Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2015 Katulani Sub-County Mock

Kiswahili Paper 2

1. UFAHAMU (Alama 15)

Soma makalama yafuatayo kisha ujibu maswali.
1.

Tokea muundo mpya wa serikali ya ugatuzi uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita, kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwamsururu wa migomo na maandamano ya raia. Fujo za karibuni kabisa ni zile zinazoshuhudiwa katika miji mikubwa za wachuuzi na wafanyibiashara wakipinga hatua za serikali za kaunti kuwatoza ushuru takribani kwa kila huduma na bidhaa ikiwemo wanyama, kuku na ndege. La kuhuzunisha zaidi katika baadhi ya majimbo imeripotiwa kuwa raia wamelazimishwa kulipa ushuru kwa kutaka tu kuona maiti za jamaa zao kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti.

Wanasiasa wameonekana kuwa na wakati mgumu kutetea mfumo huu mpya wa ugatuzi huku baadhi wakisema kwamba matatizo yanayoshuhudiwa kwa sasa yametokana na ugeni wa mfumo huo. Wengine wameinyoshea kidole serikali ya kitaifa kwamba ndiyo inayosambaratisha muundo huu. Wengine wanahoji kuwa bado ni mapema na kwamba kunatajika muda mrefu ili kufaulu.

Ni wazi kwamba kumekosekana nidhamu bora ya kusimamia maisha ya raia nchini Kenya. Matatizo yanayokumba raia kwa sasa ni dalili kuwa mfumo wa serikali ya ugatuzi umeongezea chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu. Swali ni je, hadi lini nidhamu ya kusimamia raia itakuwa ni suala la majaribio na makosa?

Hatua ya kuwarundikizia raia ushuru mkubwa ni kitendo cha unyonyaji na cha dhuluma kinachofaa kupingwa. La kufahamishiwa hapa ni kwamba ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serikali zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi wa kibepari ikiwemo Kenya. Asilimia 90 ya mapato ya serikali za kibepari huegemea ushuru. Kwa hivyo hatua ya serikali za kaunti katika kuwanyonya raia kwa kuwalipisha ushuru si ajabu bali ni thibitisho kuwa jamii ya Kenya inaongozwa na nidhamu ya kiuchumi ya ubepari mfumo wa unyonyaji na ukandamizaji. Ukweli unabakia kuwa ndani ya serikali za kibepari raia ndio hubebeshwa mzigo wa ushuru unaoishia matumboni mwa viongozi!

Miito ya mabadiliko ya katiba na ya miundo mipya ya kiutawala si lolote ila ni moja tu ya hatua za mfumo wa kibepari kujipa muda wakuishi na kuziba aibu zake za kushindwa kusimamia maisha ya watu. Kufeli huku kwa mfumo huu kunashuhudiwa hadi kwenye nchi kubwa za kibepari kama Marekani na Uingereza hivyo nazo zimekumbwa tele na maandamano na fujo za raia wakilalamikia hali ngumu ya maisha.

Maswali

  1. Yape makala haya anwani mwafaka. (alama 1)

  1. Eleza mtazamo wa wanasiasa kuhusu utepetevu wa mfumo huu. (alama 3)



  1. “Ugatuzi nchini Kenya ni mfumo wa kibepari” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea makala. (alama 3)



  1. Migomo ni zao la matatizo yaliyogatuliwa kutoka kuu. Toa sababu nyingine zinazosababisha migomo katika serikali za ugatuzi (alama 4)




  1. Thibitisha jinsi mfumo wa ugatuzi umeongeza chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu (alama 2)


  1. Eleza maana ya maneno yafuatayo (alama 2)

i) Ugatuzi


ii) Kibepari


15 marks

2. UFUPISHO (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
2.

HAKI ZA BINADAMU

Binadamu wana mazoea ya kufikiria kuwa jinsi wafanyavyo, waongeavyo na wafikiriavyo kuhusu vitu ndivyo inavyopasa kuwa. Kama binandamu tunaamini njia yetu ndiyo sahihi, yenye mantiki na inayopasa kufuatwa na kila mtu. Msingi huu huu unakwenda kinyume na kutambua kila binadamu ana haki ya kufikiri, kusema au kuongea na kutenda mradi asikiuke haki ya mwenzake iliyo sawa na yake. Nguzo mojawapo inayogongomelea hoja hii ni Haki za Binadamu.

Azimio kutangaza Haki Bia za Binadamu liliafikiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Desemba 1948. Baraza kuu hilo liliyasisitizia mataifa wanachama umuhimu wa kuyasambaza, kuenezea, na kusisitiza kusambazwa kwa azimio hilo katika shule na taasisiza kielimu. Msingi wa uhuru, haki na amani ulimwenguni ni kutambua binadamu wote wana haki sawa. Ingawa kimsingi jamii na mataifa yote ya ulimwengu yanapaswa kuthamini, kusambaza na kuhimiza umuhimu wa Haki za Binadamu zipo jamii ambazo hukiuka haki hizo. Matokeo ya ukiukaji huu yana athari hasi sana kama ilivyotokea nchini Rwanda na Bosnia. Herzegovina kulikotokea mauaji ya halaiki.

Azimio la Haki za Binadamu linajumuisha vipengele kadha ambavyo ni mihimili mikuu ya Azimio lenyewe. Kipengele msingi kabisa kinasisitiza kuwa kila kiumbe anazaliwa huru na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine. Ukweli wa kauli hii ulikokotezwa na kauli ya mwanafalsafa maarufu Jean Jacques Rosseau aliyesema kuwa kila kiumbe huzaliwa huru lakini huwa katika pingu ulimwengu mzima. Kauli hii ilitambua ukiukaji huu wa kipengele hiki. Kipengele cha pili kinasisitiza kuwa binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubezwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia, utajiri au chochote kile.

Vipengele vingine vinatukumbusha kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi. Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa au unyonge wa kutumikishwa kwa namna yoyote ile. Suala hili linasisitizwa na kipengele cha sita kinachokataza kudhalilishwa kwa watu au kutunzwa kwa namna yoyote ambayo inamfedhehesha kama kiumbe. Azimio la Haki za Binadamu linasisitiza kuwa binadamu yoyote nyule ana haki ya kupata ulinzi wa kisheria. Binadamu huyo hapaswi kubaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa.

Hata hivyo sio watu wote ulimwenguni ambao wanazifurahia haki hizi za kimsingi. Zipo lukuki za jamiiulimwenguni ambako haki za kimsingi zinakiukwa. Katika nchi ambazo zinaongozwa na watawala wa kiimla, si ajabu kuona haki za binadamu zikikiukwa. Viongozi wa aina hiyo huwa wamegeuzwa ng’ombe wa shemere na tamaa, ubinafsi na ukatili usiojua thamani ya utu. Viongozi wa aina hii wanasahau kuwa kila binadamu ana haki ya kuishi maisha huru, asipotumikishwa wala kulanguliwa kama bidhaa.

Nchi za kiimla aghalabu huongozwa na itikadi kuwa kiongozi ndiye pekee ambaye ana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda. Watu wengine wanapaswa kumfuata kisilka kama yule mbwa wa Pavlov ambaye alitokwa na mate kila kengele ilipopigwa. Viongozi wa ama hii hawachelei kuwatenzanguvuraia zao: Kuwadhalilisha kwa namna nyingi. Viongozi wa aina hiyo huiona sheria ya nchi kama iliyowekwa kwa watu wengine bali sio wao. Msimamo huu unakwenda kinyume na kipengele cha saba cha Haki Bia za Binadamu kisemacho kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria.

Baadhi ya haki zinazokiukwa katika jamii za kimabavu ni haki ya watu kuungana, kuwaza, kushiriki katika maamuzi ya serikali, kuwa mwanachama wa jumuia waitakayo, kumiliki mali, kutembea, kuishi anakotaka kutohukumiwa bila ya kuwako na utaratibu wa kisheria. Ni muhimu hata hivyo kujua ni muhimu kwa raia wenyewe kujielimisha na kuzijua haki zao. Serikali inapaswa kuwa mlinzi wa sheria zenyewe. Lakini muhimu kujua pia kuwa mlinzi naye hulindwa pia.

Maswali

a) Kwa maneno kati ya 90 – 100 fafanua Haki Bia za Binadamu zilizoafikiwa na Baraza kuu la umoja wa Mataifa. (alama 10)

Nakala Chafu











Nakala Safi











b) Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadamu. (Maneno 50 – 60).

Nakala Chafu











Nakala Safi













15 marks

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

Jibu maswali yafuatayo.
3.

Tofautisha sauti zifuatazo.

/a/

/u/

2 marks

4.

i) Ngeli ni nini? (alama 1)


ii) Maneno haya yamo katika ngeli gani? (alama 2)

Tayo


Kipepeo


3 marks

5.

Akifisha sentensi hii kwa njia tatu tofauti kuleta dhana tatu tofauti.

Babu alimchapa nyanya






3 marks

6.

Ainisha mofimu katika neno lifuatalo

Sikumkaribisha





3 marks

7.

Andika katika usemi wa taarifa

“Mtapata mwaliko wenu kesho,” alisema Salim






3 marks

8.

Andika kwa wastani

Magoma hayo yatachezwa mawanjani.






2 marks

9.

Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari

Wanafunzi wenye bidii hufuzu mtihani.






2 marks

10.

Tofautisha sentensi zifuatazo.

i) Ningekuwa na pesa ningenunua simu nzuri

ii) Ningalikuwa na pesa ningalinunua simu nzuri






2 marks

11.

Tunga sentensi ukitumia vihusishi vya:

a) Kulinganisha


b) Sababu


c) Wakati


3 marks

12.

Kwa kutoa mifano katika sentensi onyesha matumizi mawili ya parandesi

2 marks

13.

Tambua kiima, shamirisho, chagizo na kiarifa katika sentensi ifuatayo

Nyanya alimjengea mjukuu nyumba kwa matofali mwaka jana.







4 marks

14.

Eleza tofauti ya kimaana katika sentensi hizi

i) Nisimamapo huchekwa

ii) Ninaposimama huchekwa






2 marks

15.

Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia ‘o’ rejeshi na kiambishi ngeli

mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo.






2 marks

16.

i) Eleza dhana ya kishazi tegemezi (alama1)





ii) Bainisha aina za vishazi (alama 2)

Konde iliyopaliliwa ilituletea mazao mengi sana





3 marks

17.

Tunga sentensi kuonyesha maana mbili za neno chuma .






2 marks

4.ISIMU JAMII (Alama 10)

Jibu swali lifuatalo.
18.

a) Eleza maana ya istilahi zifuatazo

i) Lafudhi (alama 1)







ii) Pijini (alama 1)







iii) Lahaja (alama 1)





b) Eleza njia tatu za kupunguza tofauti za kilahaja (alama 3)



















c) Fafanua sababu zozote zinazosababbisha makosa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili (alama 4)


















10 marks

Back Top