Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 15

Kiswahili Paper 1

1.

1. Sura ya barua rasmi –barua kwa mhariri.

-Anwani mbili

-Tarehe

-Mtajo/

-Kuhusu,(KUH),MINT:YAH. –kichwa cha ujumbe)

-Mwili wa barua-Hoja zisizopungua tano zilizojadiliwa kikamikifu kiaya.

-Hitimisho

-Tamati

-Sahihi Hoja muhimu

a. Idadi inayofaa ya walimu idumishwe shuleni.

b. Kuwepo kwa vitabu vya kutosha shuleni.

c. Maktaba za shule na umma zijengwe.
d. Maabara yajengwe ili kuboresha utafiti.

e. Nidhamu ya wanafunzi na walimu idumishwe.

f. Ukaguzi wa mara kwa mara uwepo shuleni.

g. Wanafunzi wapewe mazingira bora.

h. Wazazi wahimizwe walipe karo kwa wakati ufaao.

i. Ushauri ufaao upewe wanafunzi.

j. Ushirikiano udumishwe baina ya washika dau wote.

k. Kuandaa ziara za kimasomo kwa wanafunzi.

l. Walimu na wanafunzi wanaobobea watuzwe.

20 marks

2.

2. Maana ya msamiati.

Kustawisha – kuimarisha/kuinua/kuboresha Iwe na nguvu/madhubuti/imara.

Uliosambaratika-ulioharibika/uko katika hali mbaya. Njia za kutumia

a. Kukomesha ufisadi.

b. Ujenzi na upanuzi wa viwanda.

c. Kuongeza nafasi za elimu.

d. Kuimarisha usalama/amani nchini.

e. Kuendeleza utafiti.

f. Mikopo kutolewa kwa raia kwa riba ya chini.

g. Kuhimiza watu kupenda na kuthamini bidhaa za humu nchini.

h. Kuwajibika na kupiga vita uvivu na uzembe.

i. Kuimarisha uchukuzi na mawasiliano.

j. Kuleta usawa wa kisheria.

k. Kuleta uhusiano mzuri kati ya Kenya na nchi zingine.

Tarbihi: Ikiwa mtahiniwa atazungumzia mambo haya katika wakati ulipita atakuwa amejitungia swali, atuzwe BK

(Bakshishi 01)

20 marks

3.

Swali la methali Mtahiniwa atunge kisa kinachounga mkono ukweli wa methali hii.

Yaani: Badiliko kwa mjukuu huanza na babu.

Maana ya methali -Jambo linalotarajiwa kubadilika au kuwa bora mbeleni huaza kushughulikiwa mapema.

Matumizi Hutumiwa kuwatahadharisha wale wanaosubiri hadi wakati wa mwisho kuanza kulishugulikia jambo.

20 marks

4.

Mwanafunzi asimulie kisa kuhusu habari aliyoipokea.

Habari yenyewe iwe ni kumwarifu jambo linalohuzunisha, linaloudhi, linalokera, lenye ukatili n.k.

-Aonyeshe namna alivyoipokea habari na hatua alizozichukua katiaka kushughulikia hali hiyo.

-Hatima ya mambo izungumziwe.

20 marks

Back Top