Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TEST 14

Kiswahili Paper 1

1.

(a) Swali la lazima.

Ripoti maalum/rasmi.

Insha idhihirishe mambo yafuatayo:

―Ni nani alitaka ripoti hiyo?

―Utafiti ulichukua muda gani?

―Orodha ya wanakamati.

―Matokeo.

―Mapendekezo.

―Hitimisho.

―Jina na sahihi ya mtafiti.

―Tarehe ya utafiti huo. Mtahiniwa akishughulikia nusu ya vipengele hivi atakuwa amezingatia sura ya insha.

(b) Baadhi ya hoja anazotarajiwa kuwa nazo mtahiniwa ni:

i. Ukosefu wa ajira/nafasi za kazi.

ii. Umaskini.

iii. Athari za vyombo vya mawasiliano ya kisasa k.v televisheni,sinema,mtandao,simutamba n.k.

iv. Malezi mabaya-wazazi wamepuuza jukumu lao la kuelekeza vijana.

v. Matumizi ya afyuni/mihadarati. vi. Kuibuka kwa makundi yanayosajili na kutoa mafunzo ya kihalifu kwa vijana.

vii. Ufisadi.

viii. Kutowajibika kwa walinda usalama.

ix. Mafundisho potovu kutoka baadhi ya viongozi wa kidini.

x. Uchochezi wa kisiasa.

xi. Kutoelimika.

20 marks

2.

2. Hili ni swali la hoja. Mtahiniwa anao uhuru wa kuunga pekee,kupinga pekee au kuunga na kupinga. Baadhi ya hoja za kuunga;

i. Shule nyingi zitahitajika kujengwa.

ii. Serikali italazimika kuajiri walinda usalama wengi.

iii. Kupungua kwa ardhi.

iv. Misongamano ya watu na magari k.v katika miji mikuu.

v. Rasilimali muhimu hupungua na hivyo kuibua mizozano.

vi. Uchafuzi wa mazingira utaongezeka. vii. Nafasi za kazi zitapungua.

viii. Ufisadi utakita mizizi-watu watashindania rasilimali zilizopo.

ix. Serikali itagharimika pesa nyingi kushughulikia majanga ya kitaifa.k.v ukimwi,njaa,gharika n.k.

x. Ongezeko la uhalifu.

xi. Gharama ya maisha itapanda. Tanbihi . Hoja za kuunga zionyeshwe kwa,

Baadhi ya hoja za kupinga;

i. Nchi itapata wafanyakazi na wataalamu wenye ujuzi mbalimbali.

ii. Taifa litajivunia kuwepo kwa mila na tamaduni tofautitofauti.

iii. Watu wengi huchangia kuwepo kwa soko kubwa la bidhaa zinazotengenezwa viwandani na kuzalishwa mashambani.

iv. Serikali itapata utajiri mwingi kupitia ushuru na kodi zizotozwa watu hawa.

v. Huchangia kusambaa kwa maendeleo kote nchini.
vi. Talanta na vipawa mbalimbali huzuka na hutumika kama kitega uchumi.k.m wanasoka,wanamuziki,wanariadha.n.k.

Tanbihi. Hoja za kupinga zionyeshwe kwa,

-Hakuna hoja nusu-zote zielezwe kikamilifu.

20 marks

3.

Ni swali la methali.

―Mtahiniwa atunge kisa kitakochobainisha maana na matumizi ya methali husika.

―Si lazima aeleze maana ya juu na ya ndani ya methali.

―Kisa chake kidhihirishe kwamba anayezembea kazi hubakia maskini huku mwenye bidii akitajirika na maisha yake kuwa bora.

20 marks

4.

―Hili ni swali la mdokezo.

―Mtahiniwa aanze insha yake kwa maneno aliyopewa.

Tanbihi Akianza kwa maneno mengine kando na aliyopewa au asiyahusishe kabisa,atakuwa amejitungia swali na atuzwe alama tatu.(3)

―Kisa chake kilenge kueleza yale yaliyotokea pindi tu mlango ulipofunguliwa-yawe ya furaha au ya kuhuzunisha.

―Baadaye anaweza kujikita kwenye mbinu rejeshi na asimulie yaliyokuwa yamejiri hadi mgonjwa akaletwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Tanbihi. Mtahiniwa anashauriwa kutumia mwongozo huu pamoja na ule wa kudumu ili kuweza kukadiria insha ya mtahiniwa na hivyo kumweka katika kiwango chake.

20 marks

Back Top