Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

2015 KCSE KASSU Joint Examination Test (Kabarak, Sacho, Sunshine)

Kiswahili Paper 3

SEHEMU YA A (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI- SWALI LA LAZIMA
1.

(a) Eleza sifa nne za kimtindo zinazopatikana katika methali za Kiswahili.(alama 8)
(i) Takriri:urudiaji wa maneno
− Bandu bandu huisha gogo
− Haraka haraka haina Baraka
(ii) Taswira (picha)
− Njia mbili zilimshinda fisi
− Paka akiondoka panya hutawala
(iii)Sitiari:mithilisha kitu kimoja na kingine moja kwa moja
− Mgeni ni kuku mweupe
− Ujana ni moshi
(iv) Kejeli/dhihaka
− Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
− Maskini akipata matako hulia mbwata!
(v) Balagha:maswali yasiyohitaji jibu kwa vile jibu ni bayana
− Umekuwa mumumenye kuharibikia ukubwani?
− Pilipili usiyoila yakuashiani?
− Angurumapo samba mchezo ni nani?
(vi) Tashbihi:ulinganisho kwa kutumia kilinganishi
− Mapenzi ni kama majani popote penye rotuba hujiotea.
− Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.
(vii) Kweli kinzani:hali inayopingana
− Mpanda ngazi hushuka.
− Kuinamako ndiko kuinukako
(viii) Chuku:maneno yasiyo ya kweli
− Polepole za kobe hufikisha mbali.
− Ukiwa makini utayaona macho ya konokono
(ix) Kinaya;kinyume na matarajio
− Ngoja ngoja huumiza matumbo
(iix) Tashihisi/uhaishaji/uhuishaji
− Sikio la kufa haliskii dawa
− Siri ya mtungi muulize kata {Zozote 4x2.sifa alama 1mfano1
(b). Eleza mbinu tatu ambazo hutumiwa kuzua misimu. (alama 6)
(i) Kutumia tanakali-neno mtutu_Bunduki/ hali ya kuachilia risasi
(ii) Utohozi wa maneno
Gava - Government.
Hedi - Head
Fadhee - Father
(iii)Maneno ya kawaida kupewa maana mpya
Toboa - faulu
Chuma - Bunduki
(iv) Matumizi ya tabdila
Njaro - Ndaro
(v) Kufupisha maneno
Kompyuta - komp.
(vi) Kutokana na umbo/rangi ya kinachorejelewa
Mfano Blue - Noti ya kitambo ya shilingi ishirini
Tangi - Mtu mwenye umbo nane
(vii) Ktumia isitara au jazanda
Golikipa - nyani

Mtu mlafi - Fisi
(viii) Kuunda maneno mapya kabisa;. mfano
Kuhanya - Usherati
keroro - Pombe
Kusikia ubao - Hisi njaa
Ni kubaya - hali si nzuri [ 3x2]
(c). Ni jukumu la jamii kudumisha fasihi simulizi. Dhihirisha. (alama 6)
− Kuendelea kufundisha Fasihi Simulizi shuleni
− Kufanya Fasihi simulizi kuwa hai kiutendaji kupitia shehere na halfa tofauti za kiserikali.
− Kuhifadhi tanzu mbalimbali ili vizazi vijavyo viweze kuzifahamu mfano kwa kurekodi.
− Kufanya utafiti wa kina kuhusiana na tanzu za Fasihi simulizi.
− Kuhakikisha kuwa lugha za kiasili hazififii kwa vile ndizo chanzo cha Fasihi Simulizi.
− Kuonyeshwa kwa fani mbalimbali za Fasihi simulizi kwenye vyombo vya habari kama runinga.
− Kuhimiza wanajamii hususan viongozi kuwasilisha ujumbe wao kwa kutumia fani za Fasihi simulizi kwa
mgano hotuba, ulumbi, mawaidha nk.
− Kuhimiza wanajamii kuionea fahari jadi hii na kushiriki kikamilifu katika matumizi ya fani mbalimbali mfano
mwiga.
− Kusisitiza uendelezwaji wa fani zake katika mashindano ya shule na hata baina ya shule tofauti kimaeneo na

20 marks

SEHEMU YA B (Alama 20)

HADITHI FUPI: Jibu swali la 2 au 3
2.

(a) Maskini, Babu Yangu.
− Jumuiya ya Wantantele walipinga ndoa kati ya wamidi ua makabila mengine (uk. 76)
− Babu maende alinawa kwa sababu ya ukabila. Kisa ni kuwa alikuwa anatembea na mjukuwe aliyefanana na
watentelo. (uk. 79) - mwizi wa mtoto.
− Kila wakati babu wake msimulizi alitaja neno ukabila, ni bayana kuwa jumuiya iliegemea mirango ya ukabila.
− Pia alitaja ufisadi, kuonyesha kuwa dhulumati walifisidi mali ya umma na kiwanyima waja huduma bora.
− Uongozi katika mtaa wa kochokocho, ambao ni mchafu. Hii inadhihirisha uongozi usiojali maslahi ya wananchi.
− Babu anapojaribu kujitetea kuhusu mtoto mdogo/mjukuwe hasikizwi, anauawa.
− Watu wa kochokocho walifikiri kuwa ni lazima Maende ameroga Msimulizi ndipo alimwita babu - wanamuua.
− Kulikuwa na utabaka, matajiri waliishi katika sehemu nzuri kule sakata, mitaa ya ghorofa wa maskini waliishi
mitaa ya madongoporomoka.


(b) Mwana wa Darubini.
− Kananda anajisiwa na mwajiri wake Mwatela na kimsababishia uja uzito.
− Anamdanganya kuwa angemuoa ili anyamaze na asimjulishe Maria ambaye ni mke wa Mwatela.
− Mwatela anampokonya mtoto, Mwakitawa na kusababisha utengano usiofaa wa mama na mwanawe angali
mchanga.
− Anamwuuza kwa dereva mmoja kutoka kongo ambako kananda anaelekea nchi asiyoijua wala kuwa na jamaa
wake.
− Dereva huyo baada ya kuishi naye na kumnajisi anamwuuza kama mtumwa.
− Mwatela aliwadanganya wazazi wa Kananda kuwa alikuwa ametoweka na hakujulikana aliko.
− Mwatela anampiga Maria, mkewe kila wakati anpokuja nyumbani mlevi Maria anapotaka kujua alikotoka.
− Mwatela anampa mtoto wake Mwakitawa kisu na hataki kumpiga nayo mamaye, Kananda kwa kisingizio kuwa ni
jasusi ambapo Mwakitawa anampiga Kananda nusura amuue.
− Mwatela anamweleza Mwakitawa kuwa kuna ‘adui’ au ‘jasusi’ ambaye alikuwa ni mamaye mzazi. Hapa
anamhadaa.
− Mwatela anafanya juu chini kumzuia Mwakitawa kuonana na mamake.
− Mwatela hamwelezi Mwakitawa ukweli kuhusu mamake.
− Mwatela si mwaminifu katika ndoa, anazini na Kananda bila mkewe kufahamu.
− Mwatela anakiuka haki za watoto kwa kumwajiri kananda kazi ya uyaya akiwa na umri mdogo.

Utahini

Maelezo ya neno ‘Dhulumati’ = al. 2
(Kila hadithi iwe na hoja 4 x 2) = al.16
Tanbihi hadithi moja iwe na hoja 5 zilizoelezwa vizuri. (alama 20)

20 marks

3.

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
− Maelezo ya mwandishi.
− Yanajitokeza kama mawazo/masimulizi yake Abu kuhusu mtazamo wake maishani.
− Liche ya kuzaliwa na kulelewa katika maisha ya uchochole anajibidiisha na kuyaboresha maisha yake. [ Zote 4x1]


(b) Fafanua mtazamo wake Abu kuhusu maisha.
− Kupata na kukosa hakutegemei uzawa. Licha ya Abu kuzaliwa katika umasikini halizinambadilikia baadaye
anapoinuka kiuchumi. Umasikini haumzuii kuimarika kichumi.
− Bidii na stahamala ndizo nyenzo za pekee za kujiinua. Abu amechorwa kuwa mto mwenye bidii ambaye alikuwa
na matumaini ya kupata riziki hivyo akajinyanyua kutoka kwenye uchochole.
− Vikwazo ni changamoto zinazotutia hamasa kujiimarisha. Kukataliwa kwake na Amali kunampamotisha ya
kufikia ufanisi hata mkubwa zaidi ya ule wa awali. Umaskini unamsukuma kutafuta jinsi ya kujikomboa.
− Ni wajibu wetu kuwashughulikia jamaa zetu. Anapotononeka kihali awakumbuka kuwajengea wazazi nyumba na
kuwatafutia nduguze ajira.
− Hapana pengine kama nyumbani. Baada ya kujiinua kiuchumi kule Uarabuni anarudi na kuekeza kwao
nyumbani.
− Mngwana hasahau alikotoka/asili. Anaporudi nyumbani hawasahau wenziwe waliokuwa wakifanya vibarua
pamoja. Anawapa ajira mara kwa mara ili kuwainua.
− Ndoa si ukubwa wa sherehe. Anaona vitu vingi anavyopaswa kuwa “wakweze’ ili kumwoa Amali kama
ubadhirifu. Haoni haja ya kuandaa harusi kubwa atakavyo Mama Zena.
− Ndoa inastahili kujengwa kwenye misingi ya ukweli. Anamkataa Amali anapotambua kiwa kukubali kwake
(Amali) kuolewa naye kulishinikizwa na tama ya utajiri wake.
− Mkemwema hutunukiwa mja naye Mungu. Anamwomba Mungu ampe mke mzuri ambaye angemchukua jinsi
alivyokuwa (bila kujali hali zake za kiuchumi).
− Kazi yoyote halali ni kazi mradi ikupe riziki. Abu anafanya vibarua vingi ili kujiimarisha kimaisha. Pia aendapo
uarabuni anafanya kazi ya uhamali. Habagui ajira.
− Ili kujijenga uchumi mja anapaswa kuwajibika pato. Anadunduiza fedha anazopewa uarabuni hivi arudipo kwao
anaweza kuekeza katika biashara ya uchukuzi.
− Utajiri/mali si kisingizio cha mtu kubadilika licha ya kupata mali nyingi anasalia kuwa myenyekevu kawa awali.
Habadiliki.
− Tunapofanikiwa inatujuzu kuwanyanyua wengine katika jamii. Anawaajiri vibarua wenzake katika kazi tofauti
tofauti alizozianzisha.
− Ndoa ni asasi muhimu katika kuindeleza jamii. Anafanya kila jitijadi kupata mke kama alivyotarajiwa kufanya na
jamii yake.
− Mustakabali wetu unadhibitiwa na Mungu. Mungu ndiye mratibu wa mambo yote. Anatumia Methali/msemo “ya
kesho ajua Mungu” ili kudhihirisha jinsi hali zilivyomwimarikia.
Hoja zozote 8 x 2 = alama 16

20 marks

SEHEMU YA C: (Alama 20)

RIWAYA KIDAGAA KIMEMWOZEA, Ken Walibora -Jibu swali la 4 au 5
4.

(a) Maneno ni ya mwandishi
Anaregelea Mtemi Nasaba Bora.
Sababu: Baada ya Mtemi kusoma barua aliyopata kutoka kwa mpenziwe Lowela ya kutisha
awaachilie Amani na Imani ili mapenzi yao yaendelee.
Mahala: Nyumbani kwake. (zote 4 x 1 = 4)
(b) (i) Methali:Mwiba wa kijidunga.
(ii) Tashhisi: Kijasho chembamba kumtekenya
(iii) Istiari: Mwiba wa kujidunga. (zozote 2 x 1 = 2)
(c) Umuhimu wa mtemi Nasaba Bora.
(i) Kielelezo cha viongozi wanaowadhulumu wananchi kwa kutumia mbinu za kikoloni.
(ii) viongozi wanavyotumia vyombo vya dola kuwanyanyasa wanyonge mf. Mauaji ya Chirchiri
Hamadi./Kupigwa kwa mamake Imam.
(iii)Ni kielelezo cha viongozi wanaotumia vyeo vyao vibaya m.f. kuwalazimisha wananchi kumchangia pesa mwanawe kwende kusoma ng’ambo.
(iv) Kupitia kwa Mtemi tunapata sifa za wahusika wengi. Mf Amani ni mwenye utu. [anamshawishi
Gadaffi asimmue Mtemi] (4 x 1)
(d)
− Amani na Imani kubadili imani ya wanasokomoko kwa kuyanywa maji ya mto Kiberenge.
− Amani na Madhubuti kuungana ili kupinga uongozi mbaya. Wanafichua uozo wa Mtemi na baadaye kugawia Dj,
MatukoWeye shamba.
− Amani na Madhubuti wanashirikiana kurejesha haki mahakamani kwa kutafuta mashahidi kumtoaYusufu
lawamani.
− Imani kubadilisha mtazamo hasi wa watu kuhusu walemavu.
− Imani na Amani wanamlea mtoto uhuru ili kuonyesha umuhimu wa haki za watoto.
− Dj. anabadilika baada ya kutoroka jela kwa kufanya kazi kwa bidii kwa Bw. Maozi ili kujitegemea.
− Amani anajenga nyumba yake mwenyewe ili kuonyesha umuhimu wa bidii, hategemei urithi.
− Amani anaendeleza amani baina ya wananchi ili kuleta mabadiliko .
− Kupitia kwa Amani, anatudhihirishia umuhimu wa kusameheana na kutolipiza kisasi.
− Amani anawaelekeze raia kuhusu uwajibikaji wao katika kuimarisha uongozi ,anawaonya dhidi ya kupuuza
ukatili.
− Madhubuti kukataa kushirikishwa katika ufisadi. Anataka kujitafutia kazi mwenyewe bila kutoa hongo.
− Chwechwe Makweche na vijana wenzake kuiletea nchi ya Tomoko sifa kwa kuichezea timu ya taifa kandanda.
(5 x 2 = 10)

(d)
− Amani na Imani kubadili imani ya wanasokomoko kwa kuyanywa maji ya mto Kiberenge.
− Amani na Madhubuti kuungana ili kupinga uongozi mbaya. Wanafichua uozo wa Mtemi na baadaye kugawia Dj,
MatukoWeye shamba.
− Amani na Madhubuti wanashirikiana kurejesha haki mahakamani kwa kutafuta mashahidi kumtoaYusufu
lawamani.
− Imani kubadilisha mtazamo hasi wa watu kuhusu walemavu.
− Imani na Amani wanamlea mtoto uhuru ili kuonyesha umuhimu wa haki za watoto.
− Dj. anabadilika baada ya kutoroka jela kwa kufanya kazi kwa bidii kwa Bw. Maozi ili kujitegemea.
− Amani anajenga nyumba yake mwenyewe ili kuonyesha umuhimu wa bidii, hategemei urithi.
− Amani anaendeleza amani baina ya wananchi ili kuleta mabadiliko .
− Kupitia kwa Amani, anatudhihirishia umuhimu wa kusameheana na kutolipiza kisasi.
− Amani anawaelekeze raia kuhusu uwajibikaji wao katika kuimarisha uongozi ,anawaonya dhidi ya kupuuza
ukatili.
− Madhubuti kukataa kushirikishwa katika ufisadi. Anataka kujitafutia kazi mwenyewe bila kutoa hongo.
− Chwechwe Makweche na vijana wenzake kuiletea nchi ya Tomoko sifa kwa kuichezea timu ya taifa kandanda.
(5 x 2 = 10)

20 marks

5.

(a) Uwajibikaji
− Amani anakilea kitoto Uhuru kama mwanawe baadaya Mtemi kukipagaza mlangoni kwake.
− Bi. Zuhura anawasaidia Amani na Imani kukilea kitoto Uhuru.
− Amani na Imani wanaishi katika kibanda kimoja lakini hawakiuki mipaka ya uhusiano wao.
− Imani anabadili mawazo yake kuhusu tendo la kujiua.
− Wafanyikazi wa Mtemi wanajitahidi kunadhifisha kasri.
− Amani anafunga safari ili kupata aliyemwibia mswada wake.
− Madhubuti anajitenga na ufisadi wa babake.
− Ben Bella anavunja uhusiano wake na Mashaka.
− Amani anafichua siri yake kwa Madhubuti kwa wakati ufaao.
− Amani na Imani wanafunga ndoa tu baada ya kukamilisha masomo. (10 x 1)
(b) Sadfa
− Kukutana kwa Amani na Imani pale ziwa Mawewa.
− Amani na Imani kukutana na Dj pale mto Kiberenge kisha anawapeleka kwa Mtemi.
− Amani kufika tu kwa Mtemi anapohitaji mchungaji.
− Majisifu kupata tu barua ya mwaliko wa kutoa mhadhara baada ya kubishana na Mkewe kuhusu ubingwa wake
katika uandishi.
− Bi.Zuhura anapomwita Amani chumbani kwake Mtemi anawasili.
− Amani anafika tu pale ambapo Oscar kambona anataka kulipiza kisasa kwa Mtemi.
− Amani na Imani kuajiriwa na ndugu.
− Amani na Imani wanakutana wakati tu wote wameharibikiwa na mambo.
− Dj anapita kibandani kwa Amani wakati Amani anawaza kuhusu kile kitoto Uhuru. Dj anaenda kumwita Imani
kumsaidia Amani.
− Kitabu anachopewa Amani kusoma pale pa Majisifu ni kidagaa ambacho ni kitabu chake.

20 marks

SEHEMU YA D (Alama 20)

TAMTHILIA: Jibu swali la 6 au 7
6.

(a)
Meya nyumbani mwake ili kumjulisha kuhusu matatizo ya wanacheneo.[4x1]
(b)
− Meya anawakilisha viongozi fisadi. Meya anatumia mali ya umma kujitajirisha mwenyewe.
− Meya ni kielelezo cha viongozi wabinafsi. Meya anajali maslahi yake na familia yake.anajipatia vipande vya
ardhi
− Meya anawakilishi viongozi dhalimu. Meya anawanyanyasa wafanyikazi wake kwa kulipa mshahara duni.
Anapuuza malalamishi ya wafanyikazi

− Yeye ni kielelezo cha viongozi wabadhirifu. Anatumia pesa za baraza ovyoovyo. Anapanga kuandaa karamu kubwa ya kuwalaki Mameya kuwa nchi za nje. Anaagiza vileo kutoka Urusi.
− Meya anawakilisha viongozi dikteta. Meya atambui maoni ya wanacheneo katika uongozi wake. Anafanya mambo kulingana na uwezo wake.[4x2]
(c)
− Unyanyasaji Meya anatumia askari wa baraza kuwanyamazisha wanacheneo
− Ufisadi-Meya anatumia mali ya baraza kujinufaisha.Alishirikiana na Bili na madiwani kuuza fimbo ya Meya.
− Ubadhirifu. Meya anatumia pesa za baraza apendavyo.anapanga kuandaa karamu kubwa na mapokezi ya mameya
− Udikteta analazimisha mambo. Hatambui mchango wa wanacheneo
− Udhalimu. Mstahiki meya anawadhulumu wafanyikazi wa baraza. Wafanyakazi wanalipwa mshahara mdogo pamoja na kufanya kazi katika mazingira mabaya.anawatisha wafanyikazi waliogoma kwamba baraza linaweza kuwafuta kazi na kuwapa vijana ambao walikosa kazi baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu.
− Mapendeleo. Meya anaidhinisha nyongeza ya mishahara kwa madiwani huku akiwapuuza wanacheneo[4x2]

20 marks

7.

(i) Kinaya
Tendo la baraza la Cheneo kuwaongeezea madiwani mshahara ni kinaya.Meya alikubali haraka kuidhinisha nyongeza ya mshahara ilhali wafanyikazi wa baraza wanaendelea kugoma kwasababu ya mshahara mdogo.
Meya anawadanya wanacheneo kuwa dawa ziko njiani.Ukweli ni kuwa Meya anafahamu kwa hali ya matibabu katika zahanati imedorora
(ii) Methali
Ngoja ngoja hii haisaidii matumbo. Siki anamwambia Diwani wa III. Siki anarejelea hali ya ukosefu wa dawa.
Haraka haraka haina Baraka-Waridi alidai kuwa Meya alisema alipoulizwa kuhusu kuchelewa kwa dawa Mtu huvuna alichopanda . Diwani wa III anamwambia Siki. Alikuwa akirejelea namna baraza lilivyoongozwa na mstahiki meya. Anamaanisha kuwa meya angevuna mazao ya Uongozi mbaya.
Kelele za chura hazimzuii ng’ombe kunywa maji-Bili alimwambia Meya baada ya sauti iliyodai wafanyikazi wapewe malipo bora. Ilimaanisha kuwa malalamishi hayo haingezuia meya katika kutekeleza mipango yake.
Majazi
Bwana Sosi – jina hili linaashiria mtu mwenye kupenda mlo.Alalamika wakati aliletewa viyai vidogo na Gedi mpambe wake.
Bwana sosi anapanga karamu ya kupigiwa mfano. Aliagiza vinywaji katoka urusi na divai kutoka Ufaransa.
Waridi- ua linalopendeza. Matendo ya Waridi yalionekana ya kuleta afueni kwa wanacheneo.Anawapa
wanacheneo matumaini kuwa dawa zingefika zahanatini.
Uzungumzi nafsia
Siki anajizungumzia akiwa ofisini mwake baada ya kupokea simu kutoka kwa Tatu. Anasema kuwa watu wenye njaa hawawezi kusikiliza chochote
Meya anasema na nafsi yake baada ya kuambiwa na Gedi kuwa mhazili wake amegoma.Alisema aligoma baada ya kupewa ajira.
[Ufafanuzi alama 1
Mifano 2x2=4]
Mbinu 4x5=20

20 marks

SEHEMU YA E: USHAIRI (Alama 20)

Jibu swali la 8 au 9
8.

(a) Shairi huru kwa sababu halina arudhi (alama 2)
(b) Kuonyesha jinsi kugombana ni kubaya na wagambanao huchoka na wakapatana
(c) Anatumia mshororo toshelezi na mshata (alama 2)
− Amepanga beti
− Ametumia maneno mateule kama vile neno vita
(d) Istiara
− Vipande vya matusi silaha zao
− Mabalagha - Ni nani anayekubali suluhu ?
− Nidaa - Huyo ! amshuke huyo! (3x1)
(e) Toni ya kukerwa - anaonyesha kuchukizwa na vitu hivyo (alama 2)
(f) Wamepatana baada ya kuamuliwa (alama 2)
(g) Kuonyesha hisia za mshairi (alama 2)
(h) Mtu /Nafsi ya tatu inayoshuhudia magombano (alama 4)
(j) ( i) silaha
(ii) malalamiko (2x1)
− Msanii anatuambia kuwa wakati wa jioni umefika

− Jua linapigia machweo kwaheri
− Giza linaingia kwa kishindo kikubwa (3x1)

20 marks

9.

(a) Ndege (alama 1)
(b) Mke nyumbani / mchumba (alama 1)
(c) Ukara - vina vya kati kubadilika vya kati vinatiririka
Mathnawi - vipande viwili
Tarbia - Mshororo minne (3x1)
(d)
− Mishororo minne
− Vipande viwili – ukwapi na tao
− Mizani 16 katika kila mshroro
Vima ri, ni
ri, ni
ri, ni
ni, wa (4x1)
(e)
− Tabdila - muruwa na heshima
− Inkisari ataka badala ya anataka
− Kuboronga sarufi - kama anavyo kubwa hasara (2x2)
(f) Mke mwema mwenye heshima nzuri ya kusifu , hata akifungwa atadhamini makao ana furaha kuishi kule .
Mke anayeishi nyumbani amezidiwa nguvu (4x1)
(g) Anashauri kuwa wake wanaishi katika ndoa ni wachache / wengi wana tama
(h) (i) atahama (1x2)
(ii) maneno (2x1)

20 marks

Back Top