Kiswahili Paper 3 Marking Scheme
KCSE CLUSTER TESTS 25
Kiswahili Paper 3
1. SEHEMU YA A (Alama 20)
FASIHI SIMULIZIa. Maana ya miviga Miviga ni sehemu au ibada zinazofuata utaratibu fulani wa kisanaa za maonyesho ya fasihi simulizi. (alama 2)
Inakotumiwa
i. Katika matanga ili kuliwaza wafiwa.
ii. Katika unyago kufunza wari, nasalia na mazingira yao.
iii. Katika mavuno kutoa shukrani
iv. Baada ya vita huwatolea shukrani mashujaa
v. Mtoto anapozaliwa –miviga humkaribisha.
vi. Wakati wa harusi huwapongeza wanacharusi.
vii. Matambiko.
viii. Kutawazwa kwa uongozi. Zozote 8 x 1 = 8
b). Umuhimu wa miviga
i. Hudumisha mila na utamaduni wa jamii.
ii. Huwawezesha vijana kuwa na kumbu kumbu za kila sherehe ilivyofanywa, wakati na maana yake.
iii. Huelimisha vijana.
iv. Hutahadharisha kuhusu maovu.
v. Huwezesha vijana kuelewa au kufahamu desturi zake.
vi. Huleta umoja na ushirikiano katika jamii.
vii. Huburudisha.
viii. Hufundisha unyumba na malezi.
ix. Huhimiza bidii ya kufanya kazi na kujitegemea.
x. Huleta maendeleo. Zozote 5 x 2 =10 Mstahiki
20 marks
SEHEMU YA B (Alama 20)
TamthiliaMstahiki Meya
2. Kinyume na matarajio.
i. Anaendesha baraza kwa kutumia uongo – anasema dawa zimeingia.
ii. Analalamikia maswala madogo madogo kama –viyai.
iii. Anapapia chakula hadi ananyongwa na kuchomeka.
iv. Anakataa kuskiza ushauri wa busara wasiku na diwani.
v. Anaifilisi hazina ya Barasa kwa kuidhinisha nyongeza ya mishahara.
vi. Anaiba viwanja vya baraza.
vii. Anaharibu uchumi kuwapeleka wanawe kusomea ng’ambo /mke anazalia ng’ambo.
viii. Badala ya kuboresha elimu anaiona kuwa duni na kuwapeleka wanawe ng’ambo.
ix. Anafuja pesa kwa kujistarehesha katika hoteli za kifahari.
x. Anampokonya mwanakandarasi kandarasi.
xi. Anashawishika kuiba fimbo ya meya.
xii. Anautelekeza mji kwenye uchafu.
xiii. Anatafuta maombi kwa shilingi laki moja.
xiv. Uongozi wake unashindwa kuleta uthabiti wa usalama wa chakula.
xv. Anatumia asasi km polisi kuwatawanya wapigania haki.
xvi. Anamwajiri mzahili ambaye hajahi hitimu zinazofaa.
Mstahiki meya
Muktadha wa dondoo
3a. -Maneno yalisemwa na Beka
-Alikuwa akimwambia Meya.
-Walikuwa afisini mwa Meya
-Meya alikutana na wawakilishi wa wafanyikazi. 4 x 1 = 4
(b). Malalamishi ya mzungumzaji na alioandamana nao.
i. Kutoshughulikiwa kwa maslahi ya wafanyikazi.
ii. Ajira inayojali maslahi yao.
iii. Mshahara wenye kuchelewa.
iv. Vipeni visivyo na manaa kwa mfanyikazi.
v. Ajira wanayoweza kujivunia mbele ya familia.
vi. Hawana hazina – hawaweki chochote.
vii. Mishahara midogo.
viii. Hawapati nyongeza.
ix. Watoto wao wanahitaji kula na kusoma.
x. Wanaambiwa kulipia madawa ilhali madiwani wana bima.
xi. Wanaosha vyoo bila glovu.
xii. Hawana wa kuwatetea katika vikao vya maamuzi
20 marks
SEHEMU YA C. (Alama 20)
RIWAYA : Utengano4 a. Msemaji ni Biti-kocho
b. Msemewa ni Bi Farashuu.
c. Wako nyumbani kwa Farashuu.
d. Alikuwa akifurahia alivyofaulu kumtalikisha Tamima. na kumtoa Maimuna. Zozote 4 x 1 =
4 (b). Yale msemaji na msemewa waliyofuzu kwayo.
i. Kumtoa Maimuna.
ii. Kumtalikisha Tamima.
iii. Kusambaratisha familia ya Bw. Maksuudi.
iv. Kumchochea Maimuna kuhusu mapenzi.
v. Kusababisha kipigo cha lazima.
vi. Kuvuruga kanuni za nyumba ile kwa kuleta mkunga.
vii. Kumwingiza Maimuma katika ukahaba.
viii. Kulipiza kisasi dhidi ya familia ya Maksuudi.
ix. Maksuudi kuhasimiana na Mussa. zozote 8 x 2 =16.
Utengano
5. matatizo yanayokumba mataifa yanaoendelea ya Afrika.
i. Ufisadi.
ii. Uongozi mbaya.
iii. Tamaa na ubinafsi.
iv. Umasikini.
v. Biashara ya magendo
vi. Ukoloni mamboleo.
vii. Ubaguzi wa kijinsia.
viii. Chuki na uhasama.
ix. Ubabedume
x. Kutowajibika
xi. Tamaduni finyu/hasi
xii. Mizozo ya kifamilia
xiii. Kisasi
xiv. Utabaka
xv. Ulevi
xvi. Ulaghai
20 marks
SEHEMU YA D (Alama 20)
Ushairi6. Bahari za ushairi
i. Ukaraguni –vina vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
ii. Kikwamba – Neno chema limerudiwarudiwa katika kuanza kila ubeti.
KUTUZA: Kutaja 2 x 1 = 2
Maelezo 2 x 2 = 4
(b). Umbo la beti mbili za mwisho.
i. Mishororo mine
ii. Vina vinavyobadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
iii. Mizani _____6, _____6
iv. Kuna kituo / kimalizio Zozote 2 x 2 = 4
(c). Maudhui
i. Mwandishi analalamika kuwa kitu kizuri hakidumu.
ii. Chema kinamwondoka.
iii. Nyanyake ambaye ni kipenzi chake hatarudi (kaaga).
iv. Mwanawe kafa. Zozote 2 x 2 =4
(d). Matumizi ya tabdila
i. N’ongeza
ii. Kukingojeleza
iii. Kinshaniliza iv. Kinmiondoka.
e. Msamiati
i. Ningetamani – Hata nikimtamani.
ii. Kinakuteleza –kitakuondokea.
iii. Kinshamiliza –kunifanya nilie.
iv. Ela - isipokuwa.
v. Alojipa tabu -aliyejishughulisha.
vi. Hini - hii.
7. ( a). Aina la shairi Tathmina
Lina mshororo mmoja katika kila ubeti
-kutaja alama 1 Maelezo alama 2 Jumla alama 3
b. Umbo la shairi
i. vipande viwili
ii. Mizani ___7__7
iii. Vina vinabadilika
iv. Mshororo mmoja
v. Beti 16 Zozozte 4 x 2 = 8
c. Uhuru wa mshairi
i. Inkisari sie - sisi
lipataje - tulipataje
kutaja alama 1 mifano alama 2 jumla alama 3
ii. Kuboronga sarufi - ni wapi litoka - Ilitoka wapi
Kutaja - alama 1 Mfano - alama 2 Jumla - alama 3
d. Maudhui Mwandishi azungumzia weusi na ubaya wake.
20 marks
SEHEMU YA E (Alama 20)
Hadithi fupi-Damu Nyeusi : Ken WaliboraMuktadha
i. Maneno yalisemwa mwanamke mweusi (Flora).
ii. Alikuwa akimwambia Fikirini.
iii. Walikuwa nyumbani mwa Flora na Bob
iv. Bob alitaka kumpiga bastola huku Flora alitaka kumdunga kisu. Zozote 4 x 1 = 4
b. Dhana waliyokuwa nayo watu wa Marekani kuhusu watu waafrika.
i. Watu hutembea uchi.
ii. Wanaugua ukimwi, malaria, polio, utapia mlo.
iii. Hupigana daima.
iv. Walivaa nguo mara ya kwanza walipokanyaga Marekani.
v. Hawajui mji mkuu wa Afrika.
vi. Weusi unatokana na kuangukiwa na lami au kupigwa na mianzi ya jua.
vii. Wanaishi mitini kama tumbiri.
viii. Waafrika wanaenda kusumbua Marekani.
20 marks