Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2015 KCSE Meru South Form 4 Joint Examination

Kiswahili Paper 3

SEHEMU YA A : (Alama 20)

Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine : Ken Walibora , S.A Mohammed, Kanda la Usufi : Rhoda Nyaga
1.

“Tutaondoka ndio, Lakini elewa uchungu wa mwana ajuaye ni mzazi.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Taja na utolee mfano tamathali ya useme iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
c) Eleza sifa nne za msemewa. (alama 4)
d) Eleza madhara ya mapenzi miongoni mwa wanafunzi. (alama 10)
RIWAYA , Kidagaa kimemwozea : Ken Walibora

20 marks

SEHEMU YA B (Alama 20)

RIWAYA , Kidagaa kimemwozea : Ken Walibora
2.

Eleza namna mbinu zifuatazo zilivyotumiwa na mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea
a) Sadfa
b) Kinaya

20 marks

3.

“..unautukanisha ukoo wetu mtukufu. Naona aibu kukuita ndugu yangu.”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Ni tamathali gani imejitokeza katika usemi huu? (alama 2)
c) Bainisha na ueleze migogoro kati ya ndugu hawa. (alama 6)
d) Fafanua umuhimu wa msemewa katika dondoo hili. (alama 8)

20 marks

SEHEMU YA C : (Alama 20)

TAMTHILIA.Mstahiki Meya : Timothy Arege
4.

“Haitokani na maji Sir. Ni harufu ya taka barabarani sir.”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza yaliyopelekea kuwepo kwa harufu hii. (alama 4)
c) Msemaji ana umuhimu gani? (alama 4)
d) Harufu hii ni ishara ya uozo uliotawala jamii nzi,a ya Cheneo. Fafanua aina zingine za uozo zinazopatikana katika tamthilia hii. (alama 8)

20 marks

5.

Jadili jinsi maudhui yafuatayo yamejitokeza katika tamthilia ya Mstahiki Meya.
a. Ukoloni mamboleo (alama 10)
b. Unafiki (alama 10)

20 marks

SEHEMU YA D : (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI
6.

a) Nini maana ya maigizo katika Fasihi Simulizi. (alama 2)
b) Taja vipera vyovyote vine vya maigizo. (alama 4)
c) Fafanua sifa za mwigizaji bora. (alama 8)
d) Taja vikwazo vinavyoweza kukumbuka utanzu wa maigizo. (alama 6)

20 marks

SEHEMU YA E (Alama 20)

USHAIRI
7.

Jicho , tavumiliaje , kwa hayo uyaonayo?
Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo?
Kwacho, litajalo nalije, nimechoka vumiliyo
Naandika!

Moyo, unao timbuko, maudhui tusikiayo
Nayo , visa na mauko, wanyonge yawakutayo
Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo
Naandika!

Hawa, wanatulimiya, dhiki wavumiliayo
Hawa, mamiya, na mali wazalishayo
Hawa, ndo wanaoumiya, na mafia wakutayo
Naandika!

Hawa, sioni wengine , kwao liko angamiyo
Hawa, huwapa unene,watukufu wenye nayo
Hawa, bado ni wavune, kwa shida waitikayo
Naandika!

Bado, wawapo mabwana, wenye pupa na kamiyo
Bado, tofauti sana, kwa pato na mengineyo
Bado, tuling’owe shina, ulaji pia na choyo
Naandika!

a) Ni nini shabaha ya mwandishi aliyetunga shairi hili? (alama 2)
b) Eleza kwa kutoa sababu bahari zinazopatikana katika shairi hili. (alama 4)
c) Je, mwandishi ametumia mbinu zipi ili kutimiza mahitaji ya kiarudhi? (alama 4)
d) Mtunzi wa shairi hili anawasilisha ujumbe gani katika ubeti wa kwanza? (alama 2)
e) Eleza sura ya shairi hili. (alama 4)
f) Taja mambo yanayomkera mshairi huyu? (alama 2)
g) Eleza maana za maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (alama 2)
i. zuiliko
ii. mauko

20 marks

Back Top