Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 25

Kiswahili Paper 1

Jibu maswali mawili.
1.

(i). Sura ya taarifa ijitokeze kama ifuatavyo:
(a). Anwani -Neno taarifa
- Kiini cha taarifa kwa mfano.
TAARIFA KUHUSU VISA VYA UKOSEFU WA USALAMA NCHINI NA NJIA ZA KUKABILIANA NA VISA HIVI.


(b). Utangulizi: Maelezo ya kimsingi kuhusu visa vya ukosefu wa usalama kwa mfano
Hali hii imekuwepo kwa muda upi? Maeneo yapi yaliyoathiriwa zaidi? Washika dau ni wapi?
Mambo mengineyo yanaweza kuzingatiwa.


(c). Mwili: Visa vya ukosefu wa usalama vielezwe na njia ambazo zimetumiwa kukabiliana na tatizo hili zielezwe huku washika dau wanaohusika na njia hizo wakirejelewa.


(d). Hitimisho: Maelezo ya jumla kuhusu swala hili au jitihada zinavyoendelezwa
Kukabiliana na tatizo hili.
Je kuna matarajio ya kufaulu?


(e). Aonyeshe taarifa imeandikwa na nani na jina la chombo cha habari.


f. Kusiwe na vijisehemu baada ya anwani.
ii. Maudhui.
-Visa vya ukosefu wa usalama
-Mauaji.
-Uporaji
-Utekaji nyara
-Vita
-Kuhangaisha raia kwa mfano kuwafukuza kiholela
-Uteketezaji wa majumba.
-Ulipuaji wa mabomu
-Utozaji wa pesa kwa lazima kwa wapite njia
-Kuwekwa kwa mitego ya kunasa waendeshaji magari/pikipiki.
-Maandamano yenye ghasia.
Njia za kukabiliana na tatizo hili.
-Kutuma polisi wengi zaidi kwenye maeneo yaliyoathiriwa.
-Kuimarisha njia za mawasiliano kama vile nambari spesheli za polisi.
-Kufanya msako kuwanasa wanaomiliki silaha haramu.
-Kuwachunguza wanaoingia nchini ili kubaini nia yao.
-Kukagua wanaoingia katika majumba makubwa au maeneo yenye watu wengi.
-Kubuni njia za kuwafanya vijiana watumie muda wao vyema kama vile michezo.
-Kuhusisha raia katika kuwanasa wanaovuruga usalama.
-Kutahadharisha raia dhidi ya kutembea nyakati za hatari.
-Kuweka vibandiko maalum kwenye magari ya usafiri ili kutambulisha magari hayo.


Wahusika dau
-Polisi
-Machifu
-Wamiliki wa vyumba vikuu.
-Wanasiasa.
-Idara ya uhamiaji.
-Viongozi mbalimbali.
-Waziri wa usalama.


ZINGATIA
Lazima visa vitajwe.
Lazima washika dau watajwe.
Akikosa mojawapo ya hayo mawili, na azungumzie hatua za kukabiliana na visa hivi asipite
Akizungumzia maswali yasiyohusu visa, hatua wala washika dau atuzwe D+ 04/20 ilimradi awe na sura ya taarifa.

20 marks

2.

Swali la pili
-Mtahiniwa lazima aonyeshe madhara na faida kisha atoe msimamo.
-Asipotoa msimamo asipite C+ 10/20.
-Akizingatia upande mmoja pekee asipite alama C- 07/20.


Kuunga mkono – uhuru wa vijana una madhara
-Uhuru umesababisha utovu wa nidhamu.
-Uhuru umewafanya vijana kujiingiza katika ulevi wa kupindukia, mavazi yasiyostahili na mengine.
-Umewafanya kutotii walimu / kutowaheshimu wazazi.
-Uhuru umewafanya kutothamini utamaduni.
-Uhuru umewafanya kujiingiza katika siasa zisizo na maana kimaendeleo.
-Uhuru umewafanya vijana kuwa na maandamano kiholela na kuharibu vitu.


Kupinga – Uhuru wa vijana hauna madhara.
- Vijana wanajieleza kikamilifu
-Vijana wamechangia katika ujenzi wa taifa.
-Ukandamizaji umepunguzwa kwani wanaweza kujitetea.
-Sheria zinazowapa uhuru zimewafanya wazazi kuwajibika.
-Kwasababu ya uhuru, wanagenzi wanaweza kuingiliana na kufunzana mema.


Swali la nne
Msimulizi adhihirisha kuwa yuko kwa nchi ngeni ambako kuna hali ngumu. Kisa kinaweza kuonyesha mojawapo ya hali hizi.
(i). Alitorokea nchi ngeni kwa ajili ya hali mbaya kwao. Kuko huko ugenini kuna shida.
(ii). Alihamia nchi ngeni kwa ajili ya kutafuta ajira, elimu, matibabu au ndoa. Anapata hali ngumu.
Kwa vyovyote vile, aliyotarajia msimulizi sio aliyopata.
Nafsi ya kwanza umoja itumiwe ili kisa kimrejelee msimulizi.
Kisa kikirejeleaa mtu mwingine asiye msimulizi, atakuwa ameptoke kimaudhui. Atuzwe D 03/20.
Endapo hataonyesha kuwa yuko katika nchi ngeni asiyoifahamu, amejitungia swali. Atuzwe D- 02/20.
Iwapo hataonyesha hali ngumu lakini awe nchi ngeni, amepotoka atuzwe D 03/20.

20 marks

Back Top