Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 26

Kiswahili Paper 1

Andika insha mbili
1.

i) Hii ni insha ya ripoti

ii) Sura ya ripoti izingatiwe

a) Anwani

b) Utangulizi

c) Mapendekezo

d) Tamati

iii) Mtahiniwa ashughulikie sehemu hizi nne

iv) Maudhui – ni katika sehemu ya mapendekezo

v) Sura ya ripoti lazima ionekane.Mtahiniwa asipotumia sura ya ripoti atakuwa amejitungia swali apate alama ya D- (02)

vi) Akiacha sehemu mbili za sura aondolewe maki 4s

vii) Iwapo mtahiniwa atashughulikia sehemu zingine za ripoti kama vile : yaliyoshugulikiwa na kamati, utaratibu uliotumiwa na matokeo ya uchunguzi hataadhibiwe litakuwa ni swala la mtindo lakini maudhui yawe tu katika sehemu ya mapendekezo


Majibu yanayotarajiwa:

i) Kuwa na michezo ya pamoja

ii) Kuwa na mikutano kati ya viongozi inayoshughulikia kuleta umoja wa makabila

iii) Matatizo yao yashughulikiwe kwa pamoja

iv) Chanzo cha migogoro kichunguzwe

v) Viongozi wawe mstari wa mbele kuondoa ukabila n.k

vi) Watu wa sehemu mbalimbali waimarishe utangamano kupitia ndoa, biashara n.k

vii) Sera ya kusajili wanafunzi katika shule za upili iwaruhusu wanafunzi kutoka sehemu tofauti tofauti kujiunga na shule yoyote nchini

viii) Viongozi wanaochochea ukabila wachukuliwe hatua kali

ix) Lugha za kienyeji zisitumike mahali pa kazi

x) Vituo vya utangazaji vinavyotumia lugha za kienyeji vipigwe marufuku. Tathmini hoja za mtahiniwa

20 marks

2.

2 i) Hii ni methali

ii) Mtahiniwa atoe kisa au visa kuthibitisha

iii) Methali ina pande mbili kwa hivyo mtahiwa ashughulikie pande zote mbili

iv) Akijibu upande mmoja atakuwa amejaribu kujjibu swali kwa hivyo asipite kiwango cha C (08)

v) Maana – Taa ni samaki ambaye ana kinywa kilichochongoka kama mwiba. Taa hawezi kuacha mwiba wake huo kwa kuwa ni sehemu ya maumbile yake Matumizi: methali hii hutumiwa kumnasihi mtu atahadhari na mtu mbaya au anayeweza kumletea madhara

vi) Mtahini aandike kisa kinachodhihirisha mtu anayejihusisha na mtu mbaya kisha aonywe

vii) Mtu mbaya afiche ubaya wake lakini mwishowe audhihirishe huo ubaya wake kwa kumtendea maovu

3) i) Hili ni swali la mjadala

ii) Mtahiniwa aonyeshe hoja za kuunga mkono na zile za kupinga ziweze kutetewa kwa ithibati

iii) Mtahini ahitimishe kwa kuonyesha msimamo wake

iv) Mtahiniwa akishughulikia upande mmoja asipite kiwango cha C+ maki 10
v) Ikiwa hoja za upande mmoja ni nyingi kuliko za upande mwingine atakuwa ameonyesha msimamo wake

vi) Asipoonyesha msimamo wake hilo ni kosa la kimtindo. Hapa ni pale ambapo hoja za kuunga na kupinga ni sawa katika idadi.

Hoja zinazotarajiwa

Hoja za kuunga

i) Vifaa vingi vinavyotumiwa na mwanadamu kuwasiliana husababisha madhara kwa sehemu za mwili wa binadamu k.v rununu huaminika kusababisha saratani, tarakilishi ukiitazama kwa muda mrefu huharibu macho

ii) Watu hutumia muda mwingi kuangalia runinga badala ya kutumia muda huo kujenga taifa

iii) Wezi kutumia teknohama kuwaibia watu

iv) Simu ya rununu imevunja ndoa nyingi kutokana na ujumbe mbalimbali

v) Visa vya uongo / undanganyifu vimeimarika

vi) Vijana hutazama filamo chafu kupitia kwa mtandao

vii) Watoto na vijana kujifunza mambo mabaya kupitia kwa mtandao

viii) Huathiri wanafunzi kwani wengi hupoteza muda mwingi wakiwasiliana kwenye mtandao

ix) Mtandao hutumiwa kueneza fitina, uchochezi na propaganda mbalimbali.


Hoja za kupinga

i) Imerahisisha mawasiliano

ii) Kuimarisha biashara

iii) Imefanya dunia kuwa kama kijiji kimoja

iv) Imerahisisha utendaji kazi kwa kuwepo njia mbalimbali za kuwasiliana

v) Hutoa ujumbe wa moja kwa moja kwa kutumia nukulishi

vi) Burudani kupitia michezo mbalimbali katika ngamizi / utandarithi:

4 Swali la mdokezo

i) Mtahiniwa aandike hadithi juu ya mtu aliyeshtakiwa

ii) Kosa alilolitenda liwahusishe mkewe na wanawe

iii) Apatikane kuwa mkosaji

iv) Hukumu itolewe dhidi ya mshtakiwa na hukumu hiyo iwe kali

v) Mashtaka yalenge ukiukaji wa haki za watoto na wanawake. Kisa kisipozingatia haya mtahiniwa atakuwa amepotoka apate alama ya D maki 03.

vi) Asipokamilisha kwa maneno hayo hajajibu swali Apate D- 02

vii) Akiyaweka mwanzoni au katikati atakuwa amejitungia swali apate D- 02

viii) Akiacha neno au maneno ya kimalizio atakuwa amejitungia swali Apate D- 02

20 marks

Back Top