Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 19

Kiswahili Paper 3

1.SEHEMU A: (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI
1.


(a) (i)Ngomezi ni fasihi ya ngoma/ala zingine za kimuziki bila kutumia maneno.(Kupitisha ujumbe kupitia ngoma/ala za kimuziki.)
(ii)Tariri ni orodha ya matukio muhimu na miaka ya matukio hayo kama yalivyotokea.
(iii)Miviga ni sherehe za kitamaduni zinazoonyesha usanii wa maonyesho ya kuiga jinsi tukio fulani lilivyofanyika katika uhalisia wa maisha.
(iv)Mapisi ni maelezo ya kihistoria ambayo hayana ubunifu mkubwa.Hueleza mahali ambapo jamii inaaminika ilitoka/ilihama na kufanya makazi yake ya sasa. (4x1=4mks)
(b) Misimu ni maneno au semi ambazo huzaka wakati wa kipindi Fulani na kutokomea baadaye.(2 mks)
Sifa: (i)Huzuka lakini haidumu kipindi kirefu.
(ii)Baadhi ya misimu huwa sehemu ya lugha.
(iii)Hutumika katika mikutadha tofauti tofauti.
(iv)Huweza kutoa maana mbalimbali. (zozote 2x1=2)
Mifano:-Unbwogable-Faiba-kula hepi/ngoma.
-Dot-com-Tsunami-leta diabo/noma.
- Zua kasheshe-Doo-Kupiga kamera. (2x1=2)
(c) Matatizo yanayoikabili Fasihi simulizi ni k.v
i. Matumizi ya lugha ya Sheng’.
ii. Kuhama kutoka mashambani hadi mijini.
iii. Maendeleo ya teknolojia.
iv. Ukosefu wa wazee katika jamii.
v. Ukosefu wa wasomi wengi wanaofanya utafiti katika uwanja huu.
vi. Ukosefu wa vitabu vya marejeleo.
vii. Kuathirika na tabia mienendo ya kigeri.
viii. Kuchipuka na kuenea kwa kiwango kikubwa kwa dini za kisasa.(kikiristo,kiislamu,kihindi n.k) (zozote 5x1=5 mks)
(d) Sifa za Jagina.
i. Wana sifa zisizo za kawaida.
ii. Huja vifo vya kusikitisha.
iii. Hawaishi kufaidi waliyopigania.
iv. Huzaliwa kwa njia ya ajabu.
v. Mara nyingi hutegwa na maudui kupitia kwa wanawake warembo wa maadui wao.
vi. Hupigania jamii zao ila si nafsi zao.
vii. Ni mashujaa wa kuogopwa. (Zozote 5x1=5)

20 marks

2. SEHEMU B: (Alama 20)

RIWAYA S.A MOHAMED
2.

(a) Maneno haya yalisemwa na Biti Kocho.
Alikuwa akimwambia Bw.Maksuudi.
Walikuwa nyumbani kwa Bw.Maksuudi.
Ilikuwa ni baada ya Bw.Maksuudi kutoka kwa Bi.Kazija,akakuta mkewe Bi.Tamima anayejifungia.Anampiga huku akimlaumu kwa kutoroka kwa Maimuna.Biti Kocho anaingilia kati kumzuia Maksuusi asiendelee kumchapa Bi.Tamima.
(b) Hapana asiyejua siasa dunia hii.Hii ni kwa sababu:
i. Biti.Kocho anatetea uhuru wa mwanamke kutotairishwa.
ii. Biti Kocho anamlaumu Maksuudi kwa unafiki wake kutetea usawa katika mikutano lakini anatawishwa mkewe na bintiye pale nyumbani.
iii. Biti.Kocho na Farashuu wanamsaidia Maimuna kuvunja minyororo ya utawa kwa kutoroka nyumbani.
iv. Katika mkutano wa siasa uwanjani,uhuru,watu walisma wamechoka kudanganywa na wanasiasa kwa ahadi zisizowezekana.
v. Mzee Bakari katika mkutano wa siasa anaelewa kuwa ahadi za Zanja za kuwajengea njia n.k haziwezekani kwani nchi yao ni maskini.
vi. Kazija anadhihirisha kasoro za Maksuudi na Zanga hadharani.
vii. Umma kutaka kuwapiga Zanga na Maksuudi kwa sababu wanaelewa maovu wanayowafanyia.
viii. Fadhili anakosana na kakake Maksuudi kwa sababu hakubaliani na siasa za Maksuudi za kudhulumu umma.
(Zozote 4x2=8)
(c) (i)Mnenaji,Biti Kocho,ni mwajiriwa wa Maksuudi.

(ii)Anajua kuwa amewatairisha mkewe na bintiye ingawa huko nje anapinga utawa wa wanawake.
(iii)Anaelewa kuwa Maksuudi anajifanya shehe ilhali anafanyia watu maovu.
(iv)Anajua Maksuudi alivyomtesa Mwanasururu na kusababisha kifo chake.
(v)Anajua kuwa Maksuudi ni mpenzi wa Kazija.
(vi)Anajua mpango na Kazija wa kuwakutanisha Maksuudi na mwanawe Mussa kama waume wenza.
(vii)Amefaulu kumtorosha Maimuna kwa hivyo anajua hisia za Maimuna kumhusu Maksuudi.
(viii)Biti Kocho anajua Maksuudi anavyodhulumu wafanyikazi wake kwani yeye ni mmoja wao.
(ix)Anajua mateso anayomfanyia mkewe,Bi.Tamima.

20 marks

3.

Maovu anayotenda watu yaweza kumwathiri mwenyewe au wanaomhusu baadaye.
i. Maksuudi.
-Anawanyima uhuru Bi.Tamima na Maimuna→ linapelekea kutoroka kwa Maimuna.
-Anampiga Tamima→ kunasababisha talaka na kuvunjika kabisa kwa ndoa yake.
-Kumhini Mwanasururu → kunaleta njama ya kulipiza kisasi.
-Anashiriki ukahaba → Anaaibika wanapokutana na Mussa kwa Kazija.
-Alikataa kusika ushauri wa Rashidi → alipata kipigo kikali kutoka kwa umma.
-Anashiriki ufisadi → Ananyimwa kura.
-Anashiriki ufisadi →Anafungwa jela.
ii Maimuna.
-Alikuwa na tama ya uhuru→Alijipata ukahabani.
-Alikata ushauri wa Biti Sururu kupunguza ulevi→alidhoofika kiafya.
-Alimtusi Bw.Maksuudi (mbwa mkubwa)alipotaka kumrejesha nyumbani → alipotaka kumwona badaye,alikuwa amekuja
-Alipigana na kijakazi→aliumizwa usoni.
iii. Bi Farashuu.
Anapanga njama ya kulipiza kisasi→akamharibu Maimuna ambaye badaye anaolewa na mjukuu wa Kabi.
iv. Mussa
-Anashiriki ukahaba→akafumanishwa na kutengana na tamaa yake.
v. Zanga
Alikuwa na ujeuri na majivuno na ufisadi→alikosa kura na afungwe jela.
vi. Mama Jeni.
Alizingatia uchochezi wa wasichana wake wengine →akamfukuza Maimuna na kipato chake kikapungua.(Hoja zozote 10x2=20)

20 marks

3.SEHEMU C: (Alama 20)

TAMTHILIA
4.

4) (i) Uongozi mbaya.
Meya na baraza lake waendeleza uongozi mbaya.
*Ukosefu wa dawa katika zahanati.
*Uvunjaji wa kanuni za baraza.
*Matumizi ya nguvu dhidi ya umma.
*Ukosefu wa ajira/kazi Cheneo.
*Hakuna lishe bora.
*Lishe bora inakosekana.
*Maji safi ya kunywa pia yanakosekana.
(ii)Umaskini
Wananchi wa Cheneo wana umaskini wa hali ya juu unaodhihirika kupitia:-
*Kula makombo ya mbwa.
*Kula mizizi na matunda ya mwituni.
*Ukosefu wa lishe bora(utapiamlo).
*Wanashindwa kugharamia matibabu.
*Wanashindwa kugharamia elimu.
Baraza la Cheneo pia ni maskini.
*Linaendeshwa kwa mikopo.
*Halina fedha za kuwalipa wafanyakazi.
−Wafanyakazi hawalipwi kwa wakati unaofaa.
−Wanashindwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi.
−Baraza haliwezi kuwaajiri waliohitimu kutoka vyuo vikuu.
−Meya analazimika kuuza vipande vya ardhi agharamie matibabu ng’ambo.
(iii) Utabaka
Kuna matabaka matatu katika cheo:-

Meya na Diwani I na II ni watabaka la juu(wenye mali).wafanyakazi ni watabaka la kati kama vile Siki,Tatu,Medi na Beka.Tabaka la chini ni watu kama akina Kerekecha.
−Tabaka la juu wanatibiwa ng’ambo wakati wengine wanashindwa kumudu gharama za matibabu.
−Tabaka la juu wanapata elimu ng’ambo.
−Tabaka la juu wana nyumba zilizopambwa.
−Tabaka la juu wanapata wakati wa kuburudika.
(iv)Usaliti
*Meya anawasaliti wananchi waliomchagua.
Wanacheneo wanatarajia maendeleo.
*Meya anawasaliti wazalendo waliopigania uhuru-anaendeleza ukoloni mamboleo.
*Diwani I na II wanasaliti wananchi waliowachagua –wanajinufaisha wenyewe.
*Bili anamsaliti Meya baada ya mambo kuharibika.
*Mhazili anamsaliti Meya nakuongea na wafanyakazi kugoma.
*Siki anamsaliti Meya ambaye ni binamu yake.
*Meya anamsaliti Diwani III na kumtenga katika maamuzi.
*Waridi anaisaliti taaluma yake-anasisitiza walio na fedha wasipate huduma.Anajiuzulu kazi yake na kuwaacha wangojwa wanateseka.
(v) Ukombozi
*Wafanyakazi wa baraza la mji wanangana na kupigania haki zao.
*Siki na Diwani III wanaungana na wafanyakazi kupigania masilahi bora.
*Wafanyakazi wa sehemu nyingine wanaungana mkono na wenzao(wafanyakazi wa uwanja wa ndege,mhazili na wafanyakazi wa bohari ya mafuta).
*Uongozi shupavu ndio huchochea ukombozi.
−Tatu,Medi na Beka wanawakilisha malalamiko yao bila hofu .
−Kiongozi wa wafanyakazi anahamisha umoja na mshikamano.
*Ukombozi ni suala rahisi.
−Wafanyakazi wanapigwa na kuvurumishwa na askari kwa vitoa machozi.
−Wafanyakazi waligoma wanatishiwa kufutwa kazi.
−Wafanyakazi wanatishiwa na Meya.(5x4=20)

20 marks

5.

5) (a) Maneno haya ni sauti ya kiongozi wa wafanyakazi.
Anawahutubua wafanyakazi wanapofanya maandamano.
Wako nje ya baraza la mji wa Cheneo.
Wafanyakazi wanaandamana kulishinikiza Baraza la Cheneo liwatendee haki. (AL 4)
(b) (i) Ukosefu wa dawa hospitalini.
(ii) Gharama ya maisha iko juu na mishahara ni duni.
(iii)Viongozi wanaendelea kujilimbikizia mali (zozote 2x2=4)
(c) (i) Tatizo lilikuwa mgomo na maandamano ya wafanyakazi.
(ii) Daktari Siki anafukuzwa na askari kutoka ofisini mwa Meya kwa madai ya kuchochea wafanyakazi.
(iii) Mkuu wa askari anaamuliwa kuleta askari wawatanye wanyakazi
(iv) Meya anapokutana na viongozi wa wafanyakazi anakataa kusikiliza malalamishi yao hadi watakapositisha mgomo.
(v) Wafanyikazi wa viwanja vya ndege wanaunga mgomo pia mhazili wa Meya anagoma.Meya na wenzake Diwani I na II wanatiwa mbaroni.
(zozote 4x3=12)

20 marks

4.SEHEMU D: (Alama 20)

HADITHI FUPI
6.

6) Ubaguzi.
−Ni hali ya kutengwa na wengine kwa misingi Fulani.Hapa ni kwa misingi ya rangi na alipotoka mhusika.
(i)Weupe kufikiria Afrika kumejaa uovu-k.v.ukeketaji,dhana kuwa wanaishi juu ya miti,wengine ni wala watu,uchawi na ushirikina.
(ii)Dereva mzungu anamwacha Fikirini kwenye kituo cha basi ingawa basi ni la usafiri wa umma.
(iii)Fikirini ametozwa faini mara mbili na polisi mzungu kwa kukiuka sheria za barabara ambapo watu weupe walikuwa wanasamehewa.
(iv)Wahadhiri vyuoni wanatoa alama kwa kuwapendelea weupe.
(v)Anapotembea kufurahisha macho yake anatuhumiwa kuwa mdokozi au mwizi.
(vi)Anaposahau kufunga zipu ya suruali yake anatuhumiwa mbakaji na kutozwa faini.
(vii)Wamerika weusi wanawadharau waafrika kutoka Afrika- Fiona anashurutisha Fikirini afanye ngono au ampige risasi.
(viii)Wanamwibia na kumtoa nguo zote wakimtupa nje kwa barafu na kumwambia waafrika waache kwenda Marekani.
(ix)Mhadhiri na wanafunzi weupe kuwauliza weusi maswali ya kuwadhalilisha.

20 marks

7.

7) (a)Swali hili liliulizwa na Kananda.Jibu lilitolewa na Mwatela.Walikuwa nyumbani kwa
Bw.Mwatela.Ilikuwa ni baada ya Kananda kugundua alikuwa mjamzito kutokana na kubakwa na
Bw.Mwatela.(Al.4)
(b)-Alijifungua mtoto wa kiume lakini hakuolewa na Bw. Mwatela.
-Alinyang’anywa mototo wake wakiume na Bw.Mwatela.
-Aliozwa kwa dereva wa malori ya shehena kutoka Kongo.
-Dereva alimuuza kama mtumwa kwa mtu mwingine.
-Aliokolewa na askofu mzungu na akarudishwa Kenya na kumsaka Bw. Mwatela.
-Aliumizwa kwa jiwe na Mwakitawa(mtoto wake na kulazwa hospitalini.
Hatima→aliungana na mwanawe baadaye na kurithishwa nyumba ya kifahari ya Bw.Mwatela.Mwatela
alitenga pesa za kumwelimisha Mwakitawa na kumsaidia Kananda mpaka aweze kujikimu.
Masaibu yoyote 3x2=6 (Al l2)
Hatima 1x2=2

(c) Maovu ya kijamii
a) Ubakaji-Kananda alibakwa na mwajiri wake Bw. Mwatela
b) Ulevi:Bw.Mwatela alikuwa mlevi chakari na wakati mwingi aligombana na kumchapa mkewe.Ulevi
huu ndio uliomfamya ambake Kananda.
c) Uongo: Bw.Mwatela alimdanganya Kananda ya kuwa angemwoa baada ya kujifungua.
d) Vitisho/kutishia uhai wa binadamu: Bw.Mwatela alimwambia Kananda ya kuwa kama angemwambia
Mama Sami/Maria (bibi yake)angemuua.
e) Kutumiwa vibaya kwa vijakazi: Bw.Mwatela alitumia nafsi yake kama mwajiri kumtendea Kananda
unyama ule.
f) Ndoa za lazima:Kananda aliozwa kwa dereva wa malori ya shehens kinyume cha mapenzi yake.
g) Utumwa: Dereva wa malori ya shehena alimuuza Kananda kama mtumwa kwa mtu mwingine.
h) Wizi au kunyang’anya watoto: Bw. Mwatela alimnyang’anya Kananda mwanawe.
i) Uchochezi: Bw. Mwatela alimchochea Mwakitawa dhidi ya mtu yeyote asiyemjua.Jambo hili
lilisababisha Kananda kuumizwa kwa jiwe na Mwakitawa kwa manati.
(zozote 3x2=6)

20 marks

5. SEHEMU E: (Alama 20)

USHAIRI
8.

(a) SHAIRI A(i)Tathnia(uwili)
(ii)Kikwamba-neno ‘’hofu’’ huanza kila mshororo wa kwanza.
(iii)Masivina-vina vyote kutofautiana.
(iv)Mandhuma-ukwapi unatoa wazo,utao unatoa jibu. (2x1=2)
SHAIRI B:(i)Utenzi-kipande kimoja.
(ii)Tarbia-mishororo mine.(2x1=2)
(b)Kama unataka haki yako,ni lazima uwe tayari kufa,na mwingine afe/kuua mwingine.(Al 4)
(c)(i)Takriri-neno hofu,mwanamke.
(ii)Tashihishi/uhuishi-zinazowapanda.
(iii)Tashbihi-kutumiwa ja rungu/uhuru ja ini la faru. (2x2=4)
(d)(i)Inkisari-hakiyo-haki yako.
Aso-asiye.
(ii)Tabdila-sharuti-sharti.
(iii)Msamiati wa kikale/jadi-ja. (3x1=3)
(e)(i)Ja-kama/mithili/mfano wa.
(ii)Sharuti-lazima.
(iii)Utukufu-mamlaka/cheo.
(iv)Baidi-tengana. (3x1=3)

20 marks

Back Top