Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2015 KCSE Murang'a South Mock

Kiswahili Paper 3

1.SEHEMA YA A (Alama 20)

USHAIRI Swali la lazima. Soma shairi kisha ujibu maswali
1.

1. Mvua iliyonyesha, ya maradi na ngurumo
Kutwa na kucha kukesha, kunyesha pasi kipimo
Haikuwanufaisha, wewe kazi za vilimo
Wenye kazi za vilimo walifika na hasara.

2. Mimeya walioipanda, ilitekukatekuka
Kazi ngumu waliotenda, yote ikaharibika
Hawakuvuna matunda, waliyo wakiyataka
waliyo wakiyataka, yakawa ya mbali nao.

3. Wenye kuicha mvua, isiwatose mwilini
Baadhi yao wakawa, wakimbiliya penuni
Wengine hawakutuwa, hadi mwao majumbani
Hadi mwao majumbani, na kukomeya milango.

4. Wenzangu dhihaka kando, nisemayo ni yakini
Ilibwaga kubwa shindo, mvua hiyo jamani
Na mijaji kwa mikondo, yakawa barabarani
Yakawa barabarani, mvuwa kwisha kunyesha

5. Kunyesha iliposiya, kukatapakaa tope
Zilijaa kila ndiya, isibakiye nyeupe
Ukawa mwingi udhiya, na kupita zisitupe
Pa kupita zisitupe, kwa ndiya kukosekana.

6. Japo hivyo zilikuwa, ndiya hazipitiki
Bali mimi naamuwa, kwenda japo kwa dhiki
Kumbe vile nitakuwa, ni mfano wa samaki
Ni mfano wa samaki, kuiendeya ndowana

7. Zikanibwaga telezi, sikujuwa kuzendeya
Ningekwenda kwa henezi, yasingenifika haya
Lakini tena siwezi, mwendo huo kutumiya
Sitawata kutembeya, ila tabadili mwendo.

Maswali.
(a) Kwa kuzingatia mishororo miwili ya mwisho kila ubeti, eleza bahari ya shairi hili. (alama 1)
(b) Onyesha kero zinazosababishwa na mvua. (alama 4)
(c) Eleza kanuni zilizofuatwa kutunga shairi hili. (alama 4)
(d) Onyesha namna mshairi alivyotumia idhini yake. (alama 3)
(e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari. (alama 4)
(f) Taja mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 2)
(g) Andika maana za maneno haya kulingana na muktadha wa shairi. (alama 2)
(i) kutwa na kucha
(ii) kuicha

20 marks

2.SEHEMU B (Alama 20)

RIWAYA. Ken Walibora: Kidagaa Kimwemwozea. Jibu swali la 2 au la 3
2.

... ukazae watoto..... wakaikomboe Tomoko toka kwa mkoloni mweusi.
(a) Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
(b) Kwa nini Tomoko inahitaji kukombolewa? (alama 12)
(c) Eleza sifa nne za mnenaji. (alama 4)

20 marks

3.

Kwa kurejelea mbinu zifuatazo za lugha katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, onyesha jinsi zilivyotumika kufanikisha maudhui; (alama 20)
(i) Sadfa
(ii) Barua
(iii)Jazanda
(iv) Mbinu rejeshi.

20 marks

3.SEHEMU C (Alama 20)

TAMTHILIA Timothy Arege: Mstahiki Meya Jibu swali la 4 au la 5
4.

Eleza changamoto za kung’oa uongozi mbaya katika mabaraza ya miji ukirejelea Tamthilia ya Mstahiki Meya.

20 marks

5.

“Diwani wa III na daktari Siki ni viongozi wenye uadilifu na wanaowajibika.” Thibitisha.

20 marks

4.SEHEMU D (Alama 20)

HADITHI FUPI Ken Walibora: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine.
6.

Ukitumia mifano mwafaka, fafanua mambo yanayowatumbukiza vizana katika matatizo

20 marks

5.SEHEMU E (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI.
7.

(i) Ngomezi ni nini? (alama 2)

(ii) Taja sifa sita za ngomezi. (alama 6)
(iii)Eleza dhima ya ngomezi katika majiii. (alama 12)

20 marks

Back Top