Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2015 KCSE Gem Sub-County Joint Evaluation

Kiswahili Paper 2

1. UFAHAMU (Alama 15)

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia
1.

Binadamu kwa wakati huu amemaka kwa sababu amechafua mazingira yake pasipo tahadhari. Mathalani insi amejaza gesi za sumu zitokazo viwandani nahata kuchafua mito kutokana na maji machafu kutoka katika viwanda hivyo. Takataka zinazotupwa ovyo ovyobila simile. Matokeo ya haya yote ni kwa mfano , tunapata mvua ya aside ambayo huhasiri mimea. Aidha ukanda wa ozoni unaotukinga dhidi ya miale hatari kutoka kwa jua tayari umeharibiwa na hivyo kuongeza joto duniani. Sehemu nyingi zimeanza kugeuka na kuwa jangwa huku sehemu zingine zikifurika kwa maji ya mito na mvua. Maji haya yameanza kumezavisiwa vingi vilivyo baharini.

Kutokana na madhara haya,binadamu sasa anatapatapa ili kutafuta makao kwingine kwenye salama. Ndiposa siku hizi nadhari za binadamu zimeelekezwa katika mawanda mengine nje kabisa ya kisayari hiki kidogo kiitwacho Dunia.

Kwa miaka mingi sasa, binadamu amekuwa akitafakari kuhusu uwezekana wa kuishi sayari nyingine. Hii ndiyo sababu mwaka mwaka wa 1969 walimkanyagisha binadamu wa kwa kwanza kabisa mwezini.

Lengo lilikuwa kutalii na kuchunguza uwezekano wa binadamu kuishi huko na wale watakaoweza wahamie huko.

Kwa bahati mbaya, iligunduliwa kwamba mwezini hakuna kilicho hai huko, hata mimea. Mwezini ni vumbi tupu isiyootesha chochote. Kipatikanacho kwa wingi sana ni madini tu, ambayohayawezi kumfaidi binadamu kwa lolote.

Sayari nyingine alizozitalii binadamu ni zuhura, Mirihi, Mushtarii na tuseme karibu sayari zote zinazolizunguka jua. Kilichogunduliwa ni kuwa upo uwezekano wa sayari kama Zuhura na pengine Mirihi kuwa na mvua Lakini nyingi mno isiyoweza kuruhusu mimea kukua. Nayo, Zuhura inasemekana kuwa joto sana wakati wa mchana bali mirihi ni baridi sana siku zote;baridi kiasi cha kuwa binadamu na wanyama hawawezi kuishi huko. Mushtarii yasemekana kuwa joto ajabu, ambapo hizo sayari nyingine zina joto sana au zina baridi sana. Habari hii imefunga binadamu katika jela la kijisayari chake kiki hiki kiitwacho Dunia anachokichafua kila uchao.

Je, binadamu amekata tama? La hasha! Ndiyo mwanzo na anajaribu sana kuzikata pingu alizofungwana maumbile. Vipi? Amejaribu kuchunguza uwezekano wa kuihama ardhi na kuishi baharini kwa sababu bahari inazidi ardhi mara tatu kwa ukubwa. Ni vipi ambavyo binadamu anavyodhani anaweza kuishi baharani mahali ambapo hakuumbwa aishi humo kama samaki? Jawabu ni kuwa angefanya hivyo kwa kutumia maarifa yake.

Binadamu anaamini kabisa kuwa ana uwezo wa kujenga miji mikubwa humo humo baharini...mikubwa zaidi ya hii tuliyo nayo ardhini.Anaamini kuwa anaweza kuitawala bahari kiasialichoitawala ardhi, na hivyo basi kufanya bahari impe makao na kumlisha maumbile yake kwa kujiundia mashavu kwa mfano, ili avute pumzi ndani ya maji.

Njia ya pili ya kuepukana na pingu za maumbile ni kuishi angani. Hii ina maana ya kujenga miji iliyoelea angani, kama madungu vile. Na kwa vile anga haina kikomo, binadamu atakuwa amejipatia nafasi kubwa ya kuishi bila kujali ongezeko la idadi yake mwenyewe. Yaani atakuwa anajiundia visayari vyake visivyo idadi angani!

Njia ya tatu ni kubadilisha umbo lake ili asihasirike na joto wala baridi. Binadamu wa kisasa anaamini kuwa inawezekana kumuunda upya mtu katika maabara badala ya kufanya hivyo katika mimba. Mtu huyo wa maabara aitwaye cyborg kwa lugha ya kiingereza anaweza kuwa na chuma ndani badala ya mifupa na mwili wa kawaida wa udongo na maji nje.

Kiunde huyu atakuwa hadhariki ovyo ovyo kama binadamu wa sasa aliyeumbwa kwa chumvi, maji na protini. Ama kwa njia bora zaidi, binadamu mpya wa maabarani aundwe kwa zebaki. Binadamu huyu wa zebaki hafi wala hakatiikatiki na iwapo atakatika vipande vipande basi kama zebaki, vipande hivyo vitaundika tena upya na kumrudishia umbo lake kamili la awali.

Njia nyingi za kuepukana nauangamizi ni kutumia viunde vyake vya elektroniki kama vile tarakilishi yaani kompyuta na mitambo mengine kama hiyo. Binadamu anaamini kwamba uwezo wa vyombo hivi utakapokamilishwa, basi vitamsaidia kwa lolote lile.

MASWALI
a) Kwani kutumia mifano miwili,eleza vile ambavyo binadamu amechafua mazingira yake. (alama 2)
b) Ongezeko la joto duniani limeleta hali mbili kinzani za kimazingira, zitaje hali hizo. (alama 2)
c) Eleza sababu mbili zinazomfanya binadamu kuhangaika na kutafuta makao kwingineko. (alama 2)
d) Taja mambo mawili yanayomfunga binadamu katika ardhi. (alama 2)
e) Taja na ufafanue sababu tatu ambazo unadhani huyafanya madini yaliyoko mwezini yasiletwe hapa duniani.
(alama 3)
f) Eleza mambo mawili ambayo binadamu anajaribu kukwepa kulingana na aya mbili za mwisho. (alama 2)
g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (alama 2)
i mashavu
ii asihasirike

20 marks

2.UFUPISHO (Alama 15)

Soma habari ifuatayo kisha ujibu swali
2.

Kuteswa waandishi wa habari bahari na kuwekewa vikwazo katika kazi zao ni jambo ambalo si geni.Mara kwa mara visa vinaripotiwa vya wandishi kudhulumiwa na hata kuuwawa. Visa hivi vikiripotiwa ni nadra kuwaona Wahusika wakichukuliwa hatua za kisheria. Aghalabu ripoti zenyewe zinaishia kupuuzwa katika kapu la sahau.

Riwaya Dharau ya Ini,inamulika suala hili kina cha kikatiwa kauli. Hadithi tunakutana na waandishi wa habari ya maisha katika jamii yenye kani nyingi. Kazi ya waandishi hawa inaingiliana pakubwa na ya mwenyekiti Munene na mwenzake Waziri kisongo.

Lila na Derby ambao wanaandika gazeti la ‘Mpapure’ wanaendelea kufanya kazi yao kwa ujasiri mkubwa.Inafika wakati wanafichua kashfa ya kijiji cha Madongoporomoka . Kufichuliwa kwa kisa hiki hakuwapi waandishi hawa nafasi ya kuendeleza utafiti wao. Mhariri mkuu wa gazeti la ‘Mpapure’ BW.Silverstein Makhanu anawakataza kwa madai kwamba kina Lila ni wanawake na hawataweza kuendelea na utafiti huo. Kauli hii inamkarisha sana mwandishi Derby. Baadaye, hadithi, waandishi hao wanashtumiwa kwa kueneza uvumi na kuteswa.

Dharau ya Ini ni riwaya ya kifalfasa.Ni hadithi ambayo imeandikwa kwa lugha ya kuvutia. Ni kisa ambacho kimeshehen ucheshi mwingi. Ni riwaya ya kwanza katika fasihi ya Kiswahili kutumia msimulizi ya nafsi ya kwanza , ya pili na ya tatu kwa pamoja.

Pia, imeunganishwa tanzu zote za fasihi (tamthilia, ushairi, hadithi fupi na hata fasihi simulizi). Lakini msemaji wa kawaida huenda atatizwe na usimulizi ambao unasitasita kila baada ya dakika chache. Hata hivyo Dharau ya Ini ni mchango mkubwa katika fasihi ya Kiswahili.

a) Bila kupoteza maana, fupisha aya mbili za kwanza (maneno 55-60)
b) Fafanua jinsi waandishi Lila na Derby wanavyoteswa na sababu ya kuteswa.(maneno 30-35)

20 marks

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

Jibu maswali yafuatayo.
3.

i) Eleza maana ya kiambishi. (alama 2)
ii) Tambuishi uamilifu wa viambishi katika neno ‘kitakachotolewa’ (alama 3)

5 marks

4.

Toa mifano miwili ya sauti zifuatazo :
i. Sauti ghuna ambazo ni vipasuo.
ii. Sauti hafifu ambazo ni vikwamizo.

2 marks

5.

Eleza matumizi ya ‘kuwa’ katika sentensi hizi.
i. Alikuwa mgonjwa.
ii. Alikuwa akifua.

2 marks

6.

Tumia kihusishi cha wakati kisahihi katika sentensi.

1 marks

7.

Taja uamilifu wa maneno yaliyopigiwa mistari.

3 marks

8.

Andika udogo hali ya wingi.
Mvulana mkorofi alimkata mbuzi sikio kwa kisu kikali.

2 marks

9.

Fuata maagizo
i. Mgonjwa amepewa dawa asubuhi.
(kauli ya kutendesheka mazoea)
ii. Poa (nafsi ya kwanza wingi, wakati ujao kauli ya kutendeshana)

4 marks

10.

i) Eleza maana ya kishazi huru. (alama 1)
ii. Toa mfano wa kishazi huru. (alama 2)

4 marks

11.

Tumia neno ‘teka’ katika sentensi ili kutoa maana tatu tofauti.

3 marks

12.

Changanua sentensi ifuatayo kwa jedwali.
Magadi walichoma kanisa ni maadui wakubwa sana.

5 marks

13.

Andika katika usemi wa taarifa.
“Nitajificha mumu na shehe hatanipata leo, kesho hata mwaka ujao,” Kijuba alisema.

3 marks

14.

Andika visawe vya maneno yaliyopigiwa mistari.
Lupita ndiye alitakadamu upepelezi wa shamba hili.

3 marks

15.

Tumia maneno yafuatayo kutunga sentensi moja sahihi.

3 marks

16.

Andika maneno yafuatayo kutunga sentensi moja sahihi.
Mtoto wa sungura ameuawa.

3 marks

4.ISIMU JAMII (Alama 10)

17.

…mfanyikazi mmoja wa nyumbani amefikishwa mahakamani katika kaunti ya Maganyakulo kujibu tuhuma za kumbaka kikongwe. Mwendesha mashtaka wa polisi bwana Maliza Twende alisema.
Mikaka na Makarne alifumaniwa na mshtakiwa alipelekwa rumande hadi septemba 21 mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena. Licha ya hayo, wengi wanadokeza kuwa Huenda adhabu ya kosa hilo ikuwa ni kifo au kifungu cha maisha.

Mshtakiwa aliomba apewe dhamana na Serikali ili aachiliwe huru. Hatimaye ombi hilo halikukubaliwa kwa kuwa mfanyikazi huyo hakuwa na mdhamini. Muhimu ni kuwa baada ya kesi hiyo kuamuliwa, mshtakiwa anaweza kukata rufaa katika mahakama kuu. Naye mlalamishi ameomba Serikali impe ulinzi kutokana na kuvamiwa na washirika wa mshtakiwa…

Maswali
(a) Tambua sajili hii (alama 1)
(b) Taja sifa nne za sajili hii. (alama 4)
(c) Katika kifungu hiki kuna baadhi ya misamiati ambayo imetumika na aghalabu hupatikana katika sajili nyingine
tofauti na ile ya husika
i. Taja sajili hiyo nyingine (alama 1)
ii. Taja angalau misamiati minne iliyoko katika kifungu hiki na sajili uliyotambua katika c(i) (alama 4)

10 marks

Back Top