Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2015 KCSE Kericho West Joint Examination

Kiswahili Paper 3

SEHEMU A: (Alama 20)

USHAIRI - LAZIMA Soma mashairi A na B halafu ujibu maswali ya yanayofuatia,
1.

SHAIRI A:
1. Jaribu kuwa mpole, kwa wenzio darasani,
Jihadhari na kelele, na utusi mdomoni,
Wala siwe kama wale, wanafunzi maalum,
Wasio akili vichwani, katu usiwaingilie.

2. Ujifanyapo ja vile, watoto wale wahuni,
Juwa jatakwenda mbele, utashindwa mtihani,
Na toka dakika ile, utaingia mashakani,
Jaribu uwe twaani, mwanafunzi zingatile.

3. Mtoto kuwa mpole, nakueleza yakini,
Huwa ni mfahamile, wa elimu akilini,
Ni shida kuangukile, kushindwa na mtihani,
Yataka utamakani, mwanafunzi siliwale.

4. Mwanafunzi nakukanya, kwa yale mawi mwandani,
Sizowee kusengenya, sengenyo madarasani,
Kama hilo ukifanya, utakuwa mashakani,
Ni hayo nilowaonya, kwa hiyo nawaageni.


Shairi B
Aliniusia babu, zamani za utotoni
Kanambia jitanibu, na mambo ya nuksani
Na wala usijaribu, kwa mbali wala jirani
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Liche jambo la aibu, lipalo mtu huzuni
Liuvunjao wajibu, m’bora akawa duni
Lau chamba utatubu, kulipwa hukosekani
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Usipolipwa karibu, lakutoka fahamuni
Lazima lije jawabu, ingawa pindi mwakani
Japo kuwa ughaibu, au mwisho uzeeni
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Kila neno lina jibu, usitafute kwa nini
Mambo yenda taratibu, pupa jingi lafaani
Akopeshae zahibu, atalipwa zaituni
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Ahimilie taabu, hupata mema mwishoni
La raha au sulubu, malifi ni duniani
Mambo bahati nasibu, viumbe tahadharini
Malifu ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

1. a) Linganisha shairi la A na B kimaudhui. (alama 4)
b) Linganisha na kulinganua mashairi ya A na B ukizingatia sifa za kiarudhi. (alama 4)
c) Katika shairi la A andika ubeti wa nne kwa lugha tutumbi. (alama 4)

d) Taja na ueleze idhini ya mshairi ilivyotumiwa katika shairi A. (alama 4)
e) Fafanua maana ya mshororo ufuatao ulivyotumika katika shairi la B. (alama 2)
i) Kanambia jitanibu na mambo ya nuksani.
f) Eleza maana ya msamiati ufuatao. (alama 2)
i) Nuksani
ii) Malifi

20 marks

SEHEMU B: (Alama 20)

TAMTHILIA -MSTAHIKI MEYA - T.AREGE
2.

“---Hii harufu mbaya ya taka iliyoupamba mji wetu ni kiwakilishi cha uozo ulio ndani.”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Taja na ueleze mbinu mbili za kifasihi zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
c) Kwa kurejelea Tamthilia nzima eleza uozo ulio katika mji wa cheneo. (alama 12)

20 marks

3.

Viongozi katika tamthilia ya mstahiki Meya ni vielezo vya viongozi katika mataifa mengi ya bara la Afrika. Fafanua.

20 marks

SEHEMU C: (Alama 20)

HADITHI FUPI- DAMU NYEUSI- KEN WALIBORA na S.A MOHAMMED
4.

Jadili mbinu ya ishara ilivyojitokeza katika hadithi fupi ya Gilasi ya mwisho makaburini.

20 marks

5.

Kwa kurejelea hadithi zifuatazo jadili jinsi maudhui ya mgogoro yalivyoshughulikiwa. (alama 20)
a) Mke wangu
b) Tazamana na mauti
c) Ndoa ya samani
d) Mwana wa darubini

20 marks

SEHEMU D: (Alama 20)

RIWAYA YA KIDAGAA KIMEMWOZEA - KEN WALIBORA
6.

Eleza jinsi mbinu zifuatazo zilivyotumika katika Riwaya ya kidagaa kimemwozea: (alama 20)
a) Jazanda
b) Sadfa

20 marks

7.

“--- Wamechoka hadi ya kuchoka. Mtini nondo anapapatika kutoka kujinasua toka utandabui uliomnasa”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Ni masaibu gani yaliyowakumba wanaorejelewa? (alama 6)
c) Nondo anayejaribu kujinasua kutoka utandabui ni jazanda. Jadili. (alama 10)

20 marks

SEHEMU E: (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI
8.

a) Eleza maana ya maghani. (alama 2)
b) Taja sifa zinazotambulisha maghani. (alama 6)
c) Soma mtungo huu kisha ujibu maswali
Ndimi Kisoi, dume la ukoo mtukufu
Ulojipambanua kwa mabingwa
Wachezaji hodari wa ngoma
Ndimi dume liloingia nyanjani.
Makoo yakatetemeka
Yakang’ang’ania, gozi kusakata nami
Kijiji kizima kilinijua
Wazee walinienzi
Wakamiminiza kiamboni
Mabinti kunikabidhi
i) Tambua utungo huu (alama 1)
ii) Eleza sifa za mtungo huu. (alama 8)
iii) Eleza mbinu za kisanii zilizotumiwa katika mtungo huu. (alama 3)

20 marks

Back Top