Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 20

Kiswahili Paper 3

1.SEHEMU YA A (Alama 20)

RIWAYA
1.

(a)Utengano.

i. Mawazo /kumbukumbu ya Inspekta Fadhili kama inavyojitokeza katika ubeti wa shairi aliyotunga.

ii. Nyumbani kwa Maksudi.

iii. Maksudi alikuwa akifanya mazoezi ya hotuba.

iv. Ilikuwa baada ya kukereka kuona namna Bwana Maksudi alivyotajirika kwa haraka.(zote 4x1=4)

(b) Sifa za Fadhili.

i. Mwajibikaji-Alifanya kazi yake bila mapendeleo, hakujali undugu wa Bwana Maksudi.

ii. Mpenda haki-Aliamini kuwa mtu anafaa kujipatia cheo kwa njia ya halali na haki /anatekeleza haki anapomtia Maksudi mbaroni.

iii. Mwenye msimamo thabiti-Anakataa kuhongwa na Maksudi.

iv. Amezinduka kisiasa-Anaelewa kuwa matatizo ya jamii yanatokana na ukoloni mkongwe au ukoloni mamboleo. (zote 4x1=4)

(c)

(i) Utengano wa ndugu wawili. Sababu

(ii)Fadhili anakataa ombi la Maksudi kuwa amfichie kesi ya ufisadi.

(iii)Maksudi anajaribu kumhonga Fadhili lakini anakataa.

(iv)Maksudi anamfukuza Fadhili kutoka kwake.

(v)Fadhili anatoka akimwambia kuwa watakapokutana mmoja wao atajua zaidi. (zozote 4x1=4)

(d) Uhuru haujatimia. Maimuna.

i. Alitawishwa na babake.

ii. Alinyimwa uhuru wa kuzuru mazingira yake.

iii. Alinyimwa uhuru wa kupata elimu. Zozote 2x1=2

Tamima

i. Alitawishwa na mumewe.

ii. Alinyimwa nafasi ya kupata matibabu wakati wa kujifungua.

iii. Hakuruhusiwa kusema au kujitetea mbele ya mumewe.

iv. Alipewa talaka bila kupewa fursa ya kujitetea.

v. Alitenganishwa na mwanawe mchanga. Zozote 2x1=2

Mwanasururu.

(i) Alihiniwa mali yake na kutalikiwa na mumewe. 1x2=2

Farashuu, Mama Jeni, Biti Sururu. (i)Wanajitafutia pato dogo.

(ii)Wanalazimika kutumia njia haramu kuzumbua rizki.

(iii)Maskini –waliishi katika mitaa duni. 1x2=2

Biti Kocho-ingawa aliajiriwa kwa Bwana Maksudi,hakujiweza kiuchumi na analazimika kuomba pesa. 1x2=2 (zozote 4x2=8)

20 marks

2.SEHEMU YA B: (Alama 20)

TAMTHILIA
2.

(i)Anayezumza ni Daktari Siki.

(ii)Anaongea na Waridi. (nesi)

(iii)Walikuwa zahanatini.

(iv)Wanaongea kuhusu idadi ya wagonjwa waliofika zahanatini kutafuta matibabu. (zote 4x1=4)

(b)

(i)Ukosefu wa madawa.
(ii)Ukosefu wa pesa za kulipia huduma wanazotaka/hawana pesa.

(iii)Ukosefu wa karatasi za kunakilia udodosi.

(iv)Njaa-hawana chakula.

(v)Wamekumbwa na magonjwa/utapia mlo.

(vi)Kuzidiwa na gharama ya maisha.

(vii)Wafanyikazi wa baraza kutolipwa mshahara.

(viii)Uchafu mijini/harufu mbaya.

(ix)Ukosefu wa maji

. (x)Malipo yao ni duni.

(xi)Vifo. (Zozote 8x1=8)

(c) Sababu.
(i)Raia kuendelea kuwachagua viongozi wabaya (ukosefu wa elimu) uk 12 Ujinga.

(ii)Ubinafsi wa baadhi ya viongozi

-Pendekezo la Diwani wa pili. walinda usalama kuongezwa mshahara.

(iii)Viongozi kutowashirikisha watu /raia katika maamuzi yao.

(iv)Viongozi kukataa ushauri wanaopewa.

-Mfano Meya kumpuuza Daktari Siki na Diwani wa III/mapuuza.

(v)Kutoajibika kwa viongozi –mfano Meya,Diwani I na II. Baraza kushindwa kutimiza majukumu yake.

(vi)Ufisadi-walinda usalama kuhongwa kwa kulipwa/kuongezewa asilimia ishirini,walinda usalama kutotozwa kodi.

(vii)Ubadhirifu wa viongozi-watoto wa Meya wanasomea ng’ambo/mke kuzalia ngambo.

(viii)Unafiki wa viongozi wa dini-hawamwambii Meya ukweli kuhusu uongozi wake.

(ix)Utegemezi

–Baraza linasubiri madawa kutoka ughaibuni –wameshindwa kuvumbua yao. (zozote 4x2=8 mks)

20 marks

3. SEHEMU YA C: (Alama 20)

HADITHI FUPI.
3.

Samaki wa nchi za joto

(i) wafanya biashara wa samaki Afrika(wavuvi)hawafaidiki kutokana na jasho lao ila wanaofaidi ni wafanya biashara wa ughaibuni.

(ii) Somo la Soshologia analosomea Christine katika chuo kikuu hakimfaidi hata kidogo/elimu ya chuo kikuu kutowafaidi wanafunzi.

(iii) Tendo la Idi Amin kuwaangamiza maprofesa wengi ni kinaya kwani kinachangia elimu duni vyuoni anawaangamiza ilhali nchi inawahitaji.

(vi) Chuo cha Makerere kupagazwa jina la ‘’Havard ya Afrika’’,ilhali hakiwafaidi wanafunzi wake.

(v) Chumba kibovu cha Zac kinahifadhi picha kubwa ya Bob Merley-mwimbaji mashuhuri na vitabu vya waandishi wa kigeni kama vile’’the penguin classics.

(vi) Peter anawadharau na kuwanyanyasa wafanyakazi wake ilhali hata yeye anadharauliwa huko kwao-Denmaki. /Peter ni mzungu wa hali ya chini kwao.

(vii) Christine alipomtembelea Peter ofisini mwake,alitarajia kupewa makaribisho mema lakini badala yake anazungumziwa kimadharau.

(viii) Christine ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu anafanya uhusiano na Peter ilhali halifahamu hata jina lake la pili’’Mr.Smithson’’.

(ix) Maungo ya Christine na Peter yanapogusana kitandani walikokaa,Christine anajivuta nyuma ilhali ni wazi kuwa alivutiwa sana na mzungu huyo.

(x) Dorothy dadake Christine anashindwa kumkosoa Christine waziwazi.

(xi) Muuguzi Margaret kuhusika katika tendo la kuavya mimba. (zozote 10x2=20)

20 marks

4.

(a)

(i) Maelezo ya msimulizi,. (al 1)

(ii) Akimrejelea Fikirini. (al 1)

(iii) Mahali ni kituo cha mabasi (al 1) alipokuwa amesimama Fikirini.
(vi) Dereva wa basi mwenye asili ya kizungu anaamua kutolisimamisha basi kwa kuwa abiria aliyekuwa akisubiri basi ni wa asili ya kiafrika/Anambagua Fikirini (al1)

(b) Maudhui. Ubaguzi/unyanyasaji. Al 2

(c)

(i) Dereva Mzungu wa basi la abiria anakataa kumbeba Fikirini kwa kuwa ni mweusi.

(ii) Fikirini kuuliza maswali ya kudhalilisha na kudunisha kutoka kwa wanafunzi wenzake na wahadhiri.

(iii) Sheria zinazombagua mweusi na kumpendelea mzungu-Fikirini kutozwa faini kwa kuvuka barabara taa zikiwaka rangi nyekundu.

(iv) Chuoni-Alama zinazotolewa na wahadhiri zilitolewa kwa mapendeleo.Wazungu walipendelea huku weusi wakinyanyaswa.

(v) Mkahawani-Fikirini anakumbana na mitazamo ya dharau kutoka kwa wahudumu na wateja wa Kizungu.

(vi) Fikirini kuitiwa polisi na mteja wa Kizungu kwa kusahau kufunga zipu ya suruali yake.

(vii) Fikirini kuulizwa maswali ya kudhalilisha na polisi wa Kizungu – ikiwa alielewa lugha ya kizungu.

(viii) Jela kujawa na watu weusi kana kwamba wazungu hawafanyi makosa.

(ix) Bob na Fiona kukasirishwa na kuja kwa Fikirini ughabuni. (zozote 7x2=14)

20 marks

4.SEHEMU YA D: (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI
5.

(a)

i) Kisasili. (al 1)

ii) Inaelezea jinsi kifo kilivyoingia duniani (al 2)

-Asili ya kifo.

(b) Sifa za ngano.

(i) Mwanzo maalum (fomula)-Hapo zamani za.......................................

(ii) Wahusika wanyama mf. Mjusi na kinyonga.

(iii) Wanyama kuwasilisha tabia na hisia za binadamu.Mf kuongea,kujibizana,kuitikiana,n.k

(iv) Tanakali za sauti mf .pu! (zozote 3x1=3)

(c) Kinyonga ni:

(i) Mvivu/mzembe/mlegevu.

(ii) Si mzingativu-Anachelewesha ujumbe.

(iii) Mtiifu-mwishowe alifikisha ujumbe. n,k (zozote 3x1=3)

(d)Umuhimu wa hadithi.

(i) Kuelezea asili ya binadamu.

(ii) Asili ya kifo na jinsi kilivyoingia duniani.

(iii) Matukio mbalimbali katikati ya jamii,wanyama na hata miungu mf.kwa nini kuku huchakurachakura n.k.

(iv) Huipa jamii mwelekeo/njia za kufuata.

(v) Hukumbusha jamii juu ya matukio.

(vi) Huburudisha/Huliwaza. (vii) Ni historia na utamaduni wa jamii.

(viii) Huonya /Huadibu.

(ix) Huelimisha n.k. (zozote 4x1=4)

(e)Njia za kukusanya fasihi simulizi.

(i) Mahojiano yaliyopangwa na mtafiti na wahojiwa wake.

(ii) Kwa kutumia vinasa sauti.

(iii) Kutumia video.

(iv) Kwa kuandika data au kazi husika.
(v) Kuangalia yale yanayotendeka mf. Jukwaani.

(vi) Sherehe zilizopitishwa toka kizazi hadi kingine. (Tuza zozote 4x1=4)

(f)Tambulisha vipera.

(i) Kula hepi-msimu (kuwa na haraka).

(ii) Semi yako ni ya kuazima-msemo (mtu asiringe).

(iii) Baba wa taifa-lakabu (kiongozi wa nchi).

20 marks

6.MAGHANI (Alama 10)

6.

(a)Maghani ni utungo wa kishairi ambao hutongolewa kwa kutumia sauti iliyo kati ya uimbaji na uzungumzaji. (al 2)

(b)

(i) Vivugo ni ushairi wa kujisifu ambao hutungwa papo kwa hapo na kughaniwa na mtunzi au mtu anayehusika.(al 2)

(ii) Tondozi ni tungo za kusifu watu,wanyama,vitu kama magari,miti,nk(al 2).

(iii) Pembezi-ni aina ya tondozi ambayo imekusudiwa kusifia watu wa aina fulani katika jamii kutokana na matendo yao au mchango wao katika jamii.(al 2)

(iv) Rara-Hadithi fupi nyepesi za kishairi zenye visa vya kusisimua. Zinaweza kughanwa zikiambatana na ala za muziki/husimulia mambo ya kubuni.(al 2).

(c) Ulumbi ni uwezo maalum wa kipekee wa kimazungumzo unaonyeshwa hadharani na huandamana na matendo/maigizo.(al 2).

(d) Sifa.

(i) Hutumia lugha kwa njia inayovutia na kushawishi hadhira.

(ii) Hubainika katika muktadha mwingine kama vile,hotuba,mijadala nk.

(iii) Hutumia tamathali nyingi za usemi k.v balagha,methali,misemo na viziada,lugha(toni,wimbo)

(iv) Ulumbi hutumia chuku kwa ufanifu mkubwa. (zote4x2=8)

20 marks

7.SEHEMU YA E: (Alama 10)

SHAIRI
7.

SHAIRI. A.

(i) Umaskini hudhoofisha afya.

(ii) Maskini hakopeshwi kwa urahisi.

(iii) Maskini anaweza kufa ghafla.

(iv) Maskini hata nguo ya kuzikwa (sanda) ni vigumu kupata.

(v) Mtu yeyote anaweza kuwa maskini,awe mzungu au mwafrika. (zote 5x2=10)

SHAIRI. B.

(i) Maskini anaahidi kuwa atalipa deni lakini hawezi kwa sababu hakuna atakayemkopesha.

(ii) Umaskini unafanya mtu kuwa mjeuri akawa akikopa wewe utachoka kusubiri.

(iii) Maskini analaghai,anaahidi kuwa atalipa kumbe ni uongo.

(iv) Maskini hata akishtakiwa haogopi.

(v) Hapendi kusumbuliwa bali afarijiwe. (zote 5x2=10)

10 marks

Back Top