanatakiwa kwanza kujiamini wao wenyewe
kuwa hakuna nafasi ya baadaye kwakuwa huu ndio wakati unaowaruhusu kuwa wabunifu zaidi
kushawishi maendeleo.

Mawazo yao mapya na njia zao tofauti za kukabiliana na mambo, yataleta utofauti mkubwa wa
sera, maamuzi na muelekeo wa serikali au taasisi mbalimbali.

“Uongozi wa kizazi kipya upo tayari kushika hatamu za uongozi na kuijenga Tanzania mpya,
kwa fikra mpya na maarifa mapya. Mabadiliko, kokote yalikotokea, yalidaiwa na kuongozwa na
vijana. Vijana wa Tanzania washike usukani wa kuleta mabadiliko wanayoyataka. Ukiona kijana
anamwambia kijana mwenzake hana uzoefu, basi kazi ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi.

Kutokuwa na uzoefu ni sifa ya kijana. Tusi kubwa kwa Obama mwaka 2008 lilikuwa ni kukosa
uzoefu, kukosa rekodi. Tusi hilo lilikuwa muziki kwa wapiga kura wa Marekani. Tanzania mpya
inahitaji viongozi wapya, mazoea mapya, fikra mpya na maarifa mapya. Inahitaji kuthubutu
mambo makubwa sio kulinda uzoefu wa nyuma. Tunaweza,” aliandika January Makamba
kwenye mtandao wa Facebook.

Ni kweli muda wa vijana ni sasa na sio kesho tena.

Maswali
(a) Ipe makala hii anwani mwafaka. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
(b) Ni wakati gani ambapo vijana huwa hatarini sana kukumbwa na tatizo la afya ya akilini.
(alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
c) Ni nini lengo la Umoja wa Mataifa mwaka huu kuhusu vijana? (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
d) Taja changamoto zinazowakumba vijana wenye matatizo ya afya ya akili. (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
e) Eleza mambo ambayo huchangia matatizo ya afya ya akili miongoni mwa vijana.
(alama 4)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
f) Taja mambo ambayo huchangia kutamauka kwa vijana. (alama 3)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
g) Ukosefu wa ajira umechangia uozo upi miongoni mwa vijana? (alama 3)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………

15 marks

2. UFUPISHO (Alama 15)

Soma taarifa ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata kulingana na maagizo.
2.

Utoaji wa Huduma ya Kwanza.
Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi
kutokana na hali mbaya ya uokoaji. Watu wengi ambao hujitolea kuokoa majeruhi baada ya ajali
kama za barabarani, maporomoko ya ardhi au nyumba huwa hawang’amui hata chembe jinsi ya
kukabiliana na uokoaji. Hatima ya juhudi zao ambazo hulenga kutenda mema ni kuathirika zaidi
kwa majeruhi.

Hali ya ukoaji inaweza kurekebishwa kwa kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa umma. Elimu
hii yahitajika na kila Mkenya kwani mikasa ya ajali za barabarani na nyinginezo inaendelea
kutokea kila siku.Ajali zinapotokea, si ajabu kuona makundi ya waokoaji yakibeba majeruhi
hobelahobela bila kuzingatia madhara yanayoweza kuwaongezea kutokana na ubebaji wao.
Kutojua namna ya kumbeba majeruhi kunaweza kumhatarisha na hata kusababisha kifo.

Kuna mambo mbalimbali ambayo makundi ya waokoaji yanatakiwa kuzingatia wakati yanatoa
huduma ya kuokoa. Kwanza, ni muhimu kuchunguza kama kuna hatari yoyote inayoweza
ikatokea na kuwatia majeruhi na waokoaji hatarini zaidi. Makundi ya waokoaji yameweza
kuhatarisha majeruhi kwa kuliingilia eneo la ajali mbumbumbu kama mzungu wa reli.

Hatua ya pili ni kutafuta idadi ya majeruhi. Pana uwezekano wa majeruhi kutupwa mbali na eneo
la ajali. Vivyo hivyo, kuna majeruhi ambao huweweseka baada ya ajali na kuanza kutembea
wasijue wanakoelekea. Wengi wao huanguka karibu na eneo la ajali au wakaenda mbali.

Hatua ya tatu ni kuchunguza kama majeruhi amezimia, moyo unapiga na jinsi anavyopumua. Ili
kuhakikisha kuwa majeruhi anapumua, mwokoaji atazame kama kifua kinapanda na kushuka.
Halikadhalika, mwokoaji anaweza kusikiliza au kuguza kifua na kuona kama kuna ishara za
kupumua. Iwapo majeruhi anapumua, mwokoaji amweke katika hali ambayo itaimarisha
kupumua kwake. Anaweza akamlaza chali au kumgeuza kwa pamoja na kichwa chake ili
kufungua mkondo wa hewa. Pia, mwokoaji ahakikishe hamna chochote kinywani kinachoweza
kumsakama. Ikiwa hapumui, mwokoaji anaweza kujaribu kumfanya apumue kwa kupuliza hewa
mdomoni mwake. Fauka ya hayo, upulizaji wa hewa utahakikisha kuwa damu inazunguka
mwilini vizuri.

Hatua nyingine ni kuchunguza vile amejeruhiwa. Chunguza kama majeraha ni vidonda tu au
kuna kuvunjika kwa mifupa na kubainisha ni mfupa upi. Haya yatamwezesha mwokoaji kujua
jinsi ya kumbeba majeruhi. Pakiwa na kuvunjika kwa mfupa, ni muhimu kutotumia kiungo
kilichovunjika anapobebwa.

Pia, kuchunguza vile majeruhi amejeruhiwa, humwezesha mwokoaji kujua huduma ya dharura
atakayotumia. Majeruhi akiwa anavuja damu sana, ni muhimu kuzuia uvujaji huu. Iwapo ni
kidonda kidogo, kinahitaji kufungwa ili kuzuia uambukizaji. Mwokoaji anaweza kutumia kifaa
chochote kilicho karibu kutolea huduma hizi. Kwa mfano, anaweza kupasua nguo ya majeruhi ili
apate kitambaa cha kusaidia kuzuia kuvuja kwa damu au kumfunga kidonda.

Hatua inayofuata ni kumhamisha majeruhi kutoka eneo Ia ajali hadi hospitalini. Mwokoaji
anaweza kuwatumia watu wengine kutafuta msaada. Wanaweza kupiga simu wakitumia nambari
za simu za dharura kama zile za polisi, wazimamoto au makundi ya wataalamu wa shughuli za
uokoaji. Nambari hii ya simu huwa 999 popote na huwa haina malipo. Wanaopiga simu ni
vyema kutoa maelezo ya mahali ambapo ajali imetokea, aina ya ajali na huduma za dharura
zinazohitajika pamoja na idadi ya majeruhi. Iwapo makundi haya ya uokoaji yameahidi kufika,
ni bora kuyasubiri.

Ikiwa makundi ya wataalamu wa uokoaji hayakupatikana, ni jukumu Ia mwokoaji kuhakikisha
majeruhi wamehamishwa na kupelekwa hospitalini. Majeruhi wakiwa wengi. ni bora kuanza na
wale waliozimia au wenye matatizo ya kupumua kisha kuwaendea wanaovuja damu sana.
Baadaye, mwokoaji awasaidie waliovunjika mifupa huku akimalizia na wenye majeraha
yasiyohatarisha maisha. Ni muhimu kuwabeba majeruhi kwa kutumia machela. Hii hupunguza
kuathirika zaidi kwa majeruhi. Iwapo hamna machela karibu, mwokoaji anaweza kuunda moja
kwa kutumia vipande viwili vya mbao, blanketi. shuka au makoti. Ujuzi wa huduma ya kwanza
ni mojawapo ya mambo muhimu ambavo kila mtu anapaswa kuwa nayo.
Maswali :
(a) Fupisha aya mbili za kwanza kwa maneno 55 – 65. (alama 6, 1 utiririko)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………

(b) Eleza kwa kutumia maneno 90-100, hatua zinazotakiwa kufuatwa wakati wa uokoaji.
(alama 8, utiririko 1)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………

15 marks

3.SARUFI (Alama 40)

3.

Eleza maana ya neno changamano huku ukitolea mfano.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………........................................

2 marks

4.

Andika sentensi ifuatayo katika kauli iliyo mabanoni.
Paka analamba mchuzi (kutendwa)
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………............................

2 marks

5.

Akifika sentensi ifuatayo kwa kutumia alama ya kibainishi kisha eleza matumizi yake.
Ntakwenda Unguja mwezi wa Disemba
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………..........................

2 marks

6.

Bainisha aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.
Kuimba kwa Yusufu kunaudhi
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………..........................

1 marks

7.

Andika sentensi ifuatayo katika umoja.
Manukato haya yananukia vizuri
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………............................

2 marks

8.

Eleza matumizi ya ku katika jozi zifuatazo za sentensi.
(i) Kuchora kwao kulikuwa kwa uangalifu mkubwa
(ii) Nilikuita lakini hukuitika
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………

3 marks

9.

Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani.
Kero……………………………………………………..
Nywele ………………………………………………….

2 marks

10.

Tambua viambishi awali na tamati katika neno ajaye
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………

3 marks

11.

Ikarabati sentensi hii:
Mpira yangu amepotea
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………..............

2 marks

12.

Tambua aina ya chagizo katika sentensi ifuatayo.
Walimu wataenda Mombasa Ijumaa ijayo.
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………..............

2 marks

13.

Tambua na ueleze aina za vivumishi katika sentensi zifuatazo.
(i) Viatu vyangu vimepotea
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………..............
(ii) Viatu vyenyewe vinapendeza
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………..............

2 marks

14.

Badilisha sentensi iwe katika hali ya kuamuru.
Rutto fagia chumba.
.……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………....................................

1 marks

15.

Andika sentensi ifuatayo kulingana na maagizo.
Mwanasiasa huyu alishinda kura. (Tumia kiashiria kisistizi)
………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………..........................

1 marks

16.

Onyesha hali katika sentensi zifuatazo.
(i) Huenda mvua isinyeshe msimu huu.
………………………………………………………………………………………………
(ii) Waislamu huenda msikitini kuomba kila Ijumaa.
………………………………………………………………………………………………

2 marks

17.

Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
Aliyetujengea nyumba ni Omari
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………..............
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………..............
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………

4 marks

18.

Andika kwa usemi wa taarifa.
“Nitakuja kwenu kesho,” Mwalimu alisema.
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………..........................

2 marks

19.

Tambua na ueleze virai katika sentensi hii.
Kisichana kile kimejirembesha kwa manukato mazuri ajabu
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………..........................

2 marks

20.

Eleza tofuati baina ya sentensi hizi;
(i) Ningekuwa na pesa ningesafiri kwenda Pwani.
………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………....
(ii) Ningalikuwa na pesa ningalisafiri kwenda Pwani.
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………..............

2 marks

21.

Tunga sentensi moja iliyo na shamirisho kitondo, kipozi na ala.
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………..........................

3 marks

4. ISIMU JAMII (Alama 10)

22.

a) …ya leo ni kuwapa pole wanaofuata na kuenzi makala ya Burudani,toleo la kila
Ijumaa.Mwanamziki huyu aliteka nyoyo za wapenzi wa mtindo huu wa mziki.Kwa kweli ya
Muumba hufumbwa tu!Mnapoyasoma wakumbukeni jamaa na wapenzi wa nyimbo zake.
i. Tambua sajili hii na utoe Ushahidi. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
ii. Fafanua sifa zozote za sajili hii. (alama 4)
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
b) Taja mambo yoyote manne yanayofanywa na Serikali yetu kuimarisha lugha ya Kiswahili.
(alama 4)
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………

3 marks

Back Top