Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2015 KCSE Tharaka South Joint Examination

Kiswahili Paper 2

1.UFAHAMU (Alama 15)

Soma taarifa inayofuata kasha uyajibu maswali
1.

Maisha ya binadamu ni kimoja kikubwa. Hebu jiulize jinsi uhai wako wewe mwenyewe ulivyoanza sembuse unavyoweza kupumua na kuishi siku nenda siku rudi.
Dini zimefahamisha kuwa sisi binadamu tumeubwa na Mwenyaezi Muumba. Hata hivyo Muumba hutumia mume na mke kutuanzishia maisha yetu humu duniani. Uhai wa hapa duniani huanzia katika tumbo la mwanamke muda mfupi tu baada ya mume na mke kushirikiana katika tendo la kujamiina. Katika ngono hii yenye ufanisi, mbegu moja ya manii kutoka kwa mwanaume, hudunga na kujiingiza katika yai la mwanamke huku ikilirutubisha.

Tangu hapo mtu huwa na mama akawa mjamzito. Hatua ya kwanza ya uhai?
Wanayansi wametuthibitishia kuwa mbegu katika shahawa kutoka kwa mwanaume ina kromosomu ishirini na tatu nalo yai la mwanamke lina idadi iyo hiyo ya krosomomu. Basi katika hatua ya kwanza ya uhai wake, binadamu ana kromosomu arubaini ba sita, krosomomu hizo zote ndizo humfanya mtu kuwa mkamilifu kwa kukadiria mambo mbalimbali adhimu. Kwa mfano, hukadiria kama kiumbe kitakuwa cha kike au cha kiume, mtu mweupe au mtu mweusi, mwerevu au wa wakia chache, mwenye nywele za singa au za kipilipili, atakuwa na damu ya namna gani, michoro ya vidole vyake itakuwa vipi na hata utu wake utakuwa wa namna gani katika siku za usoni.

Elimu yote anayopata mtu kutoka kwa jamii na mazingira huweza tu kujenga, juu ya yaliyokwisha
kuanzilishwa na krosomomu katika yai lililorutubishwa tumboni.
Haihalisi kabisa kufikiria kwamba katika hatua za mwanzo tumboni mwa mama kiumbe huwa katika hali ya ukupe. La hasha!yeye hujitegemea kwa vyovyote na ana upekee wake. Hatangamani na mama yake. Roho yake humdunda mwenyewe na damu yake ambayo huenda ikawa tofauti kabisa nay a mama yake, humtembea na kumpiga mishipani mwake. Isitoshe, yeye si mojawapo katika viungo vya mwili wa mama yake vinavyomdhibiti katika himaya yake ndogo.

Amini usiami, hapana binadamu hata mmoja ambaye amewahi kuwa sawa kimaumbile na mwingine na wala hatakuweko. Hata watoto pacha kutoka yai moja la mama hawawi sawa, lazima watatofautiana. Si nadra kusikia mtu amepata ajali akahitaji msaada wa damu, na pakosekane kabisa mtu hata mmoja kutoka jamaa yake wa kumwauni. Basi ukistaarajabu ya Musa utaona ya Firauni.

a) Andika anwani mwafaka ya taarifa uliyosoma. (alama 1)
b) Mwandishi ana maana gani anaposema ‘ngono yenye ufanisi’? (alama 2)
c) Uchunguzi wa sayansi umekita mzizi imani gani ya kidini? (alama 2)
d) Taja majukumu yoyote manne yanayotekelezwa na kromosomu. (alama 4)
e) Katika makala, elimu kutoka kwa jamii na mazingira yaelekea kuwa bure ghali. Kwa nini? (alama 2)
f) Eleza maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika makala: (alama 4)
i) Siku nenda siku rudi.
ii) Huwa katika hali ya ukupe
iii) Kumwauni
iv) Himaya

15 marks

2. UFUPISHO (Alama 15)

Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali uliyopewa
2.

Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi, binadamu ndiye kiumbe aliyepevuka zaidi katika fikra kuliko viumbe wengine. Anasemekana kuwashinda viumbe wengine kwa njia nyingi,hata kuweza kuwatala na kuwaratibia maisha yao. Binadamu amepewa uwezo wa kuyatawala mazingira na kukabidhiwa ufundi wa kuweza kuunda vifaa mbalimbali ili kuyakabili mazingira hayo. Uwezo huu ndio umemwezesha kukimu mahitaji ya kizazi kimoja hadi kingine kwa miaka na mikaka. Hata hivyo, kuna tofauti kubwa kati ya binadamu na wanyama. Tofauti hii inaweza kumvua binadamu sifa zake zote na kuuona ukwasi wa maarifa yake kama ishara ya maangamizi ya ulimwengu. Hii ni kutokana na hasara anayosababisha katika mazingira tulivu waliyoumbiwa viumbe wote na Muumba wao.

Lakini ifahamike kuwa mandhari ya ulimwengu tunamoishi humpendeza kila kiumbe, mathalan hewa safi itokayo miliamini, chemichemi za maji, mito na vijito mnamotiririka maji safi, vilele vya milima vilivyofunikwa kwa theluji daima dawamu, yakiwemo mabonde na tambarare zinazohimili uhai wa viumbe wengi.

Vilevile ibainike kuwa uzuri huu wa kiasili hauwezi kufikia kilele bila vichaka na misitu inayoipamba ardhi hii huku ikileta mvua. Mapambo yote haya ni kwa nguvu za maumbile; nguvu ambazo hazisababishwi na kuwa hatari kwa uhai wa binadamu na viumbe wenzake kwa sababu anayaharibu maumbile kwa kiasi kikubwa kinachomtisha binadamu mwenyewe.

Sababu mojawapo ni uchafuzi wa maji kama rasilmali muhimu ya kiasili. Uchafuzi huu umeathiri viumbe na mimea pakubwa, yakiwemo maradhi mbalimbali. Kwa kweli bila maji, uhai utatoweka duniani. Uharibifu mkubwa wa maji machafu yenye sumu hasa kutoka viwandani na kuingia kwenye mito na bahari, huwadhuru viumbe wengine wenye makao majini. Maji huleta madhara sit u kwa mimea bali hata kwa binadamu kupitia kwa ulaji wa vyakula.

Binadamu ameharibu misitu kwa ukataji wa miti kihoela hasa kwenye sehemu za chemichemi. Hali hii husababisha uhaba wa mvua ambao huleta kiangazi kinachokausha mimea na visima vya maji.
Ujenzi wa viwanda hasa katika nchi zilizostawi unaelezwa na wanasayansi wanaohusika na hali za anga kuwa umesababisha taharuki na wasiwasi mwingi. Hii ni kwa sababu umeonyesha kuharibu utandu unaozuia miale ya jua kupenya moja kwa moja kwenye sayari hii na hapo kuhatarisha uhai. Hii ni kutokana na hewa chafu itokayo viwandani. Kadri binadamu anavyochangia pakubwa katika kuondoa polepole uhai wa viumbe wote ulimwenguni.

Warsha nyingi zimefanywa ili kutahadharisha ulimwengu dhidi ya uharibifu wa mazingira na maliasili.
‘Ajenda’ za mikutano hiyo hasa zinalenga nchi zilizostawi kwani hizi ndizo zinazochafua mazingira kwa kasi zaidi kuliko zile zinazostawi.

Mapendekezo mengi yametolewa katika vikao hivyo ili kusulihisha tatizo hili lakini ni hatua chache mno zinazochukuliwa kurekebisha mambo haya. Itakuwa bora zaidi ikiwa watu watajipa jukumu la kusafisha mazingira yao. Watoto wafunzwe jinsi ya kuhifadhi mazingira yanapochafuliwa. Wakumbuke kuwa utumwa si karaha kwa sababu afya zetu na viumbe wengine zimo hatarini ikiwa mazingira yatachafuliwa. Kwa hivyo, ni jukumu la kila mmoja wetu kutunza mazingira anamoishi kwa manufaa ya leo na kesho. Viongozi wanaohudhuria kongomano la kila mwaka maarufu kama ‘KYOTO PROTOCAL’wahakikishe kuwa maazimio yote ya kulinda mazingira yametekelezwa, na sheria
kali kuidhinishwa dhidi ya raia wao, la sivyo, siku zijazo kutakuwa na mafuriko mengi ambayo yatasababisha visiwa na sehemu zote za Pwani kufunikwa na maji.

a) Eleza kwa ufupi hasara zinazoweza kusababishwa na uharibifu wa mazingira. (Tumia maneno 45- 55) (alama 1
kwa mtiririko) (alama 5)
b) Eleza hatua ambazo mwanadamu anapaswa kuchukua ili kupunguza madhara ya upanuzi wa viwanda. (Tumia
maneno 45) (alama 1 kwa mtiririko) (alama 6)

15 marks

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

3.

Kimadende hutamkwa vipi?

1 marks

4.

Bainisha chagizo na shamirisho katika sentensi ifuatayo:
mjukuu alipasua kuni asubuhi

2 marks

5.

Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mstari:
Nyumba yao mpya itafunguliwa kesho jioni.

5 marks

6.

Unda nomino moja moja kutoka na vitenzi vifuatavyo.
i) Dhulumu
ii) Tubu

5 marks

7.

Andika ukubwa wa:
i) Mfupa
ii) Mbwa

5 marks

8.

Tunga sentensi sahihi ukitumuia vitenzi chwa na fa katika kauli ya kutendewa.

4 marks

9.

Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo uliyopewa. (alama 3)
i) Kati ya vitabu hivi vyote, Kiswahili murua ndicho kizuri zaidi cha kusoma.
(Anza: Kiswahili murua…….
ii) “kuna chai?” motto aliuliza. (malizia kwa…..chai)
iii) Nchi zinazoendelea hazina malighafi yoyote. (Anza : Malighafi …..)

4 marks

10.

Eleza matumizi ya ‘kwa’ katika sentensi ifuatayo.
Moja kwa tano ya watu waliosafiri kwa gari la moshi walikula wali kwa mchuuzi. (alama 3)

4 marks

11.

Bainisha viambishi katika neon lifuatalo
Waliotuhanhaisha

3 marks

12.

Kanusha:
Upendapo sahani nyingineyo, nitakupoa.

1 marks

13.

Tunga sentensi kwa kutumia neon ‘haraka’ kama
Nomino
Kielezi

1 marks

14.

Andika umoja wa:
i) Majadala yayo hayo ndiyo yaliyotumiwa kukusanyia takataka.
ii) Amkeni mwimbe

1 marks

15.

Bainisha na uonyeshe aina za viwakilishi katika sentensi zifuatazo
i) Yule ataajiriwa kazi huko mjini
ii) Cha kuvunda hakina ubani
iii) Wanene watahojiwa

1 marks

16.

Andika sentensi zifuatazo upya ukitumia kirejeshi ‘amba’
i) Nyoka aliyemuuma punda wangu ameuawa na wanakijiji waliofika kwa wingi.
ii) Mahali palipotayarishwa pamejaa waumini walitoka nchini kote.

2 marks

17.

Tunga sentensi moja moja ukitumia alama za kuafikisha zifuatazo.
i) Alama za dukuduku
ii) Mshangao

2 marks

18.

Akifisha.
Lo ni nini huyo anayeshambulia mwanangu jirani yangu aliuliza kwa hasira nyingi.

3 marks

4. ISIMU JAMII (Alama 10)

19.

a) Fafanua sifa bainifu tano za sajili ya siasa. (alama 5)
b) Fafanua athari za matumizi ya ‘sheng’ nchini (alama 5)

10 marks

Back Top