Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2015 KCSE Cross Country Mock

Kiswahili Paper 3

SEHEMU YA A : (Alama 20)

USHAIRI: Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali
1.

1 .Naja sasa njiyani, naja kwetu mzalendo
Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando
Kwetu mi nakutamani,kulo na mwingi uhondo
Nifaye ni ile nyundo, kulo na mwingi uhondo
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini.

2. Naja kwingine kuwapi, kulojaa langu pendo
Nenda nende kwinginepo, sawa nako kwa muundo
Kaa kwingine anapo, ela kwenye lakwe gando
Nijaye nyundo, misumari hadharini

3. Naja nije rudi papo, panigandane mgambo
Ningaambwa kwetu hapo, kwanba kwanuka uvundo
Sitakwenda pengiinepo, tarydi kuko kwa mwando
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

4. Naja sitapakimbiya, ningambwa kuna vimomdo
Takuja kuvielekeya, vingajiya kwa rundo
Nilipozawa ‘tafiya, sikimbii kweanda kando
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadhamini

5. Naja kiwa mikomaa, kuzidi nilivyo mwando
Tena najiandaa, kwa fikira na vitendo
Kwetu nije kuifaaa, na kuitiliya pondo
Nijaye na ile nyundo, misumari hadhamini

6. Naja na ingawa siwaekei mifundo
Moyo wangu ushatuja, mawi nalotendewa mwando
Ela wataoningoja na viwivitendo
Nijaye ni ile nyundo, musimari hadhamini.

Maswali
(a) Lipatie shairi hili kishwa mwafaka (alama 2)
(b) Onyesha jinsi kanuni za utunzi zilivyotumiwa kusanifu shairi hili (alama 5)
(c)Kwa kutoa mifani mwafaka eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa (alama 5)
(d) Taja na ueleze mbinu inayopatikana katika ubeti wa tatu (alama 2)
(e) Eleza ujumbe unaopatikana katika ubeti wa hili mshororo wa tatu (alama 2)
(f) Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari (alama 4)
(g) Andika maneno haya kwa lugha sanifu (alama 2)
(i) Mwando
(ii) Ningambwa

20 marks

SEHEMU YA B (Alama 20)

TAMTHILIA: Jibu swali la 2 au la 3
2.

(a) Jadili mbinu mbalimbali zilivyotumiwa na Meya Sosi (alama 10)
(b) Jadili uozo wa kijamii unaojitukuza katika jamii ya cheneo (alama10)

20 marks

3.

Jadili matumizi ya mbinu zifuatazo
(i) Kinaya
(ii) Mbinu rejeshi
(iii) Tahamki
(iv) Uzungumzi nafsia
(v) Nyimbo

20 marks

SEHEMU YA C : (Alama 20)

HADITHI FUPI- DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE- Ken Walibora
4.

Kwa kurejelea hadithi zozote tano, jadili matatizo yanayowakumba vijana katika jamii

20 marks

5.

“Nani amekwambia kwamba mimi unanihusudu? Linin nimekulalamikia hivyo au kumlalamikia
mtu mwingine..?
(i) Eleza mkutadha wa dondoo hili (alama.4)
(ii) Eleza sifa za msemaji wa maneno haya (alama.6)
(iii) Onyesha jinsi msamehewa alivyojionyesha uozo wa kijamii (alama.10)

20 marks

SEHEMU YA D : (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI
6.

(a) (i) Ni nini maana ya ngomezi (alama 2)
(ii) Fafanua sifa tano za ngomezi (alama 5)
(iii) Taja mifano mitatu ya ngomezi kisasa (alama 3)
(b) (i) Bainisha aina nne za watendaji wa fasihi simulizi (alama 4)
(ii) Eleza sifa sita bainifu za mtendaji fasihi sismulizi (alama6)

20 marks

SEHEMU YA E (Alama 20)

RIWAYA-KIDAGAA KIMEWMOZEA
7.

“Nyamaza kulia, “ Amani alimwambia “Shika hilli shati nadhani litakufaa”
Akampa hilo shati la kaki
Maswali
(a) E;eza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
(b) Eleza sifa kuu za yule anayelia (alama 4)
(c) Yule anayelia anamanufaa gani baadaye (alama 2)
(d) Nini kilifuata kupewa shati?
(e) Nini kilimfanya mzungumzaji kufika hapa?

20 marks

Back Top