Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2016 KCSE 4MCK Joint Exam

Kiswahili Paper 2

SEHEMU A: UFAHAMU (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali yafuatayo.
1.

Wanawake, wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika kchi zinazoendelea ni baadhi ya watu
waliotopea na kubobea katika uchochole mkubwa. Jumla ya idadi kubwa ya wanawake hawa wanaoishi chini ya kiwango cha chini cha umaskini inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 6000. Hii ni idadi kubwa hasa ikikumbukwa ni asilimia kubwa ya wanawake wanaoishi kwenye maeneo haya.

Ulimwengu umeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu pamoja na kuwalo kwa matatizo ya kiuchumi duniani. Kadhalika matatizo mengine ni mitafuruku na vita vya kikabila, majanga ya kiasili mathalani mafuriko, ukame na milipuko ya volcano. Usisahau pia kuwa kuna uharibifu wa kimazizingira, mabadiliko ya desturi na kusambaratika kwa familia na misingi yake. Tatizo ligine ni kuwa kuna kuongezeka kwa hali ya wanawake kuwa wazazi pekee na hivyo kuongeza familia zinazosimamiwa na wanawake (ambao tumewataja kuwa wanakumbwa na umaskini mkubwa).

Wanawake wanaoishi mashambani wanakumbwa na makubwa. Kwanza, kama maskini wanaishi katika mazingira magumu. Vile vile kama wanawake wanakabiliana na mapendeleo ya kisera na kitamaduni yanayowadharau na kuwapuuza wanawake wana mchango wao katika maendeleo. Tatu, kama viongozi wa familia, hasa wanaolea na kutunza jamaa za mzazi mmoja, wanapambana na uongozi wa familia pamoja na uzalishaji. Aghalabu hawapati usaidizi wowote katika majukumu kama haya bali wanalazimika kupambana nayo peke yao. Kutokana na hayo yote wanawake hawapati nafasi nzuri kushitikii katika maamuzi ya maswala yanayowahusu. Maswali mengi yanamuliwa na wanaume pasipo kuwahusisha Wanawake.

Licha ya dhiki yao kubwa, wanawake hawa wanachangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa njia mbali mbali. Mchango huu unaonekana katika kiwango cha jamii, taifa na familia . Katika kiwango cha kijamii na kitaifa wanawake chio hanzo cha nguvukazi kwani ni wao na watoto wao wanaotekeleza kazi nyingi hasa za nyumbani na mashambani. Mara nyingi huwa na uwezo bora wa kutunza chochote Waliocho nacho kuliko wenzao wanaume.

Kifamilia wanawake wa mashambani wanashugulika mchana kutwa katika hali ngumu ya hewa aifha jua kali au mvua wameeleka wanao migomgoni mashambani ili kupata chakula kwa familia zao. Jukumu la kuandaa chakula nyumbani bado linaachiwa wale wale wanawake wanaokizalisha mashambani.

Jambo lisilopingika ni kwamba wanawake wanatekeleza majukumu makubwa ba muhimu katika kizazi cha binadamu na ndio hasa mihimili ya jamii yoyote staarabu. Kwa hivyo, ni kinaya kitupu kudhalikisha wanawake. Mataifa mengi yaiiyoendelea ni yake yaliyoondoa vikwazo vyao mbele ya wanawake na kuwaacha watekeleze wajibu wao. Kadhalika wanaume wa huku wanawaona wanawake kuwa wenzao katika kujenga jamii sio watumwa au watumishi wao wanaoumia na kutumikishwa kama vifaa na bidhaa.

Inafaa jamii zinazodumisha wanawake zitambue kuwa ubaya wa tendo hili sio tu kudumaza maendeleo yake hali pia kutoa mfano mbaya kwa vijana ambapo wataendeleza ukandamizaji huu kwa vizazi vijavyo. Kwa hivyo, jamii inawabijika kutenda lililo sawa kwa kuwapa hadhi wanawake wote.

Maswali
a)Ipe tarrifa hii anwani mwafaka. (Al.1)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
b)Nakili maafa matatu ya kimaumbile yaliyotajwa katika kifungu hiki. (Al. 3)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
c)Eleza sababu tatu zinazowazuia wanawake kushitiki katika maamuzi ya masuala yanayowahusu
kulingana na makala hay. (Al. 2)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
d)Wanawake hutekeleza majukumu gani katika jamii na taifa kutokana na makala haya? (Al. 3
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
e)Kuna tofauti gani baina ya wanawake wa mataifa yaliyoendelea nay ale ambayo hayajastawi. (Al. 2)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
f)Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye taarifa. (Al. 3
uchochole
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………

ii)kudhalilisha
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
iii)mitafuruku
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………

15 marks

SEHEMU B: MUHTASARI (Alama 15)

Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali.
2.

Ustawishaji wa Kiswahili ni shughuli ya kila mtu. Kunahitajika ushirikiano baina ya wananchi, wasomi, wanasiasa, vyombo vya habari na asasi mbalimbali za elimu, kila mojawapo ikitoa mchango mahususi katika juhudi za kuikuza na kuindeleza fahari hii ya Mwafrika.

Hata hivyo magazeti ndio uti wa mgongo katika ustawishaji wa Kiswahili kwa sababu yanatoa mchango mkubwa zaidi. Magazeti ya Kiswahili ni kiungo muhimu baina ya wasomi na wananchi wa kawaida. Musuala ya kinadharia yanayojadiliwa na wasomi vyuoni kuhusu lugha na fasihi
hayana maana yoyote iwapo hayatajitokeza katika matumizi ya lugha na fasihi magazetini kwa manufaa ya umma. Wananchi nao wanaweza kuwasiliana na wasomi hao kupita magazeti hayo.

Usomaji wa msamiati na istilahi hizo zilivyotumiwa katika magazeti ndipo wasomaji na wapenzi wa
Kiswahili wanaweza kujua kuzuka kwa msamiati na istilahi, na matumizi yake. Baadhi ya magazeti yako Safu zinazoshughulikia lugha ya Kiswahili na msamiati wake. Tahakiki za vitabu vipya vya Kiswahili zinaweza kuchaapishwa magazeti ili wanafunzi, walimu na wasomaji kwa jumla
wafahamishwa kuhusu kuwepo kwa vitabu na ubora wa vitabu vyenyewe.

Magazeti ya Kiswahili pia yanaweza kutumiwa kueneza ukweli kuhusu historia ya Kiswahili na matumizi sahihi ya lugha hii. Ikilinganishwa na redio, magazeti hutoa kumbukumbu ambapo unaweza kurejelea.

Inashangaza kuwa wakati mwingine, lugha ya Kiswahili ‘inabomolewa’ kisarufi na kimsamiati katika
magazeti ya Kiswahili.Si muhali kusome gazeti lililoja makosa ya hijai na kimsamiati. Makao mengine
huwa yanatokana na tafsiri mbovu inayofanywa. Kwa bahati mbaya, baadhi ya magazeti
hutegemea habari zilizoandikwa kwa Kiingereza hili kutafsiri. Pia makosa mengi huwa ni ya kisarufi
Na kimamtiki ambayo husababishwa na mazoea ya kuzungumza na kuandika Kiingereza.

Hata hivyo, ikumbukwe kwamba kuna mtindo wa matumizi ya lugha, yaani sajili inayokubalika
magazetini na I na sifa maalumu. Kuna wakati ambapo misingi ya sarufi ya lugha inaweza kukiukwa
kukidhi mahitaji ya matumizi ya lugha katika muktadha fulani.

Magazeti ya Kiswahili yanapotumiwa hivyo, yanaweza kustawisha lugha hii na wakati huo
kuwafahamisha, kuwaelimisha na kuwaburudisha wananchi kikamilifu. Haya yanawezekana kupitia
Uandishi wa habari, makala, matangazo, vibonzo, mafumo, hadithi, maoni, mijadala ya umma kuwa
masuala ibuka kama vile siasa, mazingira, katiba, utawala na kadhalika.

Isitoshe, magazeti yanaweza kutumiwa kama chombo muhimu cha kuhakiki matumizi ya lugha ya
Kiswahili katika vyombo vingine vya habari kama vile redio na runinga. Yanaweza pia kutumiwa
kuhakiki matumizi ya Kiswahili vitabuni, shuleni, ofisini, bungeni, katika vituo vya polisi na mikutano ya kisiasa na sehemu nyinginezo za utumishi wa umma zinazotarajiwa.

MASWALI
a)Kwa nini magazeti ni muhimu katika ustawishaji Kiswahili na jamii kwa jumla? (maneno 60-70).
(al. 10) 2 (mtiririko).
Matayarisho

8 x 1 = 8

b)Ni matatizo gani yanayokumba matumizi ya Kiswahili magazetini? (30-40). (al. 5)
(1 mtiririko)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
4 x 1 = 4 + 1

15 marks

SEHEMU C: (Alama 40)

MATUMIZI YA LUGHA.
3.

Eleza sifa bainifu za sauti /j/
……………………………………………………………….
……………………………………………………………….

2 marks

4.

Taja sifa tatu za silabi.
.………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………

3 marks

5.

Tenganisha silabi katika neno.
Ustadhi.
…………………………………………………………………………….. ½ x 4 = 2

2 marks

6.

Taja vitenzi vya silabi moja ambavyo huwa na maana zaidi ya moja.

i)………………………………………………………………………………………………………………………….
ii)Tumia mojawapo ya vitenzi ulivyotaja kutunga sentenzi mbili kubainisha maana mbili tofauti. (al. 2)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………

2 marks

7.

Tumia neno ‘katili’ kama
i)Kielezi (al. 1)
………………………………………………………………………………………………………………..
ii)Kivumishi. (al. 1)
………………………………………………………………………………………………………………..

2 marks

8.

Bainisha hali zilizo katika sentensi zifuatazo. (al. 2)
i)Watu wenyewe watembea kwa haraka.
………………………………………………………………………………………………………………..
ii)Msafara utakuwa umekaguliwa, maarusi watakapowasili. (al. 2

…………………………………………………………………………………………………………….

4 marks

9.

Bainisha aina za vivumishi katika sentensi hii.
Kitabu changu ni hiki kilichochorwa picha mbili nadhifu.
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………

4 marks

10.

Eleza maana ya sentensi hii ukizingatia kauli ya kutendama.
Mfupa wa samaki ulimsakama kooni.
…………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………

2 marks

11.

Andika sentensi hii iwe katika usemi halisi.
Mwashigadi alimwambia shangazi yake kuwa angempokea mjomba iwapo angempata.
…………………………………………………………………………………………………………………

2 marks

12.

Changanua sentensi hii kwa kutumia vishale.
Tulimtembelea mgonjwa jana hospitalini.
………………………………………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
8 x ½ = 4

4 marks

13.

Andika Katika wastani wingi.
Kibuzi kilikiharibu kijiche changu
…………… …………………. ……………… ……………….

2 marks

14.

Onyesha matumizi mawili ya nukta mkato.
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………

2 marks

15.

Eleza maana ya shamirisho kipozi.
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………

1 marks

16.

ambulisha kiima na chagizo.
Alifika kwangu asubuhi.
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………

2 marks

17.

Tunga sentesi kudhihirisha matumizi mawili ya ku.
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………

2 marks

18.

i)Eleza dhana ya kishazi tegemezi. (al. 1)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
ii)Tunga sentensi moja yenye vishazi viwili tegemezi. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………………………

2 marks

SEHEMU D: ISIMU-JAMII (Alama 10)

19.

SEHEMU D: ISIMU-JAMII (al. 10)
Eleza uhusiano uliopo baina ya Kiswahili na lugha za kibantu.
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………..
……………………………………………………………………………………………………………….

10 marks

Back Top