Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2016 Pre KCSE

Kiswahili Paper 2

1.UFAHAMU (Alama 15)

Soma makala yafuatayo kisha ujibu mswali
1.

Mafuta yanayopatikana kwenye fukwe za bahari, moshi wa magari, takataka na bidhaa nyinginezo
zinazotupwa hapa na pale ni vichafuzi vya mazingira. Vichafuzi huathiri afya zetu na kuathiri wanyama pamoja na mimea. Wanadamu wanyachafua mazingira yao kwa kila aina ya bidhaa mbaya zakikemikali zinazotoka viwandani au kwenye viwanda vya kawi au nguvu. Bidhaa hizo ni matokeo ya maisha ya siku hizi anayosihi binadamu.

Licha ya ukweli huu, ni muhimu kujua kuwa uchafuzi wa mazingira haukuanza leo. Miaka na miaka
iliyopita, viwanda vimekuwa vikitoa mawingu makubwa ya moshi wenye sumu. Hata hivyo, uchafuzi wa mazingira umeongezeka maradufu kutokana na kuongezeka kwa viwanda. Uchafuzi umesambaa ardhini, kwenye anga na majini. Msambao huu unapatikana katika pembe zote za ulimwengu wetu. Je, kuna aina zipi za uchafuzi?

Kwanza kuna uchafuzi wa halianga. Huko juu angani kuna tabaka linalojulikana kama ozoni. Tabaka hili huwa ni ama ya gesi ya oksijeni na linaunda kinga fulani dhidi ya miale ya jua. Miale hiyo ya jua huweza kusababisha saratani ya ngozi inapomfikia binadamu. Hata hivyo, uchafuzi wa mazingira unaelekea kuliathiri tabaka hili. Vilevile baadhi ya kemikali zinazotumiwa katika friji au jokofu au kwenye mikebe ya marashi ya kupulizia na upakiaji bidhaa, huu haribu ukanda huo.

Aina nyingine ya uchafuzi ni ile tunayoweza kuuita uchafuzi wa kiajali. Huu ni uchafuzi ambao hutokea kama ajali, yaani binadamu hatendi kimakusudi. Mfano mzuri ni meli inayovuja mafuta baharini. Mafuta haya huwaathiri na kuwaua wanyama wanaoishi baharini kama samaki na ndege na hata kuyaharibu mazingira yenyewe.

Miji mikubwa hukumbwa na uchafuzi mwingine unaohusiana na kuwako kwa idadi kubwa ya magari.
Magari haya hutoa moshi unaochanganya gesi ambazo huungana na nyingine zinazoletwa na viwanda vikubwa. Mchanganyiko huu unapoungana na maji, husababisha mvua ya asidi. Mvua hili huweza kuiua mimea. kuathiri majengo na hata kuwaua wanyama wa pori ambao huenda wakayatumia maji hayo. Magari hutoa moshi uliochanganyika na madini aina ya risasi ambayo huweza kuathiri siyo tu mazingira bali pia mfumo wa akili wa binadamu.

Uchafuzi mkubwa unaopatikana katika mazingira mengine yetu ni utupwaji ovyo wa takataka. Fauka ya hayo, watu hufukia ardhini takataka ambazo huweza kuwa na matokeo mabaya kwa sababu ya kupenyeza kwenye udongo na maji yanayotumiwa na watu na mimea. Kila siku tunatupa takataka bila ya kujali wala kubali. Takataka hizi ni kama makopo, mifuko ya plastiki,mabaki a sigara au maganda ya matunda. Baadhi ya takataka ni hatari kwa wanyama na nyingine huweza pia kusababisha majanga kama moto. Aidha, takataka hizi hufanva mazingira yetu yaonekane machafu.

Sote tunajukumu kubwa la kuchangia kupunguza uchafuzi wa kimazingira ya kwanza ni kuelimishana na kutambua umuhimu wa usafi wa mazingira yetu. Tunapaswa kutia takataka zetu katika vijalala maalum au mahali tunapoweza kuzichoma na kuziteketeza. Njia nyingine ni kuhakikisha kuwa tunatunza vitu kama mifuko, chupa na kadhalika ambavyo huweza kuunda upya na kutumiwa tena. Hali kadhalika, katika miaka ya hivi karibuni. kumekuwapo na juhudi za kuwahimiza wenye magari kutumia mafuta ya gari ambayo hayana madini ya risasi. Kwa njia hii tutasaidia kuyaboresha mazingira yetu. Vilevile pana umuhimu wa kutilia mkazo utumiaji wa bidhaa ambazo zinaweza kuoza na kuvunjikavunjika au kusagika na kuwa sehemu ya udogo. Hatua ya kwanza ya kupambana na uchafuzi wa mazingira ni kujielimisha na kuwajibika.

Kila mmoja akitoa mchango wake tutafanikiwa. Kumbuka kuwa kinga na kinga ndipo moto uwakapo.

Maswali :
(a) Vichafuzi ni nini ? (alama 1)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(b) Ongezeko la viwanda limechangaije uchafuzi wa mazingira ? (alama 2)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(c) Tabaka la ozoni huathiriwaje na uchafuzi? (alama 2)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(d) Athari zipi zitatokea iwapo mazingira hayatatunzwa ? Fafanua. (alama 4)
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(e) Kwa nini miji mikubwa hukumbwa na uchafuzi kuliko sehemu zingine ? ( alama 2)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(f) Eleza nui mbili za uchafuzi wa mazingira zilizotajwa katika kifungu hiki. (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(g) Eleza maana za misamiati ifuatayo kama ilivvotumiwa katika kifungu. (alama 2)
(i) Msambao
………………………………………………………………………………………………………………
(ii) Mazingira
………………………………………………………………………………………………………………

15 marks

2. UFUPISHO (Alama 15)

Soma taarifa ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata kulingana na maagizo.
2.

Utoaji wa Huduma ya Kwanza.
Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji. Watu wengi ambao hujitolea kutoa majeruhi baada ya ajali kama za barabarani, maporomoko ya ardhi au nyumba huwa hawangamui hata chembe jinsi ya kukabiliana na uokoaji. Hatima ya juhudi zao ambazo hulenga kutenda mema ni kuathirika zaidi kwa majeruhi.

Hali ya ukoaji inaweza kurekebishwa kwa kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa umma. Elimu hii yahitajika na kila Mkenya kwani mikasa ya ajali za barabarani na nyinginezo inaendelea kutokea kila siku.

Ajali zinazotokea, si ajabu kuona makundi ya waokoaji wakibeba majeruhi hobelahobela bila kuzingatia madhara wanayoweza kuwaongezea kutokana na ubebaji wao. Kutojua namna ya kumbeba majeruhi kunaweza kumhatarisha na hata kusababisha kifo.

Kuna mambo mbalimbali ambayo makundi ya waokoaji yanatakiwa kuzingatia wakati yanatoa huduma ya kuokoa. Kwanza ni muhimu kuchunguza kama kuna hatari yoyote inayoweza ikatokea na kuwatia majeruhi na waokoaji hatarini zaidi. Makundi ya waokoaji yameweza kwa kuliingilia eneo la ajali mbumbumbu kama mzungu wa reli.

Hatua ya pili ni kutafuta idadi ya majeruhi. Pana uwezekano wa majeruhi kutupwa mbali na eneo la ajali. Vivyo hivyo, kuna majeruhi ambao huweweseka haada ya ajali na kuanza kutembea wasijue wanakoelekea. Wengi wao huaanguka karibu na eneo la ajali au wakaenda mbali.

Hatua ya tatu ni kuchunguza kama majeruhi amezimia. moyo unapiga riajinsi anavyopumua. Ili kuhakikisha kuwa majeruhi anapumu, mwokoaji atazame kama kifua kinapanda na kushuka. Halikadhalika, mwokoaji anaweza kusikiliza au kuguza kifua na kuona kama kuna ishara za kupumua. Iwapo majeruhi anapumua. mokoaji ameke katika hali ambayo itaimarisha kupumua kwake. Anaweza akamlaza chali au kumgeuza kwa pamoja na kichwa chake ili kufungua mkondo wa hewa. Pia mwokoaji ahakikishe hamna chochote kinywani kinachoweza kumsakama. Ikiwa hapumui, mwokoaji anaweza kujaribu kumfanya apumue kwa kupuliza hewa mdomoni mwake.

Fauka ya hayo, Upulizaji wa hewa utahakikisha kuwa damu inazunguka mwilini vizuri.
Hatua nyingine ni kuchunguza vile amejeruhiwa. Chunguza kama majeraha ni vidonda tu au kuna kuvunjika kwa mfupa na kubainisha ni mfupa upi. Haya yatamwezesha mwokoaji kujua jinsi ya kumbeba majeruhi. Pakiwa na kuvunjika kwa mfupa, ni muhimu kutotumia kiungo kiliehovunjika anapobebwa.

Pia kuchunguza vile majeruhi amejeruhiwa, humwezesha mwokoaji kujua huduma ya dharura atakayotumia. Majeruhi akiwa anavuja damu sana, ni muhimu kuzuia uvujaji huu. Iwapo ni kidonda kidogo, kinahitaji kufungwa ili kuzuia uambukizaji. Mwokoaji anaweza kutumia kifaa chochote kilicho karibu kutolea huduma hizi. Kwa mfano, anaweza kupasua nguo ya majeruhi iii apate kitambaa cha kusaidia kuzuia kuvuja kwa damu au kumfunga kidonda.

Hatua inayofuata ni kumhamisha majeruhi toka eneo Ia ajali hadi hospitalini. Mwokoaji anaweza kuwatumia watu wengine kutafuta msaada. Wanaweza kupiga simu wakitumia nambari za simu za dharura kama zile za polisi, wazimamoto au makundi ya wataalamu wa shughuli za ukoaji. Nambari hii ya simu huwa 999 popote na huwa haina malipo. Wanaopiga simu ni vyema kutoa maelezo ya mahali ambapo ajali imetokea, ama ya ajali na huduma za dharura zinazohitajika pamoja na idadi ya majeruhi. Iwapo makiindi haya ya ukoaji yameahidi kufika bora kuwasubiri.

Ikiwa makundi ya wataalamu wa ukoaji hayakupatikana, ni jukumu Ia mLoai hakikisha majeruhi wamehamishwa na kupelekwa hospitalini. Majeruhi wakiwa wengi. ni born kuanza na wale waliozimia au wenye matatizo ya kupumua kisha kuwaendea wanaovuja damu sana. Baadaye mwokoaji awasaidie waliovunjika mifupa huku akimalizia na wenye majeraha yasiyohatarisha maisha. Ni muhimu kuwabeba majeruhi kwa kutumia machela. Hii hupunguza kuathirika zaidi kwa majeruhi. Iwapo hamna machela karibu, mwokoaji anaweza kuunda moja kwa kutumia vipande viwili vya mbao, blanketi. shuka au makoti.

Ujuzi wa huduma ya kwanza ni mojaapo a mambo muhimu ambavo kila mtu anapaswa kuwa nayo.

Maswali :
(a) Fupisha aya tatu za kwanza kwa maneno 50 – 60 (alama 5 ut.1)
Nakala chafu

Nakala safi

(b) Eleza kwa kutumia maneno 90-100, hatua zinazotakiwa kufuatwa wakati wa uokoji. (alama 7 ut.2)

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

3.

(i) Taja vigezo viwili vya kizingatiwa katika kuweka konsonanti katika makundi ( alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(ii)Taja sifa bainifu ya sauti za vokali (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………………

3 marks

4.

Tambua jinsi neno mgeni lilivyotumika katika sentensi zifuatazo.
(i) Mwanafunzi mgeni amesajiliwa shuleni
………………………………………………………………………………………………………………
(ii) Mwanafunzi aliyesajiliwa shuleni ni mgeni
………………………………………………………………………………………………………………

4 marks

5.

Tunga sentesi mojamoja kubainishi :
(i) Kiwakilishi huru (ngeli ya li-ya wingi)
………………………………………………………………………………………………………………
(ii) Kiwakilishi kiambata nafsi ya kwanza wingi
………………………………………………………………………………………………………………

4 marks

6.

Andika sentensi ifuatayo upya ukibadilisha vitenzi vilivyopigiwa mstari katika kinyume
Mwanafunzi alisimama kisha akakitega kitendawili.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………

2 marks

7.

Tugna sentensi yenye maneno uliyopewa hapa
W + U+ N + T + T + E
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………

3 marks

8.

Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wastani umoja.
Vijibwa vya walowezi viliuawa na watoto ya maskini
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………

2 marks

9.

Tumia hali ya –po- kutunga sentensi ili kuleta dhana ya
(i) Wakati maalum ( alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
(ii) Wakati usiodhihirika ( alam 2)
………………………………………………………………………………………………………………

4 marks

10.

Eleza tofauti kati ya sentensi hizi :
(i)Nisingelifika mapema ningelimkuta mwalimu darasani.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(ii) nisisgenelifika mapema nisingelimkuta mwalimu darasani.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………

4 marks

11.

Tunga sentensi mojamoja kwa kunyambua vitenzi ulivyopewa kulingana na hali kwenye mabano
- fa (kutendea) ( alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
- la ( kutendesha) ( alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………

4 marks

12.

Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
Rais na naibu wake wameahidi kupunguza mishahara yao.

4 marks

13.

Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi :
Watahiniwa wa kidato cha nne walikumbushwa na mwalimu mkuu kuwa mtihani wao wa mwigo ungeanza mwezi wa Agosti, kisha akawahimiza wasome kwa bidii.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………

3 marks

14.

Tumia kiambishi ndi kutunga sentensi ili kuonyesha dhana ya msisitizo katika ngeli k i-zi wingi.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………

2 marks

4. ISIMU JAMII (Alama 10)

15.

(a) Eleza maana ya sajili ya lugha (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(b) Fafanua mambo manne yanayosababisha kuibuka kwa sajii tofauti. (alama8)

10 marks

Back Top